detective mfaume
Member
- Dec 23, 2016
- 31
- 69
Mtu wa falsafa, mwanamikakati, mpanga mipango na muandishi aliekua na uwezo, na mawazo ambayo yanatumika kwa kiasi kikubwa na mashirika ya kijasusi, kutoa elimu yakijasusi, usalama wa mataifa, taaluma ya usimamizi wa sheria, mashindano ya kibiashara, siasa na utaalamu wakivita.
The Art of Strategy
Na
Mfaume Hassani Hamadi
Mwanafunzi Shahada ya Usimamizi Wa Sheria UDSM.
Young intelligence and security analyst
Professional law enforcer.
Sun Tzu alikua ni General wakichina alieishi katika zama zilizoitwa Spring Autumn, Miaka ya 722-481 BC.
Kabla yakupandishwa cheo na mfalme Helu alipewa jaribu la kupima uwezo wake katika kuongoza na kufunza washindani wapiganaji.
Sun Tzu alitakiwa kuwabadilisha makahaba 360 wa mfalme ili waweze kua wanajeshi na wapiganaji mahiri watakaoweza kuingia vitani dhidi ya maadui.
Sun Tzu aliwagawanya makahaba wa mfalme katika makundi mawili.
Ili kutengeneza utii sun tzu aliwapa vyeo vyajuu (ukamanda) makahaba wawili waliokua wakipendwa zaidi na mfalme.
Akawapa amri kugeuka kulia. Kwa mara yakwanza wakacheka (labda kwasababu ya aibu na kutokuzoea)
Sun Tzu akasema General anawajibu wakuhakikisha wafuasi wake wanaelewa amri waliyopewa vizuri. Kisha akarudia kutoa amri kwa mara yapili, wakacheka tena.
Mara hii akatoa amri kua makahaba wawili hawa waliopendwa na mfalme wachinjwe mbele yake kwakukaidi amri.
Akateua maofisa wengine ambao kwa mara hii hawakusita kufata amri mara moja bila kujiuliza.
Baadae alitoa maana ya kitendo chake kua kama wafuasi wameelewa amri kisha wakakataa kuifata huo ni uzembe wao. Pale general anapochaguliwa na mfalme, ni wajibu kutekeleza majukumu yake hata kama mfalme atapinga.
Hapa nakumbuka msemo niliofundishwa na mwalimu wangu, Dr Jingu kua.
Politicians give order to go to war, but the drama of war is vested to the General
Kutokana na ujasiri huu mfalme alitokea kumuamini sana sun tzu na kumpa cheo cha juu kuliongoza jeshi.
Sun Tzu aliandika kitabu kiitwacho The Art of War chenye sura 13 kinachozungumzia masuala mbali mbali ya kimikakati yakivita dhidi ya adui. Anaamini kua vita ni swala la kuishi au kufa lisilohitaji drama za aina yeyeote.
Mikakati Dhidi ya Adui.
Vita ya akili ina nguvu kubwa kuliko vita ya nguvu.
Adui hapaswi kujua uwezo wako. Ukiwa na nguvu muonyeshe wewe ni dhaifu na ukiwa dhaifu muonyeshe kua una nguvu yakunpiga.
Ni lazima kujua mipango na siri za ndani za adui yako, ikiwemo hata kutumia kachero na ma shushushu.
Katika ushindani au vita anaeshinda ni yule ambae anajijua na anamjua adui yake kiundani na mapema zaidi.
Kama unajijua na humjui adui yako usitegemee kushinda, na kama hujijui na pia humjui adui yako utashindwa wakati wote.
Mshindi ni yule anaejua muda sahihi wakushambulia au kuto kumshambulia adui.
Adui anaweza kua na uwezo mkubwa zaidi yako lakini asikushinde, kwakumzuia kukushambulia au kukusambaratisha.
Unaweza mzuia kwakujua mipango na hatua zake mapema kisha kumvuruga.
Ukiwa mbali muonyeshe adui kua uko karibu, na ukiwa karibu nae muonyeshe kua uko mbali ili kumstukiza na kumzuia kutojiandaa.
Kumdanganya na kumfubaza adui yako asijue una mipango gani.
