Mfano wa unyama utokeao kama utekelezaji wa lililokuwa agizo la Mh. Pinda (Graphic)

point ni kwamba kwa tamko la pinda, ni kuipa tabia hiyo legitimacy. Ni kukubali kuwa hatuna utawala wa sheria, ni kusema kuwa watu "wakichoshwa" basi wachukuwe hatua papo kwa papo dhidi ya wale wanaosababisha hisia hiyo ya kuchoshwa. Hoja ni kwamba, awe mwiba mbuzi, mgoni, au muuaji (haijalishi anayemuua nani) sheria ni lazima iwe dikteta. Tukiweka exception (kama ilivyofanya serikali) kuwa anayeuwa albino basi naye auawe papo hapo hapo basi tunakuwa tumehalalisha uvunjaji wa principle.

Na kama Nyerere alivyosema ukiivunja kanuni kubwa, basi kanuni hiyo itatafuta njia ya kukuvunja..! I know.. he was right.

Mwanakijiji, inawezekana Pinda alikuwa akikikubali kile ambacho wengi labda hatutaki kukikubali, nacho ni hatuna utawala wa kisheria na umetushinda.....
 
This is not dying peacefully....how can you die peacefully after being on a receiving end of such a beating?

Wakati niko Secondary, wakati wa likizo fupi, nilichukua train kutoka Dodoma kwenda Dar. Ndani ya behewa tukakuta kikundi cha Waimbaji kwaya kutoka Kilosa ambao ndiyo walikuwa wanarudi Kilosa kutokea Mwanza walikokwenda kutembelea waumini/kanisa la huko. Alikuwemo jamaa mmoja mzinga wa mtu na kavaa lile "Over-roll" lenye Mikanda kama yule babu wa KASSAV. Kufika njiani na ule uchovu huku behewa la thirdclass(kajamba nani) likiwa limejaa kama kawaida enzi hizo, nilianza kusinzia huku nimesimama. Pembeni akawa amesimama yule mzinga wa baba wa Kilosa. Sijui nilikuwa nasinzia vipi ila jamaa ghafla akaanza kufoka kuwa kaniona tangu zamani sana. Najifanya nalala kumbe nataka kumwibia. Alikuwa anasubiri tu niingieza mkono anidake. Ila nafikiri hili zaozi lake alisubiri muda mrefu hadi akachoka na kuamua kurusha kombora la kujihami ili hata kama mimi ni mwizi, basi ajue kuwa ameshanistukia.
Siku hiyo nilijua kuwa ntauwawa. Bahati mbaya hata kwenye behewa walikuwemo wanafunzi wachache sana, wengi walikuwa wasafiri kesho yake. Mungu bariki watu hawakununua maelezo yake. Nilijitetea kwa kumwambia kuwa mie ni mwanafunzi na si KIBAKA. Nilitoa na kitambulisho changu na kumpa asome. Na nikamwambia leo tumefunga shule na nitaenda Pasaka nyumbani. Yule baba alijisikia aibu sana kwani maelezo yangu yalikuwa na ukweli sana. Mwanafunzi mwenye kitambulisho tena cha shule nzuri tu inayofahamika enzi hizo unaheshimika sana.
Huwa nikisikia au kuona picha za Vibaka wameuawa kwa kweli zinanikumbusha hilo tukio. Sijui wangenipiga hadi kufa? Sijui wangenirusha dirishani usiku wa manane? Sijui wangelini........ I wish ningelimpata huyo baba wa Kilosa...... tena anajiita MSABATO.

Hicho kwa kweli hakiwezi kuwa KIFO CHA AMANI maadamu hadi leo hii nakumbuka na ni miaka mingi sana. Pana wakati POLISI walikuwa wanakamata watu wanaochoma watu. Ila kwa hali iliyopo, POLISI ndiyo wanahodhi MAJAMBAZI kazi ipo. Duuu, CCM kweli KIBOKO.

NB: Nyani, Thanx!!!!!!
 
Mimi nadhani kitu kinachosababisha mauaji haya kuendelea ni kuchoka kwa wananchi kutokana na urahisi wa washitakiwa kupata dhamana (Mahakamani ama Polisi) kwa urahisi. Mahakama na Polisi hawana synchronisation zinazoweza kujua washitakiwa wana historia gani katika makosa mbalimbali wanayoshitakiwa nayo, na hivyo kusababisha washitakiwa hao kupewa dhamana kwa urahisi.

