Alikufa akaja kufufukia Tanzania
"Leo ninayo maneno muhimu. Songeni karibu muyasikie. Ninayo amri ya Mfalme wetu. Nataka kukusomeeni. Amri yenyewe imeandikwa kwa shairi. Mnajua Mfalme wetu anavyopenda mashairi (Watu wanacheka)" Na shairi lenyewe ni kama ifuatavyo:
Nimechoka mashtaka, kila kitu kuwa ghali
Basi natoa amri kwa, hao wote wenye mali
Kutoka siku ya leo, hata kesho ya Ukweli
Kila kitu pesa moja, kwa kila ratili moja
Wauzaji wa Kichaa, na wote wangu raia
Wanawake kwa waume,wakubwa wadogo pia
Ifuateni amri, asofata atalia
Kila ratili moja, iuzwe kwa pesa moja.