Hapo zamani za kale palikuwa na Mfalme ambaye hakujali kitu chochote katika mamlaka yake isipokuwa mavazi yake, aonekane amependeza.
Mfalme huyu hakufanya kazi wala hakupatiliza majukumu yake, alikuwa akiagiza tu. Yeye kila mwisho wa wiki alipanda farasi wake akatoka mjini na walinzi wake, akiwa na mavazi mapya tofauti na ya wiki iliyopita.
Ikaendelea hivyo kwa muda.
Hilo wakalitambua wajanja wa mjini.
Siku moja wajanja wawili wakamwendea Mfalme. Wakajitambulisha kuwa wao ni mafundi stadi wa kutengeneza mitindo ya nguo ambazo hazijapata kuonekana. 'Sisi tuna uwezo wa kukutengenezea nguo ya ajabu mno. Ni watu wenye akili tu na wajanja ndiyo watakaoiona.
Ama kweli wajinga, wasiokupenda na wanafiki...hawataona kitu' wakamwambia.
Mfalme yule akafurahi sana, na mara moja akawapa matapeli wale tenda ya kumshonea nguo hiyo ya ajabu.
'Nitawagundua wote wanafiki wasionipenda' Mfalme yule akajiambia moyoni mwake!
Matapeli wakaingia kazini. Mwezi ukapita na nguo ikawa haijaletwa.
Mfalme akaamua kutuma Usalama wake wa Taifa, kutazama kulikoni? Walipofika, wakawakuta kweli matapeli wale wamesimama wanatoka jasho....lakini hawakuona nguo yoyote! Kwa vile Mfalme alijigamba mbele yao kwamba ni wale tu wanaompenda na kuwa na utii wa dhati ndiyo watakaoliona vazi lile....wale walirudi huku wakimsifia sana Mfalme na kwamba vazi litakwisha karibuni.
Mfalme akaandaa sherehe kubwa siku ya kuzindua vazi lile, akaita ma Fleva yote ya mjini. Watu wakakusanyika kupita kiasi kuja kushuhudia vazi hilo la ajabu. Kila mtu akijinaki kuwa 'ataliona tu' maana yeye ni 'chawa' madhubuti wa Mfalme!
Acha bwana midundiko ianze siku hiyo ya siku.
Mfalme akaanza msafara wake wa farasi mia moja kupitia barabara za mji akiwa amevaa kile matapeli walichomwambia ni vazi la kipekee!
Wananchi, kwa kuhofia kuonekana wapumbavu, wasio na utii na wanafiki.....wakawa wanashangilia kwa nguvu, wakisifia 'mtindo' wa vazi lile. Mfalme akiwapungia mkono wanachi wake, furaha moyoni wimbo mdomoni: 'asanteni, asanteni wananchi wangu waaminifu wenye mapenzi ya dhati. Kutoka hapa tutaiendeleza nchi hii kwa umoja wetu'!
Huku tamasha ikikaribia kumalizika, mama mmoja akiwa na mwanawe wa miaka mitatu, akapata nafasi ya kupenya hadi nafasi ya mbele na kuwa ana kwa ana na Mfalme. Kile kitoto kilipomwona Mfalme tu kikacheka sana na kupiga kelele, huku akivuta khanga ya mamaye: ' Mamaaa eeh, mtazame yule...! Mbona yuko uchii vilee?'
Mfalme akastuka, na watu wakaanza minong'ono, wengine wakinong'ona; ' Eboo! hata mimi nilikuwa naona mauzauza...maneno ya mtoto ni kweli!' Ila Mfalme akaendelea hivyo hivyo ingawaje alijuwa alitapeliwa, na raia pia wakaendelea hivyo hivyo kukubali utapeli, wakihofu vinginevyo wataonekana wanafiki, wasio na mapenzi na Mfalme na nchi!
HADITHI YANGU IMEISHIA HAPOOO.
ONYO: Hii ni hadithi, tena imetokea zamani kabla ya mimi kuzaliwa, ukiifasiri vingine shauri yako, utapambana na hali yako!