Naamini kama mtu akishitakiwa kwa kosa la wizi ama kosa jingine lolote, akapewa dhamana halafu akarudia kosa lile ama jingine, inabidi asipewe dhamana tena hadi atakapopata hukumu yake mahakamani. Utaratibu wa jeshi la Polisi kuruhusiwa kukubali udhamini kwa wakosaji, nadhani pia unachangia mambo haya kuendelea na si ajabu yakafikia mahali yakatushinda kabisa.

Mahakama inabidi iwe ndio chombo pekee chenye mamlaka ya kutoa dhamana kwa washitakiwa wa makosa yote kwa kuzingatia pamoja na mambo mengine, utii wa dhamana kwa washitakiwa hao. La sivyo, wananchi wataendelea kuchoshwa na wakosefu hao, na wao watachukua sheria mikononi kila kukicha.
 
Thats more than too much. rapid constitutional changes are of more imporatace! We must by any means insist serious rule of law! Delaying that.........its planting the seed of our own destruction.
 
Kama baadhi ya wabongo wana hasira kweli na kuibiwa basi wangewachoma moto na kuwaua majambazi halisi nchini mwetu ambao ni MAFISADI. Huu ni unyama wa hali ya juu wanaowafanyia raia wengine kisa tu mtu kaiba mbuzi au cell phone. Kama ni wajanja kweli wakawatafute kina Mramba, Yona , Chenge, Mkapa, Liyumba NA MAFISADI wengine wote na kuwachoma moto mpaka kuwaua. Mimi nataka mtu ambaye atarekodi mauaji ya hawa vibaka wadogo na tuyatangaze kwenye vyombo vya habari duniani kama ilivyo kwa mauaji ya albino.

Ni Tanzania pekee ambapo JAMBAZI KUBUHU LA KIFISADI lililoiba mabilioni ya shilingi linatanua mtaani na kibaka mdogo aliyeiba kuku au cell phone ya shilingi 50,000 anauawa. Baadhi ya wabongo ni watu wa ajabu sana na hawana utu kabisa.
 
Mimi nimewahi kushuhudia. Usiku moja nikiwa nimelala nyumbani kwangu Makumbusho niligutushwa na sauti na kelele za mwizi, mwizi. Kuchungulia dirishani niliona kundi la watu likimpa kibano kijana moja nje ya geti langu. Niliamka na kutoka nje na nilipolikaribia geti nikanasa baadhi ya maneno ya hao jamaa - walikuwa wamemkimbiza mwizi wao kutoka Mwananyala. Niliogopa nilipoona silaha walizokuwa nazo kuanzia magongo hadi mapanga. Taratibu nilirudi ndani na sikuweza kulala tena - usiku mzima mlio wa hofu wa yule kijana ulitanda masikioni.

Pamoja na kuwa na kawadia ya kuwahi kazini, asubuhi nilishindwa kutoka kitandani kama siku zote - hivyo nilipiga simu nikamwambia bosi wangu kuwa nilijisikia vibaya. Sikufungua geti langu mpaka saa tatu na nilipotoka nje nilishangaa kuona maiti bado ipo pale pale na watu walikuwa wanapita kama vile hawaioni. Nilirudi ndani na sikutoka tena mpaka saa saba mchana nilipochungulia na kuona gari la polisi limefika !! Kama kuna kitu sitakisahau ni hizo sura za hao waliokuwa wanamsulubu mtuhumiwa - zilikuwa si za binadamu - zilikuwa za viumbe visivyo na huruma - wanyama. Is this what Pinda was advocating ? - God forbid !!!
 
Last edited:
Kama kuna kitu sitakisahau ni hizo sura za hao waliokuwa wanamsulubu mtuhumiwa - zilikuwa si za binadamu - zilikuwa za viumbe visivyo na huruma - wanyama. Is this what Pinda was advocating ? - God forbid !!!

Mag3

Una BAHATI umeona hizo sura za wauwa vibaka. Ukija pata MKOSI wa kuona wale wanaokatakata vipande vya Albino na kuviweka ndani ya mfuko na kuondoka navyo, basi kuanzia siku hiyo utakuwa VEGETERIAN. Na kibaya zaidi ukipata balaa kubwa kabisa kabisa la kumuona MGANGA WA KIENYEJI akichukua viungo hivyo, kuvichoma na KUVIPONDAPONDA ili iwe dawa, hapo ndipo utachoka kabisa. Shilingi ina Pande mbili - PINDA!!
 
