Mfano wa unyama utokeao kama utekelezaji wa lililokuwa agizo la Mh. Pinda (Graphic) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mfano wa unyama utokeao kama utekelezaji wa lililokuwa agizo la Mh. Pinda (Graphic)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Feb 5, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Feb 5, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Global Publishers

  Mauaji ya kutisha yaliyofanywa na wananchi wenye hasira dhidi ya kijana aliyejulikana kwa jina moja la Idd aliyetuhumiwa kutaka kuiba mbuzi kwenye banda eneo la Kigogo jijini Dar es Salaam, yamelaaniwa na baadhi ya wakazi wa eneo hilo.

  [​IMG]

  Licha ya kijana huyo kufumwa akiiba, wananchi hao walisikitishwa na namna kijana huyo alivyoteswa hadi kuuawa.
  Ilielezwa na mwanamke mmoja mkazi wa eneo hilo aliyejitambulisha kwa jina la Mama Omari kuwa, mtuhumiwa akiwa na wenzake wawili walinaswa na wananchi majira ya alfajiri wakifanya jaribio la kuiba mbuzi kwenye banda la mzee mmoja (jina halikutajwa).

  [​IMG]

  Alisema mama huyo aliyeshuhudia unyama aliofanyiwa Idd kwamba, wakiwa kwenye harakati za kumtwaa mbuzi huyo, mwenye mali aliwaona na kuwapigia kelele za mwizi ambapo wananchi walijitokeza na kumnasa kijana huyo, huku wengine wakifanikiwa kukimbia.

  "Walipomkamata walimvua nguo, wakaanza kumkata na viwembe, kumpiga kwa mawe huku wakimtaka atubu dhambi zake kabla ya kumtoa uhai.

  Baadaye walimchoma moto hadi ngozi ikatoka akawa anahangaika, watu hawakujali wakaendelea kumtesa hadi alipokata roho," alisema mama huyo kwa masikitiko.

  Mwananchi mmoja mkazi wa Kigogo ambaye hakupenda jina lake litajwe gazetini alisema kuwa, kitendo cha wananchi kujichukulia sheria mkononi kinatokana na watu kuchoshwa na vitendo vya kihalifu.

  "Kwa mfano eneo letu vibaka ni wengi sana, watu wanaibiwa kila siku na wahusika wanakamatwa lakini siku mbili wanaonekana tena mitaani, ndiyo maana watu wanajichukulia sheria mkononi," alisema Hamis Juma.

  Hata hivyo, msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Kamanda Abdallah Msika amekuwa akiwaomba wananchi kutochukua sheria mkononi na kuwataka wawe wavumilivu wakati jeshi lake likiendelea kuweka mikakati ya kukomesha vitendo vya uhalifu nchini.

  NB:
  Naamini Waziri Mkuu alimaanisha kitu kama hiki. Ingawa kwenye kesi za wizi wa "mbuzi" adhabu ya kifo namna hii ni kitu cha kulaaniwa, nina uhakika kama jamii tuko tayari kuona wauaji wa albino wakipewa kibano namna hii na kuuawa papo hapo.

  Kwa vile serikali imetoa kinga kwa wananchi kuchukua sheria mikononi, tusishangae kuona picha za namna hii zikidai kuwa "x ni muuaji wa albino". Waziri Mkuu ambaye alilia kuona mauaji ya albino sijui anaweza kujisikia vipi watu wakianza kutiwa moto, kupata kipigo namna hii kwa kisingizio cha "kutekeleza agizo la serikali".
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Feb 5, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Miafrika never cease to amaze me!

  Tokea mimi niko dogo watu kujichukulia sheria mkononi na kutoa kisago kwa watuhumiwa wa wizi imekuwa kama ni kitu cha kawaida. Hili ni tatizo la muda mrefu sana na sitakosea nikisema hatuwezi kufuata, kusimamia, na kutekeleza sheria. Utekelezaji wa sheria kwetu sisi ni dhana ngeni. Kwa sasa, mpaka nitakapothibitishiwa visivyo, nasema hilo ni jambo jingine ambalo hatuliwezi na hatuliwezi kwa sababu Miafrika Ndivyo Tulivyo.

