Jembe Jembe
JF-Expert Member
- Jun 9, 2016
- 757
- 1,822
MFANYABIASHARA Maarufu anayemiliki vituo vya mafuta jijini Arusha, Maganga Lago anatuhumiwa kumfanyia ukatili wa kutisha mfanyakazi wake wa ndani aliyetajwa kwa jina Moja la Teleza raia wa nchi Jirani kwa kumpiga na kisha kumchoma na pasi ya moto akimtaka kimapenzi.
Tukio hilo ambalo limeripokiwa kituo cha Polisi cha Muriet jijini Arusha na mtuhumiwa kukamatwa na kuwekwa mahabusu , anadaiwa kutenda unyama huo mwishoni mwa mwezi wa Aprili nyumbani kwake .
Inadai kuwa Maganga mara baada ya kuitwa kituo cha polisi Muriet alifanikiwa kuwarubuni polisi wa juu wa kituo hicho na kufanikiwa kumwachia ,ambapo Maganga aliamua kumsafirisha binti huyo ili kuelekea kwao kwa kwa wakala aliyemleta,ikiwa lengo ni kuficha ushahidi.
Hata hivyo inadaiwa kuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Arusha (RC0) alibaini mpango huo na kuamuru binti huyo aliyekuwa anasafirishwa kushushwa kwenye basi akiwa amefika eneo la Babati na kurejeshwa mkoani Arusha na sasa yupo chini ya jeshi hilo huku mtuhumiwa akiwa amepandishwa kizimbani .
Taarifa zinadai kwamba Maganga alimtaka kimapenzi kwa nguvu msichana huyo baada ya kugoma kumpa mshahara wake kwa sharti kwamba mpaka ampatie ngono lakini msichana huyo aligoma ndipo alianza kumshambulia na kumchoma na pasi huku akimtukana matusi kwa lengo la kutimiza haja yake.
Mmoja ya jirani na mfanyabiashara huyo (linahifadhiwa)alidai kwamba tabia za mfanyabiashara huyo kuwataka kingono wafanyakazi wake wakiwemo wa vituo vyake viwili vya Mafuta anavyomiliki ni jambo la kawaida .
"Huyu jamaa anatabia mbaya sana kila msichana anayemwajiri lazima amtake kimapenzi ndio maana hawakai anawabadikisha kama nguo kila siku analeta na kufukuza kuna mwingine alimpa mimba kablanya huyu akamfukuza ,na ukiona amemfukuza ujue amemkataa"Alisema jirani huyo ambaye aliomba jina lake kufichwa!
Alidai kuwa mfanyakazi huyo wa kike aliletewa kutoka nchi jirani ya Burundi lakini katika kipindi chote alichofanyakazi hakuwahi kumlipa mshahara wake akumshinikiza kufanya naye ngono.
"Siku ya tukio Teleza alitaka kulipwa fedha zake ili aweze kujikimu kwa baadhi ya mahitaji lakini Maganga aligoma kumpatia akitaka kufanya naye ngono ndio ampatie ujira wake lakini msichana huyo alikuwa mkali kudai haki yake ndipo Maganga alianza kumpiga na kisha kumchoma na pasi sehemu za mwili wake"
Akihojiwa na dhidi ya unyama huo Maganga alidai kwamba sio kweli kwamba alikuwa akimtaka kimapenzi msichana wake wa kazi bali alikuwa akidai mshahara wake wa miezi miwili ambao alikuwa amemtunzia.
"Unajua huyo msichana nililetewa kutoka sijui nchi gani na alikuwa akiishi hapa tunamhudumia na kulea kama mtoto wa nyumbani ikiwemo kumpatia mahitaji ,ila mshahara wake nilikuwa namtunzia mpaka siku akitaka kuondoka ndo nimpatie "Alisema Maganga.
Hata hivyo hakuweza kukataa ama kukubali kama alihusika na tukio la kumjeruhi kwa kumchoma na pasi msichana wake huyo.
Baadhi ya Mashuhuda walidai kuwa mfanyabiashara huyo amekuwa na tabia ya kufanya matukio hayo bila kuchukuliwa hatua kutokana na uwezo wake kifedha kurubuni vyombo vya dola na kumtaka waziri Gwajima mwenye dhamana hiyo kuingilia kati ili haki kuweza kutendeka.
Jitihada za kumpata kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha Justune Masejo ili kuongelea tukio hilo hazikufanikiwa baada ya siku yake kutopokelewa
Hata hivyo taarifa zinadai kwamba tayari jeshi la polisi limempandisha mahakamani mfanyabiashara huyo huku msichana huyo Teleza akipatiwa hifadhi maalumu na jeshi hilo.
Katika hatua nyingine Maganga anadaiwa kumfanyia ukatili wa kutisha mke wake wa ndoa mara baafa ya kumwamuru dereva wake amshushe kwenye gari porini wakati wakisafiri kuelekea Mkoani Singida .
Taarifa zinadai kwamba Maganga kwa sasa haishi na mke wake na kwamba mke amemfungulia mashtaka ustawi wa jamii kuhusu mali na watoto kesi hiyo ilikuwa inafanyika leo may 2,mwaka huu ofisi za ustawi wa jamii jijini Arusha
Ends.