Mkuu wewe utakuwa na taarifa muhimu sana, yaani unajua mpaka treatment ya viungo vya albino inavyokuwa kwa nini usimsaidie pinda hawa watu wakakamatwa badala ya yeye PINDA kutoa agizo linalopingana na kiapo chake?
 
Ilitakiwa iwe fundisho kibaka akiuliwa mtaani kwenu mtaa mzima mahakamani
Yale yale!!!.Utamadununi huu mbaya kwa maoni yangu umetokana na mambo kadhaa.Moja kuchelewa kwa vyombo vya ulinzi hasa polisi kushukulikia upelelezi ili mtuhumiwa apate adhabu yanayostahili.Pili mahakama zetu kuchelewasha kesi ili mtuhumiwa apate adhabu yake.kutokana na sabu hizi wananchi hukosa imani na vyombo hivi na kuamua kuchukua sheria mikononi mwao.Ingawa kweli ni kwamba udhaivu wa vyombo hivyo nao unatokana na upungufu wa watumishi kwa maana askari na mahakimu. upungufu wa vitendea kazi nk nk
 
Mag3

Una BAHATI umeona hizo sura za wauwa vibaka. Ukija pata MKOSI wa kuona wale wanaokatakata vipande vya Albino na kuviweka ndani ya mfuko na kuondoka navyo, basi kuanzia siku hiyo utakuwa VEGETERIAN. Na kibaya zaidi ukipata balaa kubwa kabisa kabisa la kumuona MGANGA WA KIENYEJI akichukua viungo hivyo, kuvichoma na KUVIPONDAPONDA ili iwe dawa, hapo ndipo utachoka kabisa. Shilingi ina Pande mbili - PINDA!!

Sikonge

Tofauti ni kuwa Pinda kama Waziri Mkuu anatoa baraka kwa vitendo ambavyo havina tofauti na vilivyotendwa - ambavyo vyote ni upotevu wa maisha na uvunjaji wa sheria. Je Pinda atakuwa anatabasamu akiona na kushuhudia huyo mtuhumiwa wa mauaji akisulubiwa hadharani ? Naomba unielewe - siwaonei huruma wauaji wa Maalbino hata kidogo - pia kuna wachuna ngozi, wauaji wa vikongwe, vichanga na wenye upara kama mimi !!
 
Hapa mkuu Shy unakuwa extremist. Mtaa mzima? Thats too much!

Anywayz. Nadhani ni rahisi kulaani kwasababu we have every right to do so. Kuua kibaka kwa kosa la wizi sio sahihi. Kujichukulia sheria mkononi kwa kifupi sio sahihi. Lakini kwa wale ambao mmeshakumbwa na wizi wa vibaka au majambazi, mtakubaliana na mimi (japo kwa shingo upande) kwamba some vibaka na wezi deserve to die. Yes, its against humanity and human rights, lakini kama alivyosema Pinda, inatia uchungu sana. Just imagine wezi wanakuja nyumbani kwako, wanakukamata wewe baba mtu wanakuingilia kinyume na maumbile mbele ya mkeo na watoto, wanamuingilia mkeo mbele na nyuma etc mbele yako na watoto. Hii inauma kiasi gani?

Katika hali hii, leo na kesho, nikisikia mwizi anakimbizwa nyumba ya jirani, natoka na kiberiti na petrol kabisa. Because I strongly believe hawa watu wanastahili kifo tu. Sheria inapindishwa pindishwa mno. Hawa watu hawaadhibiwi vya kutosha. Wengi wanaachiwa tu muda mfupi baada ya kukamatwa. Wananchi wamechoka. Nadhani wale ambao wamewahi kuibiwa na kufanyiwa ubaya will share the same sentiment.

Zero naungana nawewe asilimia 200%, tatizo hapa sio Pinda pinga anaingia lawamani kwa kuwa ni Kiongozi wa Taifa kimsingi alifanya blunder kusema vile. Hata hivyo swala la jino kwa jino lilishakuwepo kwenye fikra za wananchi kama ulivyoeleza. Kwa kweli aliyewahi experience wezi wa Tanzania hawezi kabisa kuwa nahuruma na vifo vya wezi. Hawajamaa kwanza wakija nikama wapo vitaana amazake amazako. Uzembe wa vyombo vyadola pia unachochea adhabu hii kwani watu hawa polisi wakienda wanaachiwa bila adhabu ya maana na wakirudi mtaani wanahakikisha wanalipa kisasi kwa waliowafikisha katika vyombo vya dola. Hii ndio sababu mimi na wengine tunaunga mkono adhabu hizi mpaka hapo vyombo vya dola vitakapokuwa na uwezo wa kudhibiti wezi na kuwashughulikia. Tukiwavumilia tutakufa sisi tunaochangia significantly katika uchumi wa nchi na kuwaacha wanaotafuna uchumi wa nchi wakiwemo vibaka na wezi wengine.
 