  Mtu jiulize, ni watu wangapi mpaka hivi sasa ambao wameshapoteza maisha kwa kutuhumiwa kimakosa kuwa ni wezi? Maana all it takes ni mtu mmoja tu mtaani kusema...mwiiiiiizi....and that's it. Hii ni jamii ya aina gani jamani?
   
 3. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #3
  Feb 5, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kazi kweli kweli......! Pinda akiona hii picha atalia au atacheka assuming huyu jamaa alifanyakosa la kumuua albino?
   
 4. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #4
  Feb 5, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Agizo alilotoa Waziri Mkuu wether ni kuua wauaji wa maalbino or not was very incorrect.
  Watanzania wanachokifanya sasa is disrespecting the judicial system.with time they will have their own parliaments in the streets making and enacting laws and before we all notice its gonna be anarchy.
  Waziri Mkuu asitake wananchi wajaribu utamu wa kukaa in the bush or in a state of anarchy coz bringing them back to civility going to be rather an issue!
   
  Last edited: Feb 5, 2009
 5. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #5
  Feb 5, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Ilitakiwa iwe fundisho kibaka akiuliwa mtaani kwenu mtaa mzima mahakamani
   
 6. Zero

  Zero JF-Expert Member

  #6
  Feb 5, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 301
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hapa mkuu Shy unakuwa extremist. Mtaa mzima? Thats too much!

  Anywayz. Nadhani ni rahisi kulaani kwasababu we have every right to do so. Kuua kibaka kwa kosa la wizi sio sahihi. Kujichukulia sheria mkononi kwa kifupi sio sahihi. Lakini kwa wale ambao mmeshakumbwa na wizi wa vibaka au majambazi, mtakubaliana na mimi (japo kwa shingo upande) kwamba some vibaka na wezi deserve to die. Yes, its against humanity and human rights, lakini kama alivyosema Pinda, inatia uchungu sana. Just imagine wezi wanakuja nyumbani kwako, wanakukamata wewe baba mtu wanakuingilia kinyume na maumbile mbele ya mkeo na watoto, wanamuingilia mkeo mbele na nyuma etc mbele yako na watoto. Hii inauma kiasi gani?

  Katika hali hii, leo na kesho, nikisikia mwizi anakimbizwa nyumba ya jirani, natoka na kiberiti na petrol kabisa. Because I strongly believe hawa watu wanastahili kifo tu. Sheria inapindishwa pindishwa mno. Hawa watu hawaadhibiwi vya kutosha. Wengi wanaachiwa tu muda mfupi baada ya kukamatwa. Wananchi wamechoka. Nadhani wale ambao wamewahi kuibiwa na kufanyiwa ubaya will share the same sentiment.
   
 7. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #7
  Feb 5, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mwanakijiji,
  Na heshima zote kwako. Huoni kuwa TATIZO LIMELALA sehemu nyingine?? Mie nafikiri hili tatizo la watu KUTOKUHESHIMU sheria linaanzia hizi nyumba mbili yaani IKULU na BUNGE. Huko wanapeleka ugonjwa huo hadi serikalini na unafika hadi mitaani.

