Mfalme Akihito wa Japan aomba kung’atuka

Mfalme Akihito wa Japan aomba kung’atuka

kabwinyola

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2016
Posts
564
Reaction score
708
_90708159_eeb9aef5-344e-49d7-9dd9-a3d3b3f8025f.jpg

Wananchi waonekana kushangaa baada ya Mfalme Akihito kutangaza matamanio yake ya kung'atuka

Mfalme wa Japan Akihito ameeleza mapenzi yake ya kutaka kung'atuka.
Akihutubia taifa hilo kupitia runinga, amesema ana wasiwasi kwamba umri na udhoofu wa afya yake huenda vikamfanya ashindwe kutekeleza majukumu yake.

Kwa sasa, hakuna nafasi kisheria kumruhusu mfalme kuondoka madarakani Japan.Lakini muda mfupi baada ya hotuba yake, Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe, amesema atathmini kwa makini matamanio ya mfalme huyo.
_90708160_4d9a31e3-2da1-4b7a-a5b3-dc56698c1516.jpg

Mfalme Akihito

Mfalme Akihito amekuwa madarakani tangu kifo cha babake, Hirohito, mwaka 1989.Habari kwamba anataka kung'atuka zilianza kutokea kwenye vyombo vya habari mwezi jana.Mfalme Akihito wa Japan aomba kung’atuka
 
Hahahaha wakati yeye uongozi wake ni wakurithi akitaka anabaki mpaka afe huku kwetu mugabe hataki kuondoka
 
Back
Top Bottom