Mimi nadhani kitu kinachosababisha mauaji haya kuendelea ni kuchoka kwa wananchi kutokana na urahisi wa washitakiwa kupata dhamana (Mahakamani ama Polisi) kwa urahisi. Mahakama na Polisi hawana synchronisation zinazoweza kujua washitakiwa wana historia gani katika makosa mbalimbali wanayoshitakiwa nayo, na hivyo kusababisha washitakiwa hao kupewa dhamana kwa urahisi.

Naamini kama mtu akishitakiwa kwa kosa la wizi ama kosa jingine lolote, akapewa dhamana halafu akarudia kosa lile ama jingine, inabidi asipewe dhamana tena hadi atakapopata hukumu yake mahakamani. Utaratibu wa jeshi la Polisi kuruhusiwa kukubali udhamini kwa wakosaji, nadhani pia unachangia mambo haya kuendelea na si ajabu yakafikia mahali yakatushinda kabisa.

Mahakama inabidi iwe ndio chombo pekee chenye mamlaka ya kutoa dhamana kwa washitakiwa wa makosa yote kwa kuzingatia pamoja na mambo mengine, utii wa dhamana kwa washitakiwa hao. La sivyo, wananchi wataendelea kuchoshwa na wakosefu hao, na wao watachukua sheria mikononi kila kukicha.

Ni kweli lakini Mkuu ukumbuke kwamba utunzaji wetu wa kumbukumbu sio mzuri. Kwa hiyo wakati mwingine sio rahisi kwa hao polisi kuweza kuwa na kumbukumbu na uhalifu wa mtu fulani. Kwa mfano mtu kafanya uhalifu tegeta na taarifa zake zikapelekwa/zikaandikishwa hapo tegeta na akapata dhamana polisi, baada ya muda wa siku kadhaa huyu huyu mtu akafanya tena uhalifu Tabata taarifa zake zitakapopelekwa hapo Tabata kituoni,hawa walinda amani hawatakuwa na kumbukumbu yoyote ya tukio la mtu huyu alilolifanya Tegeta na kwao itakuwa bado rahisi kumpatia dhamana.
Mie nadhani mpaka tutakapoweza kuwa na mfumo mmoja ambao ni bora wa kutunza kumbukumbu za waalifu wote kwenye mtandao wa komputa kwa walinda amani/polisi na kila kituo kikiunganishwa na vingine kwa mtandao wa komputa itakuwa rahisi kuweza kubaini kama huyu mtuhumiwa kafanya kosa wapi na kama bado ana kesi ya kujibu au la.
 
Juzi juzi kuna dada mmoja alikabwa na vijana pale daraja la mto kizinga kuelekea Mbagala, wale vijana walimchana chana vibaya dada wa watu kwa wembe.. bahati nzuri kuna watu wakajitolea kumsaidia wakamkamata kijana mmoja.. Kilichotokea hapo mmmmh mpaka sasa sitaki tena nyama..... Yule kaka alipigwa vibaya sana, wakamchoma macho kwa bisibisi, wakamkata viganja vya mikono, walipoona amechoka yuko hoi wakammwagia petrol, wakamchoma... Kusema ukweli ilitisha sana, mbaya zaidi polisi walikuwepo hata hawakusaidia mpaka walipoona ameteketea kabisa ndo wakaenda kubeba mzoga uliobaki. Kuna mama akauliza kwanini walifanya vile badala ya kumpeleka post tu maana ni karibu, walimwambia yule mama akae kimya maana hajawahi kuibiwa eti wamechoka maana polisi wanakula njama na wale vijana, hata wakiwapeleka unashangaa kashatoka.... Cjui tunaelekea wapi, Mungu atuhurumie.
 
Mkuu wewe utakuwa na taarifa muhimu sana, yaani unajua mpaka treatment ya viungo vya albino inavyokuwa kwa nini usimsaidie pinda hawa watu wakakamatwa badala ya yeye PINDA kutoa agizo linalopingana na kiapo chake?