  Maadamu nchi yetu RAIS ana madaraka makubwa sana, bila wasiwasi naweza kusema tatizo linaanzia huko. Ila hapa siwezi kusema Kikwete. Limeanza hata kabla yake kuwa Rais. Nafikiri uzembe ulianzia kwa Nyerere, Mwinyi akaupa speed kubwa sana. Viongozi wetu hawana adabu. Hivi mtu kama Ditopile anayeacha kituo chake cha kazi Tabora na kuja Dar kuuwa dereva wa Daladala, na rais wala haimpi shida. Uhuni wa Mkapa hadi anakuja kuwa anawapa na akina Warioba wale. Wezi kama Chenge na wenzake na Rais wala hasemi kitu. Haya maovu yote yana/yamefanyika na wala watu hawachukuliwi hatua inapelekea watu kuacha kufuata sheria. Sasa mitaani watu wamechoka. Pinda aseme au asiseme, KIPIGO KITAENDELEA. Hawa watu siku moja yafanyike Mapinduzi Tanzania, aje Rais na chama kingine. Siku hiyo utaona hasira za watu mara wakimpata Lowassa, Rostam, Mkapa, Chenge, Rashid ect. Ila Manji nafikiri na Wahindi wenzake watakuwa tayari India maana wakisikia tu uchaguzi, haoooooo!!!!
   
 8. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #8
  Feb 5, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nitakubaliana na wewe na hili tatizo limeanzia kwenye katiba yetu ambayo ni matatizo ya siku nyingi Rais amekuwa akiingilia sana madaraka ya mahakama.
  Ila wewe kusema Ditopile alitoka tabore kuja kuua siyo sahihi hata kidogo.maana Ditopile was provoked and he killed na akampigia simu Tibaigana ameua na Tinaigana ndio akaanza kumtetea ameua kwa bahati mbaya.
  Wananchi wote wanapaswa kuelimishwa hasa kwenye sekta ya sheria!
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Feb 5, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280


  Zero.. kuna jambo moja ambalo labda unalimiss. Albino akishambuliwa na mtu anayeyetaka kumuua na akamgeuzia kibano akamuua mtu huyo hiyo inaitwa "self-defense". Tunaposema kuwa haki ya kuishi ilindwe maana yake ni kuwa haki hiyo inapotishiwa basi mtu anayo haki ya kujitetea hata kwa kuua.

  Hivyo, mwizi au jambazi akikuingilia nyumbani kwako na akafanya kitu ambacho unaamini ni tishio kwa uhai wako na wewe ukimpiga nyundo na kumuua, hiyo ni kujihami. Hakuna atakayekushtaki na mimi nitakutetea.

  Hatupingi watuhumiwa wa mauaji kuuawa, tunachopinga ni kuwaua pale endapo uwezo mwingine wa sheria unaweza kuchukua mkondo. Hiyo picha hapo juu inaniambia kitu kimoja tu.. watu hawajali sheria. Kundi la watu wote wanaoangalia huyo jamaa unattaka kuniambia wameshindwa kumkamata, ushahidi wa mbuzi, n.k na kumpeleka polisi?

  Huyo hakustahili kuuawa namna hiyo.


  Kuamini peke yake haitoshi kwani na mtu kama wewe anaposhika kiberiti na mafuta ya taa na mimi naamini kuwa anastahili kifo vile vile kwani muuaji ni muuaji tu. Ukija mtaani kwangu na kiberiti chako utakutana na mtutu wa bunduki!

  Huyo mwizi hajakuibia wewe, na wakati mwingine hata ujui alichoiba nini wewe unakurupuka na kiberiti chako. Siku moja niko makutano ya Uhuru na Msimbazi pale, kuna duka linauza vitu vya electronics za zamani. Jamaa sijui kafanywa nini kaiti "mwizi huyo" .. ilichukua ndani ya dakika moja watu kuanza kumshindilia jamaa mangumi. Dala dala ambayo hata haijui nini kimetokea konda wake akataremka mbio kaenda kumchapa jamaa ngumu, halafu huyo akawahi kudandia gari yake!

  Bahati nzuri mapolisi tuliokuwa nao karibu wakaingilia kati pale. Tukaja kugundua kuwa jamaa walikuwa wanataniana tu!


