Mfanyabiashara ashusha tuhuma nzito kwa RTO Arusha

Mfanyabiashara ashusha tuhuma nzito kwa RTO Arusha

Hahah mpk imebidi uwakariri majina mkuu.
Naunga mkono hoja yako,kuna wale Matrafiki wanawake wazee Anna (matege)na Rehema,ukilogwa ukawapa leseni,hawakuachii bila Ten.Lazima wakulazimishie kosa
 
Trafik Arusha nadhani ndio wanaongoza kwa kuchukua rushwa kuliko sehemu nyingi nilizopita unakuta wamekaa pale Philips nyuma ya mataa ni kukusanya rushwa tuu hasa kile kikosi kibachoongozwa na yule mwanamke wanatumia Nissan Chura harafu hapo hapo wanapokaa mbele taa ya kijani inawaka sekunde chache tuu wao hawashughuliki na kupunguza foleni ni usumbufu kwa kwenda mbele na wala rushwa wakubwa..
 
JWTZ wanakulaje rushwa?
Mkuu kwa utafiti wangu mdogo (na usio rasmi) nilioufanya.. Nimebaini kuwa wanaoongoza kwa rushwa nchi hii ni Ikulu, PCCB, CCM, TRA, Polisi, JWTZ, TPA, wakifuatiwa na wananchi wenyewe.
Kwa anayetaka kuhoji zaidi asubiri nitaanzisha uzi wa kuweka vielelezo vyote bayana..
Kwa hiyo hitimisho langu ni kuwa rushwa haitakaa iishe..
Muhimu ni mtu mmoja mmoja kupambania haki yake!
 
Green inawaka for 30 seconds,Red inawaka for 2 minutes.

Ujinga mtupu pale.
Trafik Arusha nadhani ndio wanaongoza kwa kuchukua rushwa kuliko sehemu nyingi nilizopita unakuta wamekaa pale Philips nyuma ya mataa ni kukusanya rushwa tuu hasa kile kikosi kibachoongozwa na yule mwanamke wanatumia Nissan Chura harafu hapo hapo wanapokaa mbele taa ya kijani inawaka sekunde chache tuu wao hawashughuliki na kupunguza foleni ni usumbufu kwa kwenda mbele na wala rushwa wakubwa..
 
Hi huwa najiuliza kwanini PCCB hawawakamati traffic police na wanasikia malalamiko ya wananchi kila siku, lakini pia mamlaka zinazohusika kwanini zinashindwa kuweka maeneo maalumu ya ukaguzi wa magari na maeneo hayo kufungwe CCTV cameras for transparency reasons?

Mimi naona tunatumia gharama kubwa kujifanya tynadhibiti hili mara lile wakati mambo hayo yangeweza kufanywa kisayansi zaidi ili kupunguza gharama za kuajiri wala rushwa

Teknoloji haina uwezo wa kuzia rushwa au upigaji
 
Rushwa ina njia mbili, aidha UNALAZIMISHWA utoe rushwa ili uachiwe kwa sababu unamakosa au unataka mambo yako yaende haraka au UMELAZIMISHWA utoe rushwa kwasababu umebabikiwa makosa au pia wanakukwamisha ili utoe rushwa.
Sasa wenye mabasi ya magari tuseme hawataki kutoa rushwa basi wahakikishe hawana makosa kwenye magari yao na Kama yanamakisa wkubali kutoa faini tu na sio zaidi. Na wenye mabasi wakizungushwa na kukwamishwa basi inabidi wafanye mgomo wa angalau siku mmoja tu. Na wenye mabasi wote waungane, ikitokea kwamba wamelazimishwa kutoa rushwa au wanazungushwa na kucheleweshwa hadi watoe rushwa basi hapo wafanye mawsiliano na wagome. Hilo suala nina uhakika litashughulikiwa mara mmoja. Na wakivabikiwa makosa wajitahidi kushibitisha kwamba hawana makosa, siku hizi kuna njia kibao ya kumnasa mtu. Si lazima umchukue video unaweza ukarekodi kwenye simu yako pia.

Huwezi ombwa rushwa kama huna makosa
 
Teknoloji haina uwezo wa kuzia rushwa au upigaji


Hakuna kinachoshindikana wataalam waki-invest kwenye kufikiri na kutatua matatizo, resources zielekezwe kwa watafiti siyo wanasiasa
 
Green inawaka for 30 seconds,Red inawaka for 2 minutes.
Ujinga mtupu pale.
Nilidhani wamekosea kwamba kuna siku watarekebisha kumbe hamna wao Trafik wanakaa mbele ya Taa na kukamata wanaopita na taa iwe hata ya njano ni ujinga ujinga tuu pale...
 