Wewe nawe. Unameza Matonge mazimamazima, yatakukwama bure. Jaribu kufikiri kidogo kabla hujajianika uelewa wako wa mambo. Wanasema read between the line.

Mag3, ndiyo maana nasema shilingi ina pande mbili. Solution si kumshambulia Pinda wa majambazi/vibaka. Kuna haja ya kumuanzia Kikwete kwa kulea haya (yeye kama mshika madaraka), WAZIRI Mama Sophia Simba ambaye tumeambiwa kuwa anauwezo mkubwa sana na ni msomi na mwisho TULIE NA Waziri wa Mambo ya Ndani bila ya kujali ni Masha au Mrema au ........ Mwisho kuna haja ya kujenga kambi za mafunzo kwa ajili ya kuwafunga Vibaka. Hizi ziwe kama ile kambi ya JKT ya Chita ambayo huweki hata ulinzi kama wa Jela. Mtu akifika huko, akijaribu kutoroka basi Simba wanamsubiri.... Vibaka hawa wawe wanakula miezi kadhaa na akiwa huko wafanye kazi za shamba ili kulisha mashule ya secondary, mahoteli, Vyuo nk.

Kama hilo hatuliwezi basi WAUWA Albino, wapelekwe hospital, wanyofolewe viungo vyao na hivyo viuzwe na hizo hela zisaidie Albino wengine. Viungo vya binadamu kama Moyo, maini, figo, macho, nk ni mali sana dunia hii. Kuna haja gani kuuwa na kipoteza hivyo vitu huku kuna watu kibao wanahitaji??
 
On a quick note, hili la waziri mkuu jamani si alishalijutia na kulitolea ufafanuzi, kes nini analetwa tena hapa on the picture wakuu? hili la kujichukulia sheria mikononi wala halijaanza leo na wala halitaisha leo wala kesho! ni jambo la kusikitisha sana walilofanya hao wananchi wa kigogo katika mfumo wa sheria.

lakini nadhani tumwache Pinda apumzike kwa hili.
 
Juzi juzi kuna dada mmoja alikabwa na vijana pale daraja la mto kizinga kuelekea Mbagala, wale vijana walimchana chana vibaya dada wa watu kwa wembe.. bahati nzuri kuna watu wakajitolea kumsaidia wakamkamata kijana mmoja.. Kilichotokea hapo mmmmh mpaka sasa sitaki tena nyama..... Yule kaka alipigwa vibaya sana, wakamchoma macho kwa bisibisi, wakamkata viganja vya mikono, walipoona amechoka yuko hoi wakammwagia petrol, wakamchoma... Kusema ukweli ilitisha sana, mbaya zaidi polisi walikuwepo hata hawakusaidia mpaka walipoona ameteketea kabisa ndo wakaenda kubeba mzoga uliobaki. Kuna mama akauliza kwanini walifanya vile badala ya kumpeleka post tu maana ni karibu, walimwambia yule mama akae kimya maana hajawahi kuibiwa eti wamechoka maana polisi wanakula njama na wale vijana, hata wakiwapeleka unashangaa kashatoka.... Cjui tunaelekea wapi, Mungu atuhurumie.

Bantu girl.. hapa umenipa wazo moja .. let me work on that.. utawala wa sheria hauna haraka vinginevyo jamii inaweza ikajikuta inaingia kwenye tatizo jingine kabisa.. kuwa leo mtu kakamatwa, kesho kafikishwa mahakamani, keshokutwa kanyongwa... halafu wiki moja baadaye ushahidi unaonesha kuwa siyo yeye mhusika wa uhalifu..!
 
Mzee Mwanakijiji,
Mkuu shukran kwa habari hii lakini mjomba vipi wewe na Pinda kuna kitu gani hasa?...
Hivi kweli wewe huoni uchungu kwa tukio hili isipokuwa kulitumia kama kielelezo cha yatakayofuata if wananchi watamsikiliza Pinda!..
Mkuu haya ni mambo yanayotokea kila siku, nadhani ingekuwa bora sana kama ungefuatilia kwa undani kisa hiki na ukayatoa majina ya wahusika, ukasisitiza sheria ichukuliwe dhidi ya huyo mzee uloficha jina lake na kikubwa zaidi wale wote waliohusika na kitendo hiki wafikishwe mahakamani (kwa lugha yenu)...Binafsi, wote waliohusika na kifo cha huyu mwizi wa mbuzi pamoja na wote wale wanaoiba simu na kuuawa, malipo halili na funzi la kusimamisha sheria ni murder one - hukumu yao ni kifo tu..
Kwa nini usifikirie hivi....kuwa huyo mtu ni sawa na Albino anavyouawa kisha hukatwa viungo vyake miguu na mikono wakaondoka navyo!..