  No they won't! Unafikiri katika mbingu hii ni wewe tu na wengine wanaojua ubaya wa kuibiwa? Kama kuna tatizo la sheria maana yake ni kuwa kuna tatizo la serikali. Na kama ni serikali ni viongozi walioko madarakani. Unabadilisha uongozi madarakani kwa kura na kuchagua watu unaofikiri watasimamia sheria.

  Kusema utekelezaji wa sheria ni mbaya halafu kila uchaguzi mnarudi kuwachagua watu wale wale mnatarajia nini? Chenge kaoneshwa kavunja sheria guess what.. kapewa Uwaziri mara mbili!

  Fikiria Dr. Idris kavunja sheria akazawadiwa ukurugenzi na hata alipotaja kujiuzulul akabembelezwa abakie! Sasa tatizo siyo kwamba sheria ni mbaya au hazisimamiwi, tatizo ni kuwa watu wamezoea ubovu mno, kwani hao hao wenye kukurupuka na viberiti na mafuta ndiyo hao hao kesho wanaimba CCM nambari wani!
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Feb 5, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Nyerere kwa kosa gani? Nyerere alipotumia sheria kushughulikia nidhamu hadi watu wakawa wanaogopa wakamuita "haambiliki" na wengine wakasema "hakuna aliyemkatalia". Hivi unajua viongozi wangapi wakati wa Mwalimu walikuwa wakitumuliwa kazi hasa miaka ya mwishoni ya utawala wake. Unajua kwanini?

  Nyerere aliporithi nchi kutoka kwa wakoloni hakurithi watendaji, na wataalamu wengi Watanzania. Sasa afanye nini kama nusu yao ni wabovu? Angalia barua yake kuhusu "Pomposity" au kuhusu tatizo la Rushwa. Hakuwa na wataalamu wa mahesabu kama tulionao sasa (in quantity and quality), hakuwa na madaktari, wahandisi, n.k kama tulionao leo bwelele. Sasa nusu yao wakiwa na ufisadi anafanya nini kutimua wote au kuchukua hatua zenye hekima?

  Leo hii hakuna udhuru wa kumvumilia daktari, mhandisi, mwanasheria, hakimu, ambaye ni fisadi.. wote leo ni replaceable! Hadi Rais mwenyewe.

  Na hata tukikubali kuwa tatizo lilianza wakati wa Nyerere na tukikubaliana kuwa Nyerere ndiyo baba wa Taifa la Mafisadi, na tukampa na cheo kuwa ni Fisadi wa Mafisadi wote, so what? Tatizo lipo sasa na yeye yuko kaburini. Tatizo hili halitattuliwa na marehemu au mahayati wapendwa! Tatizo hili ni letu, ni la kizazi chetu, ni tatizo la walio hai siyo la wafu!
   
 11. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #11
  Feb 5, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Nilijua tu Nyerere ataibukia mahala fulani....
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Feb 5, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Of course, ni kama mzimu fulani hivi.. mtu anaumwa kichwa, Nyerere, mtu kaiba EPA Nyerere, mtu kaweka vijicenti ulaya huko Nyerere, mtu kafumaniwa Nyerere.. huyo Nyerere alikuwa ni mungu wa aina gani huyo ambaye bado anashikilia akili za watu hivyo?

  Kwanini basi tusiombe familia yake itupe mwana ambaye ni mfalme ili angalau tupate "Nyerere" mwingine wa kumbebesha mizigo ya taifa letu? PInda atoe maagizo yaajabu ajabu watu wanakimbilia Nyerere..

  Napenda take yako kuwa "Waafrika ndivyo tulivyo".. mimi nadhani kwa jinsi watanzania wanakwepa kuwajibika wao wenyewe au kuwawajibisha wale walioko madarakani sasa ndivyo hivyo hivyo wanathibitisha kuwa "watanzania ndivyo tulivyo".

