Mfanano wa UKUTA na Gwajima

Mfanano wa UKUTA na Gwajima

Kama ilivyokuwa kwa UKUTA, Askofu Gwajima naye kafanya hivyo hivyo.

Kawapandisha hawaa wafuasi wake, misukule wake, na wadandia treni lake halafu siku ya siku ilipofika kawaacha wananing'inia bila ya kuwapatia kile walichodhani watakipata toka kwake.

Kiki keshaipata [ambayo huenda imeambatana na rupia kiasi fulani].

Nadhani sasa mashiko ya hiyo nuksani yake na mkuu wa mkoa wa Dar yanaanza kufifia.

Kwa vile tumekuwa ni watu wenye kupenda penda matukio ya muda mfupi, nasubiri kwa hamu tukio lijalo litakalobamba.

Sijui ni tukio lipi lijalo ambalo litabamba katika siku na majuma yajayo lakini nadhani ule uchaguzi wa kumpata rais wa wale wadada na makaka 'wasomi' kule Arusha huenda ukawa ni mmojawapo.

Tusubiri tuone.
Nimeshuka mpk mwisho nikajua nitaona vyeti vya Daudi bashite kama hakuna haiwezi kuisha kirahisi acha kujidanganya
 
Kaka umetumwa? Hili suala lipo sensitive kinoma. Mkuu wa mkoa unashindwa kukanusha tuhuma, na mamlaka zipo kimya, halafu sisi wananchi tukae kimya. Shame on you!!
 
Wengine ni wasindikizaji tuwaChe simba na yangatuone nani bingwa maana wote wananafasi
 
Bashite haifutiki japo mnajitutumua kuifukia kwa nyuzi kama hizi. Ni mpaka hapo tuone vyeti vya Bashite
 
Yaelekea alivyokamatwa na kupekuliwa juzi, Gwajima kanywea.

Kwa upande wa makonda: yeye kaharibu credibility za watu; na yeye kachafuliwa. Safi kabisa.
 
Wafuasi wake, misukule wake na wadandia treni lake watakuambia ameamua kutunza kombora akisubiri mashambulizi kutoka kwa maadui!

Hii nchi ina matatizo zaidi ya tunavyodhani!
 
Kama ilivyokuwa kwa UKUTA, Askofu Gwajima naye kafanya hivyo hivyo.

Kawapandisha hawaa wafuasi wake, misukule wake, na wadandia treni lake halafu siku ya siku ilipofika kawaacha wananing'inia bila ya kuwapatia kile walichodhani watakipata toka kwake.

Kiki keshaipata [ambayo huenda imeambatana na rupia kiasi fulani].

Nadhani sasa mashiko ya hiyo nuksani yake na mkuu wa mkoa wa Dar yanaanza kufifia.

Kwa vile tumekuwa ni watu wenye kupenda penda matukio ya muda mfupi, nasubiri kwa hamu tukio lijalo litakalobamba.

Sijui ni tukio lipi lijalo ambalo litabamba katika siku na majuma yajayo lakini nadhani ule uchaguzi wa kumpata rais wa wale wadada na makaka 'wasomi' kule Arusha huenda ukawa ni mmojawapo.

Tusubiri tuone.

Hujielewi wewe Mouuzi
 
Back
Top Bottom