A picture is worth a thousand words!
Ebu tazama watu walivyojipanga huko nyuma wakimtazama jamaa akivuta roho tena wamejikusanya kama vile kuna sherehe, leo maneno ya Pinda ambaye ni reflection yetu sisi unayapa uzito kiasi hiki mkuu ukasahau sherehe ya kina ndivyo tulivyo kwa mwizi wa mbuzi!..
Come on now, Pinda alichemsha sote tunafahamu hilo lakini kutumia picha za huyu mtu kwanza inanipa mshangao huyo Mpiga picha alikuwa akisubiri nini kutomsaidia jamaa, hata kama kumpeleka Hospitali.. Yaani kweli mtu unachukua picha ya binadamu mwenzako akipigwa hadi kufa kwake kisha mnakuja hapa na kutuonesha huruma in advance kwa wachawi ambao pia wanaua Albino bila huruma yoyote...

Samahani mkuu lakini hii haikukaa sawa kabisa!..This story alone worth a heading!
 
Mzee Mwanakijiji,
Mkuu shukran kwa habari hii lakini mjomba vipi wewe na Pinda kuna kitu gani hasa?...

Tatizo langu ni Pinda ni kuwa akiwa ni muwakilishi wa serikali ametoa agizo la kutaka watu wavunje sheria ati kwa sababu "viongozi wote wamechoshwa". Ingekuwa ni kuvunja sheria ndogo tungeweza kuchukulia alipitiwa lakini alipoitisha watu wauawe hapo hapo alivuka mpaka wa uchungu na kuingia uwanja wa kisasi.

Katika uwanja wa kisasi ni wachache sana hupona, kwani kila mwenye uchungu anakuwa na haki ya kisasi, na kila anayesababishiwa kisasi anapewa uchungu!

Hivyo tatizo langu na Pinda ni kuwa hadi leo hii hajatoa kauli au wito wa kutaka watuhumiwa wa mauaji ya Albino wafikishwe kwenye vyombo vya sheria na kabisa hajakataza watu kujichukulia sheria mkononi.

Hivi kweli wewe huoni uchungu kwa tukio hili isipokuwa kulitumia kama kielelezo cha yatakayofuata if wananchi watamsikiliza Pinda!..

Uchungu wangu mimi unazidi uchungu wa kihisia. Sioni furaha yeyote katika kuangalia picha hiyo bali kitisho ya nini kinawezekana. Hebu fikiria kama huyo mtu hapo angekuwa anadaiwa kuwa ni muuaji wa albino na wananchi wamemkamata na kumpa kibano? Kwa wengine hilo "anastahili" but what if people are wrong!?
Mkuu haya ni mambo yanayotokea kila siku,

Mzee wewe ni mwingine ambaye anarudia hili kwangu kana kwamba mimi sijui kuwa watu wanauliwa kila siku namna hii. Tangu utoto wangu nimekataa hili na believe me nimepata nafasi nyingine za kulipiza kisasi namna hiyo kwa kumuita mtu mwizi.

Siku moja ilikuwa siku kuu moja hivi ya kidini, pale Mwanza karibu na barabara inayokwenda Isamiliko kwenye kona ya "I turn, U turn" kama blocks tatu au nne kutoka shule ya msingi Nyanza kuna duka la Icecream na vikolombwezo vyako (si mbali sana na Ghandhi Hall). Nikiwa nimejipanga foleni kuwanunulia watoto icecream, popcorn n.k nikasikia mtu kasimama nyuma yangu na yeye akijifanya kuagiza vitu kumbe mkono mmoja alikuwa anani pick pocket..

Bahati nzuri ingawa natoka Bush, mimi si wa bush hivyo, nikakishika kile kidole na kukikunja bila kusema kitu, nikatoka foleni. Nimemkamata hivyoo hivyo bwana mdogo huyo.. nikamuuliza "Nikuitie "mwizi"?" Macho yake na uso wake ulivyobadilika hadi leo nakumbuka. Alipiga magoti na marafiki zake wakaja kuniomba nimsamehe. Nilimuachia. Lakini kama ningeamua kumuitia mwizi, ningemuua yule kijana!