Ili kushinda unatakiwa kujua udhaifu na nguvu adui aliyonayo.
Mlazimishe adui ajitokeze na aanze kutekeleza mipango yake ili upate urahisi wakumvuruga na kutumia udhaifu wake kumshambulia.
Mpambanaji mzuri sio yule anaeshambulia, bali yule anaeweza kumshinda adui bila mapambano.
Kutumia Kachero, Shushushu na ujasusi.
Taaluma ya ushushushu kwa sasa inaaminika nakutumika na mataifa yote duniani, katika kukusanya taarifa zakiusalama na mambo mengine kwa maslahi ya nchi.
Sun Tzu aliamini kua katika kupata taarifa za adui yako unapaswa kutumia spy wa aina tano. Ambao ni
(i) Local spies
(ii) Moles/inward spies
(iii) Double agents/converted spies
(iv) doomed spies
(v) surviving spies.
Aina hizi za mashushushu nitakua nikizielezea katika Makala zangu zitakazokua zikielezea na kuchambua maswala ya usalama, usimamizi wa sheria na ujasusi.
Kutoa kafara
Kuna wakati inakupasa kutoa kafara vitu au watu wachache miongoni mwa jeshi lako ili kuzidi mbinu za adui na kumshinda.
Labda nitoe mfano kuelezea nukta hii ambayo najua itakua na utata kwako msomaji hasa pale linapokuja swala lakutoa kafara watu wako (wanajeshi au hata wananchi).
CIA Operation Northwoods
Katika miaka ya 1960s shirika la kijasusi la marekani CIA lilipanga kuendesha operation maalumu iliyoitwa “operation northwoods” katika kipindi cha vita baridi “Cold War”.
Lengo la operation hii ilikua ni kufanya matukio ya kigaidi nchini marekani dhidi ya mali na wananchi wake yenyewe, kisha kuisingizia Cuba juu ya matukio hayo, ili kupata nguvu ya wananchi “public support” katika kuivamia Cuba.
Cuba ilikua ni hasimu na tishio kubwa kwa marekani.
Japo majarida mbalimbali yakijasusi yanaeleza kua operation hii haikufanikiwa kutokana na raisi John Kennedy kutoikubali, ambaye badae aliuwawa. Jopo la viongozi wa juu wa ulinzi na usalama marekani walisaini na kupitisha mpango huu.
Hapa tunaona kua marekani ilikua tayari kuua wananchi wake ili kutimiza kinachoitwa maslahi ya taifa.
Angalia pia OPERATION CHAOS, iliyoisha kwa wanachuo wanafunzi wengi kuuwawa.
Kuungana
Sun tzu anaamini kutengeneza muungano pale inapohitajika. Mfano kuunganisha mataifa kwa lengo lakiulizi na usalama wa washirika dhidi ya maadui.
Moja ya sababu kubwa inayotajwa na waandishi mbalimbali, ya Tanganyika kuungana na Zanzibar, 1964 ilikua ni swala la kiusalama Wa mataifa haya mawili yaliyokuja kua taifa moja. Katika historia nchi nyingi zimefanya hivyo pia.
Haya ni machache katika mchango wa mwanafalsafa huyu kwa ulimwengu wasasa. Hata hivyo baadhi ya waandishi zaidi kutoka mataifa ya magharibi hawaamini uwepo wamtu aliekua anaitwa sun tzu huko uchinani. Wanaamini labda kitabu cha the Art of War kiliandikwa na watu wenye utaalamu wakiusalama na uzoefu wakivita.
Lakini yote ya yote alieandika kitabu anaonyesha alikua ni mtu mwenye uwezo mkubwa na mawazo chanya katika masuala ya usalama wa nchi na ushindani.
NOTA BENE
Adui anaweza kua na nguvu na uwezo, lakini tukamshinda kwa mikakati kisha tukamuangusha.
Katika nyanja zote
i) Siasa
ii) Uchumi na biashara
iii) Jamii
The Art of Strategy
The Eye That Never Sleeps
mfaumehassan@gmail.com
+255 745 624 754
Sent using Jamii Forums mobile app