PCCB siku hizi inaongozwa na Mapolisi. Hii limefajika makusidi ili iwe rahisi kuihibiti na ipoteze uhuru wa kufanya kazi zake kulingana na sheria ya chombo hicho. Badala yake katika zama hizi PCCB inatakiwa kufanya kazi kama idara ya serikali tu na kwa maelekezo ya wanasiasa. Nadhani hii ndiyo ilikuwa sababu ya kumwondoa yule mkurugenzi mbobezi wa sheria. Kuna vyombo pendwa vya serikali ambavyo rushwa ndani yake imeongezeka maradufu na PCCB ķamwe haiwezi kuwagusa bila kuelekezwa.
Pccb nao wanavuta si mchezo. Hivi diwani athumani mnakumbuka madudu yaliyompa URAS miaka ile?
 
Mfanyabiashara na Mmiliki wa Mabasi ya kusafirisha abiria mikoani kutoka kampuni ya KIMOTCO ,Benedict Mberesero,amewalalamikia askari wa usalama barabarani katika Jiji la Arusha,kwa vitendo vya Rushwa iliyokithiri akidai wamegeuka mamlaka ya mapato TRA.

Akiongea katika kikao cha wadau wa usafirishaji jijini Arusha,mbele ya Kamanda wa Kikosi cha usalama barabarani Nchini,(SACP)Futunatus Musilimu, alimshutumu Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Arusha ,RTO Joseph Bukombe kuwa amekuwa kinara kwa kuongoza kikosi cha askari kukusanya Rushwa kutoka kwa wasafirishaji .

Amedai kuwa vibanda vya ukaguzi wa mabasi katika eneo la kituo kikuu cha mabasi jijini hapa ,vimegeuka vibanda vya kukusanya Rushwa kwa mabasi mbalimbali yanayoelekea mikoani na fedha hizo huwasilishwa kwa wakubwa .

"Napenda niseme ya Moyoni naona watu wamekuwa waoga kusema ,ukweli ni kwamba suala la Rushwa ni kubwa kwa Trafiki hapa Arusha naomba uchunguze mwenyewe ujionee" Alisema Ben

Aliongeza kuwa hivi karibuni alibambikiwa kesi ya matumizi mabaya ya Silaha ambapo alipigwa na askari wa usalama barabarani na kutupwa selo kituo cha Polisi kwa makosa aliyodai ni ya usalama barabarani.

"Namshukuru RPC alilishughulikia suala langu na bila yeye bila shaka ningekuwa nimefungwa kwa kubambikiwa kesi za uongo kwani si kweli kwamba Mimi nilitishia askari kwa silaha" Alisema .

Alimtuhumu RTO Bukombe kutoa ushirikiano pindi anapopigiwa Simu kwa nia ya kuomba msaada.

Akijibu hoja hizo ,RTO Bukombe Alisema tuhuma zilizoelekezwa kwake hazina ukweli Bali ni chiki zilizolenga kumchafua.

Alisema mabasi ya Kimotco yanaongoza kwa kuvunja sheria za usalama barabarani na pindi anapochukua hatua inaonekana kwamba RTO Bukombe mbaya na kuanza kumchafua kwa kusema askari anawatuma kukusanya Rushwa.

Ends.....View attachment 1145584
Rushwa na polisi haswa traffic nisawa na mizizi na ardhi
 
Huwezi ombwa rushwa kama huna makosa
Makosa yanakwepo na pia yasiwepo. Umekamatwa na trafic ukiwa na kosa na unatakiwa uliow 30000 au zaidi lakini huyo trafik na pokea 10000 tu na unaendelea na kazi yako, hili ni rushwa uliotoa kwa hiari yako, Na pia kuna badhi ya sehemu ambazo huna kosa lakini unakwamishwa na wahusika ili utoe rushwa ili ufanikishe masuala yako, hasa ni shufhuli za kiofisi Kama kufuatilia leseni au kabali.
 
Makosa yanakwepo na pia yasiwepo. Umekamatwa na trafic ukiwa na kosa na unatakiwa uliow 30000 au zaidi lakini huyo trafik na pokea 10000 tu na unaendelea na kazi yako, hili ni rushwa uliotoa kwa hiari yako, Na pia kuna badhi ya sehemu ambazo huna kosa lakini unakwamishwa na wahusika ili utoe rushwa ili ufanikishe masuala yako, hasa ni shufhuli za kiofisi Kama kufuatilia leseni au kabali.

Mkulima hula shambani,mwenye ofisi hula ofisi ni mwake
 
Back
Top Bottom