  Ni rahisi zaidi kumlaumu Nyerere kwa matatizo ya TAnzania na kama Wamarekani wanavyomlaumu marehemu George Washington kwa vita vya Iraq na hali mbaya ya Uchumi wa Marekani leo hii. Ni sawa kabisa na jinsi Waingereza wanamlamu Queen Victoria kwa matatizo ya Uingereza leo hii!
   
 13. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #13
  Feb 5, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Kevo,
  Kwa kugongwa kwa gari la SERIKALI, tena lina bima, sidhani kama ilikuwa sawa kupiga mtu risasi. Anyway hilo lilishaongelewa na si muhimu hapa. Hapa la muhimu ni kuwa ALIKUWA NJE YA KITUO CHAKE CHA KAZI bila kumtaarufu boss wake. Ila mambo ya kishkaji unajua tena. Mifano kama hiyo iko mingi. Hata hii ya watu kwenda kuweka sahihi UK tena sijui CAFE? Na rais anaona mswano tu.

  MwanaKIJIJI,
  Ngoja nikukumbushe SALA YA BWANA WAKATI WA NYERERE.

  "Baba yetu uliye Msasani ....... UTUSAMEHE MAKOSA YETU KAMA ULIVYOMSAMEHE BARONGO......"
  Nyerere nina heshima naye kubwa sana. Ila haya mambo ya KULEA wazembe kazini alikuwa nayo sana. Hebu ona mfano wa MWINYI aliyechoma Vizee huko Shinyanga (wakati huo Pinda alikuwa kashasema??) na JKN akamtoa na mwishoni akampa asante kwa kumfanya RAIS WETU. Haya juzi tumesoma ya Mgonja ambaye alikuwa akitembeza VAZI LA ADAM mbele ya vitoto vya watu kwenye mashule ya Sekondari ya Kike. Na yeye akaja zawadiwa nini? Ukuu wa mkoa??
  Wakati anafanya haya, hasa la Mwiyi, Tanzania ilikuwa na wasomi wengi sana. Angeliweza kutafuta mtu wa maana na kumwachia. Hii ilikuwa miaka mingapi tangu Wakoloni waondoke? Naelewa na yeye alikuwa binadamu kama sisi na kusema ukweli MILELE ntampa heshima kubwa sana huyu Mzee. Ila jambo moja ambalo milele ntapingana nalo ni hili la KULEA Wazembe na kuwapa UHAMISHO mara wanapoboronga sehemu. Amen.
   
 14. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #14
  Feb 5, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Nyani na Mwanakijiji,
  Naona mnatoka NJE ya yale niliyoyasema. Mie nimetoa lawama kwa KIPANDE cha kazi alizozifanya JKN na wala si kwa yote aliyoyafanya. Ni sawa na Mkapa. Nalaani mengi aliyoyafanya ila kuna mengine kafanya mazuri tu.
  Mie kwangu siyo kila kitu ni BLACK and WHITE. Na mtu hatanifanya niamini vinginevyo. Hata aje mtu kama MALAIKA na awe kiongozi, najua sehemu fulani na yeye anaboronga. Ila ntapima siku zote mabaya na mazuri na huko kulikolalia mzani ndiko ntamuweka jamaa. JKN mzani wake umelala kwenye MAZURI. Ila si kweli kuwa upande wa mabaya hamna kitu. Vipo vi-gram vingi tu............... Sasa nikivisema kidogo basi YANAKUWA MAKUBWA? Kama kuna mtoto wa JKN anaweza kuongoza nchi kama baba yake na kurudisha heshima kwa nchi yetu, basi na iwe hivyo.
  Hata kama atakuwa na yeye HAPENDI MPIRA (aibu ya TAIFA STAR mbele ya Rais huku hawana mashati) na michezo kwa ujumla, poa tu kwani sasa hivi tunashinda kombe gani la nje? Hata kukimbia hatumo na heri enzi zake walikuwepo wengi tu akina Shahanga, Mwinga Mwanjera? Ikangaa, Filbert Bayi, etc. Hivyo, NAUNGA kabisa mkono mtoto wa JKN aje na awe Rais ili muradi ajisikie kweli nchi ni yake. Labda kwa akili za Kiafrica tulivyozoea kuwa na Mfalme na sasa tuna Rais, kuna sehemu tunakosa LINK. Lowassa anaona Tanzania ni kisima cha kuiba. JKN aliona nchi yake.
  Niliangalia mazishi ya mfalme Hassan wa Jordan. Iliposhindikana kutibiwa, akarudi Jordan kusubiri kufa. Akazunguka na ndege kuangalia nchi yake na anasema machozi yakwa yanamtoka. Yes, kuangalia nchi yake, watu wake nk na si "Kisima cha kuchota utajiri".
   