Lakini siku moja kule Tanga maeneo ya New Nguvumali, kuna kijana alikamatwa akiiba "kuku" wa afisa mmoja wa Mkoa na akawa anapelekwa kituoni Chumbageni na raia. Alipofika mitaa fulani hivi vijana wakaanza kuzengea kuuliza kwanini mnapeleka polisi mwizi huyo? wakaanza kudonyoa kwa ngumi, mwisho wale wazee waliokuwa wameshikilia walizidiwa nguvu, na yule kijana aliomba hifadhi ya maisha yake kwa wazee wale lakini hawakuweza kumuokoa. Aliuawa kwa kupigwa mawe! Nilikuwa shule ya Msingi hapo na bado nakumbuka hadi eneo lenyewe (Palikuwa na Mwembe na Bomba la Maji!)

NImeyasema hayo kwa sababu sizungumzii kutoka hewani, na ninafahamu watu kujichukulia sheria mikononi hakukuanza leo. Sisemi kwa sababu sina uchungu bali kwa sababu uchungu ukielekezwa vibaya unafikisha kwenye kisasi.
nadhani ingekuwa bora sana kama ungefuatilia kwa undani kisa hiki na ukayatoa majina ya wahusika, ukasisitiza sheria ichukuliwe dhidi ya huyo mzee uloficha jina lake na kikubwa zaidi wale wote waliohusika na kitendo hiki wafikishwe mahakamani (kwa lugha yenu)...

Laiti ningekuwa na uwezo wa kufuatilia vitu hivi vyote. Ndiyo maana tuna Polisi na vyombo vya usalama.

Binafsi, wote waliohusika na kifo cha huyu mwizi wa mbuzi pamoja na wote wale wanaoiba simu na kuuawa, malipo halili na funzi la kusimamisha sheria ni murder one - hukumu yao ni kifo tu..

Hiyo hukumu haitolewi mitaani bali mahakamani tu baada ya ushahidi wote kutolewa na mtu kupewa nafasi ya kujitetea. Nje ya hapo ni kuishi katika utawala wa mwituni.

Kwa nini usifikirie hivi....kuwa huyo mtu ni sawa na Albino anavyouawa kisha hukatwa viungo vyake miguu na mikono wakaondoka navyo!..

Naweza kufikiria hivyo lakini hilo haliondoi uzito wa kile ambacho macho yameona. Mwizi wa Mbuzi anauawa namna hiyo! na watu wanasimama pembeni kuangalia kana kwamba aliyekufa ni nzi!
 
A picture is worth a thousand words!
Ebu tazama watu walivyojipanga huko nyuma wakimtazama jamaa akivuta roho tena wamejikusanya kama vile kuna sherehe, leo maneno ya Pinda ambaye ni reflection yetu sisi unayapa uzito kiasi hiki mkuu ukasahau sherehe ya kina ndivyo tulivyo kwa mwizi wa mbuzi!..

Maneno ya pinda siyapi uzito, ni mazito mno tayari!

Come on now, Pinda alichemsha sote tunafahamu hilo

Si "sote" tunafahamu hivyo. Na Pinda hakuchemsha, Pinda alichofanya ni kuvunja Katiba na kupoteza sifa ya kuwa Waziri Mkuu. Huwezi kuwa Waziri Mkuu halafu wakati huo huo ukatangaza watu wavunje sheria ati kwa sababu "umechoshwa". Hilo haliwezekani.

lakini kutumia picha za huyu mtu kwanza inanipa mshangao huyo Mpiga picha alikuwa akisubiri nini kutomsaidia jamaa, hata kama kumpeleka Hospitali.. Yaani kweli mtu unachukua picha ya binadamu mwenzako akipigwa hadi kufa kwake kisha mnakuja hapa na kutuonesha huruma in advance kwa wachawi ambao pia wanaua Albino bila huruma yoyote...

mzee haistahili kushangaa kwa sababu umeshasema inatokea kila siku!

Samahani mkuu lakini hii haikukaa sawa kabisa!..This story alone worth a heading!

nakubaliana na wewe kabisa.. lakini bila kuweka twist ya maneno ya Waziri Mkuu, hii ni kitu kile kile cha kawaida.
 
Back
Top Bottom