Mzee Mwanakijiji,
Mkuu unajua unanishangaza sana...Hivi kweli wewe unaona picha hii ni jambo la kawaida kwa sababu yanatokea kila siku?..
Mzee unaniwekea maneno kinywani; kwenye jibu langu kwako nimesema hivi kuhusu hizo picha:
Sasa sijui wapi umeona nimesema au kuashiria kuwa hili "hii picha ni jambo la kawaida kwa sababu yanatokea kila siku"? Nitakuwa ninajipinga, kwani kama ninaona ni jambo la kawaida, why bother even bringing it to attention of more people? It'll defeat the purpose.
.umeshindwa kabisa kujiuliza maswali mengi kama alofanya Fundi Mchundo kutokana na picha hiyo badala yake unazungumzia kuvunja katiba isiyomsaidia mwananchi kitu chochote..
Sijui kama "nimeshindwa kabisa". Kuna maswali yanayoulizwa kwa maandishi na maswali yanayoashiriwa kwa picha. Tunajadiliana hapa kwa sababu nimefanikiwa watu kuhoji kile wanachokiona. Maswali yangu yanabakia pale pale kuwa hili ambalo tunaona "ni la kila siku" linapopata baraka ya Waziri Mkuu linatisha kuliko watu wanavyofikiria.
Nikisimama na kuangalia picha hiyo na kusikitika haitoshi. Siyo mimi wala wewe anayeweza kumsaidia huyo ndugu yetu aliyeuawa kishenzi hivyo. Hata hivyo tunaweza kuzuia mtu mwingine kuuawa namna hiyo. Hilo ndilo lengo langu katika mjadala huu. Sasa mtu anaweza akasikitika na kujisikia vibaya kuhusu picha hiyo lakini hilo halitoshi isipokuwa kuonesha utayari pia wa kuzuia jambo kama hilo kurudiwa tena.
Kwa kauli ya Pinda uwezekano wa matukio kama haya kutokea tena ni mkubwa kwani serikali imesema wananchi wachukue sheria mikononi wasisubiri mahakama!
Yaani wewe unakubali watu kama hawa waendelee kuyafanya wanayoyafanya nje ya katiba lakinim sio Waziri mkuu kusema kile mnachozoea kukifanya..
Nikikubali hivyo nitakuwa sina sababu ya kumpinga Waziri Mkuu, kwani kama Waziri Mkuu hawezi kuamuru kitu nje ya Katiba iweje tena nikubali Mtanzania kama huyo auawe nje ya Katiba? Ni ile ile contradiction, and I don't like contradiction.
Labda nirudie hapa, mauaji ya mtu huyo hayastahili, hayana sababu, na wale waliofanya vitendo hivi wanastahili kuchukuliwa hatua zote. Lakini zaidi ni watu wote wanaotengeneza mazingira ya watu kujichukulia sheria mikononi mwao kama alivyofanya Waziri Mkuu. Siungi uvunjaji wa sheria uwe wa Waziri Mkuu au wa mtu mtaani. Hakuna aliyejuu ya sheria.
ukasahau kwamba yeye ni relfection yako..
Huo msemo hauna ukweli kwa sababua ngekuwa reflection yangu angetetea Katiba au kupinga mauaji ya watu nje ya sheria. So, anaweza kureflect Watanzania wengine, lakini hanireflect mimi.
Mkuu wangu mimi sifikirii kabisa swala la mchawi kuawa kama huyu bali nafikiria hao Albino na huyu jamaa ambao tayari wamekwisha poteza roho zao kwa vitendo ambavyo ni pinzani na katiba...
Unaona wewe umesema "mchawi kuuawa" hilo hulifikirii (ina maana akiuawa mtu anayedaiwa ni mchawi haikusumbui)! lakini unasema akiuawa albino au huyu jamaa ndiyo unafikiria. Well, hapo ndiyo ninatofautiana na wewe.
Wakati wameuawa "majambazi" kule Kilimanjaro chini ya mikono ya Polisi nilisimama kama peke yangu kutaka uchunguzi ufanyike kwani taarifa zote zilionesha kuwa waliuawa execution style. Watu wakanipinga kwa sababu waliouawa ni Majambazi!
Hiyo tofauti mimi sina. Kwangu mimi mchawi, albino, mwizi wa kuku, n.k wote kwanza kabisa ni wanadamu. Hivyo napinga kabisa mauaji ya mwanadamu mmoja chini ya mikononi ya mwanadamu mwingine. Kuna exception mbili tu ambapo mauaji naweza kuyakubali. Yamefanywa kama kujikinga (aidha vitani, polisi, n.k kwa mujibu wa sheria za upiganaji) na pili kutekeleza hukumu halali ya mahakama. Nje ya hapo, mtu anayeitwa mchawi, ana haki ya kuishi kama vile kikongwe na albino aliyonayo.
Wananchi wamechoka kuishi ktk maisha ya woga na ndio maana wamechukua sheria mikononi mwao kwa sababu serikali imeshindwa kuwalinda..
Hiyo ndiyo pointi yangu pia, lakini kama wameshindwa maana yake wachukue sheria mikononi? Kama jibu ni ndiyo, kwanini tunajisikia vibaya kuhusu hii picha? Hapana, tatizo la usimamizi wa sheria ni kubwa mno na ni jukumu letu kuhakikisha hilo linafanyika.