 15. M

  Moelex23 JF-Expert Member

  #15
  Feb 5, 2009
  Joined: Oct 8, 2006
  Messages: 497
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  ENOUGH IS ENOUGH.

  This is a TRAGEDY and Mh. Masha being a lawyer should condemn this ASAP, The PM and The President also. U can not justify SENSELESS killing no matter what the guy (RIP) did. May his blood be on all of us Tanzanians who are hypocrites and would have rallied if the dead was from a well to do family.

  Shame on all of us and May The Almight Rest His Soul In Eternal Peace.
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #16
  Feb 5, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  well he later died.. peacefully!

  [​IMG]
   
 17. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #17
  Feb 5, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  This is not dying peacefully....how can you die peacefully after being on a receiving end of such a beating?
   
 18. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #18
  Feb 5, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Nadhani hatumtendei haki Waziri Mkuu. Kwani hao mbuzi walikuwa albino? Tabia hii ya kuchoma wanaodhaniwa kuwa vibaka haikuanza na tamko la Pinda. Ni aibu yetu sote kama jamii.
   
 19. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #19
  Feb 5, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  point ni kwamba kwa tamko la pinda, ni kuipa tabia hiyo legitimacy. Ni kukubali kuwa hatuna utawala wa sheria, ni kusema kuwa watu "wakichoshwa" basi wachukuwe hatua papo kwa papo dhidi ya wale wanaosababisha hisia hiyo ya kuchoshwa. Hoja ni kwamba, awe mwiba mbuzi, mgoni, au muuaji (haijalishi anayemuua nani) sheria ni lazima iwe dikteta. Tukiweka exception (kama ilivyofanya serikali) kuwa anayeuwa albino basi naye auawe papo hapo hapo basi tunakuwa tumehalalisha uvunjaji wa principle.

  Na kama Nyerere alivyosema ukiivunja kanuni kubwa, basi kanuni hiyo itatafuta njia ya kukuvunja..! I know.. he was right.
   
 20. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #20
  Feb 5, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Ndio maana hapo mwanzo nikasema kuwa mimi tokea niko kido..shule ya vidudu haya mambo yalikuwepo na kama nina kumbukumbu nzuri, sikuwahi kumsikia kiongozi yeyote wa ngazi ya juu serikalini akikemea uchukuliwaji wa sheria mkononi na wananchi dhidi ya watuhumiwa wa wizi. Mimi mwenyewe nimeshuhudia watuhumiwa watano waliowahi kupigwa mtaani kwetu hadi wakafa halafu wakachomwa moto (ila mimi sikushiriki). Yaani sisi tunaishi kama manyama porini. Tuko jamii ya ajabu sana.

  Nani hapa ataniambia hajawahi kushuhudia mtuhumiwa wa wizi akipata kibano? Usikute humu humu tunao walioshiriki katika kutoa vibano hivyo maana kuna kipindi ilikuwa kama fashion vile akipatikana mwizi na wewe angalau uwe umempatia angalau ngumi kama sio kumrushia kitofa. I tell you, we are something else!
   
Loading...