Na hao Albino ni matokeo pia ya serikali kushindwa kuwalinda...hawa wote ni victims wa sheria butu na utamaduni mchafu ambao tunaujenga sisi wenyewe... kama alivyosema Fundi Mchundo hapo kuna watoto wadogo kabisa wakiona jinsi huyo mwizi akiuawa, haya picha hiyo nyingine hata Mbwa amekaa na huzuni, binadamu anapita akichukua picha tu.. Hii inadhihirisha wazi sisi ni watu wa aina gani...
Samahani mimi siko kwenye kundi la watu wa aina hiyo. Wapo watu wanaoona ni bora kukaa kimya mbele ya adversity kama hiyo mimi sipo hivyo. Siwezi kukaa na kuona mtu anauawa na mimi napiga picha, naangalia au nashuhudia bila kufanya kitu. Siwezi. WEngine wanaweza.
Nitashukuiru sana kama utafikisha ujumbe huu kwa waziri wa mambo ya ndani na vyombo vya Usalama nchini, bunge na pengine hata kwa rais ambaye anachukulia maswala haya YOTE kwa uzito mdogo sana.
.
Mzee, hili ni jukumu letu wote. Sisi wengine tunaongeza chumvi tu lakini sisi sote tunaweza. Kama Watanzania wakishika simu na kumpigia simu WAziri wa Mambo ya Ndani, Rais, Waziri Mkuu n.k wanaweza kujua nini kinaendelea. Lakini guess what, watu hawatafanya hivyo. Hawatathubutu kufanya hivyo. Sijui ni kwanini?
Nitakuomba tena jaribu kujenga ujumbe wapo na kuelekeza nguvu zako ktk kuondoa mauaji kama haya iwe Albino au wezi kwani sheria ni msumeno..unakata pande zote isiwe OK kuuawa kwa Albino lakini watuhumiwa hadi sheria itumike..
Let's stop the kilings za hawa watu kwanza kisha ndio tuta worry kuhusiana na katiba.
.
Hatuwezi kusimamisha mauaji haya nje ya Katiba, period.
tuweke nguvu zetu ktk kusisitiza serikali na vyombo vyote vya haki za dunia kutupia jicho mauaji kama haya ili viongozi wetu wapate kuwajibika...
Hawawezi kuwajibika nje ya sheria.
Je, sio sisi tuliokuwa tunaunga mkono Israel inayoyafanya huko Palestina mbona hatuombi sheria itumike!..
Sakata la Palestina mimi sikulitolea maoni. Hivyo sijui kwa kweli ni nani aliunga mkono mambo ambayo Israeli ilikuwa inafanya au mambo ambayo Hamas ilikuwa inayafanya.
tunajenga hoja kwamba mchokoizi ni nani na nani mwenye haki ya kujilinda tena tunaipa hata sharia kikatiba leo Pinda kusema tu wauaji nao wauawe imekuwa swala la kukamatia kiasi hiki mkuu wangu..
Sina la kusema kwenye hilo kwani sikutoa hoja yoyote kuhusu suala la Palestina na Israeli. Nitaawacha wengine waliofanya hivyo wajibu.
terrorist wanauawa na viongozi wa nchi zote za magharibi wametuma majeshi yao kuua hawa terrorist iweje tuone haki matendo kama hayo lakini sio usemi wa Waziri wetu mkuu inapofikia swala la wachawi au kwa sababu hawa ni ndugu na jamaa zetu..
Waziri Mkuu wetu ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania siyo wa Israeli au Palestina. NInajali yanayotokea Tanzania, haya mengine ya kimataifa nayaweka kwenye maudhui yake. Siwezi kumlalamikia Omert wala Abbas wala kutaka wao wawajibike. Ni jukumu la watu wao kufanya hivyo. Mimi wa kwangu ni Lowassa, Idris, Kikwete, Chenge n.k !
Mkuu hawa wachawi na watu wote wenye imani za kichawi ni home grown Terrorist,
No sir.. mchawi ni terrorist!? That is a leap I'll not dare to attempt. Kwa sababu kuliko Shinyanga wanasema wazee vikongwe wenye macho mekundu ndiyo wachawi, nikikubali hoja yako kuwa wachawi ndiyo homegrown terrorists nitakubali kuwa vikongwe =>Wachawi=>terrorists.. No sir I DO NOT AGREE.
now how to deal with them ni shangamoto nalotaka sana kulisikia badala ya hizi habari za Pinda wakati Albino wanaendelea kufa kila siku...
Nimeshatoa mapendekezo yangu, na jana nimepata confirmation yamefika na yameanza kufanyiwa kazi. Bado nafikiria kushiriki kwa namna nyingine zaidi lakini vyovyote ilivyo siko tayari kuacha sheria au Katiba ipuuzwe au kuchezewa kana kwamba is optional.
Samahani mkuu wangu unajua inaniuma sana kuona picha kama hizi kwa sababu ni kitu kinachotokea kweli.. sifikirii kesho itakuwa vipi kutokana na maneno ya Pinda kwani ombi lake yawezekana kabisa isitokee... kwa mazingara yetu sisi wote woga wa wachawi!
Sidhani kama wote ni woga wa wachawi. Mimi siogopi wachawi, sitetemeki mbele yao na hakuna lolote wanaloweza kufanya kwa kutumia ndumba na tunguri zao kunidhuru mimi. Hivyo wengine wanaogopa mimi siwaogopi kwani sina sababu ya kuwaogopa. And believe me, I know what I'm talking about.