Mfahamu samaki pomboo (Dolphin)

Mfahamu samaki pomboo (Dolphin)

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2018
Posts
21,709
Reaction score
35,704
Samaki ambaye humsaidia binadamu apatapo matatizo majini.

Kwa asili samaki huyu ni samaki anayekula nyama, hubeba mimba kwa miezi kumi mpaka 12 na huzaa mtoto mmoja au wawili, ni samaki mwenye kasi kubwa ya kusafiri majini, hatagi bali anazaa pia mtoto wake humnyonyesha, samaki huyu ana sifa nyingi sana alizonazo mwanadamu ukianza na hiyo ya kuzaa na kunyonyesha, lakini pia Pomboo hupendelea kuishi kifamilia.

Mara zote utapowaona huwa katika makundi, ni samaki msafi ambaye hapendi uchafu, ukirusha kitu majini yeye hukirudisha kwa kukipiga na mkia wake, midomo yao imechongoka na vijimeno vyake ni vidogo vidogo sana lakini hatari. Pamoja kwamba samaki ndio chakula chake kikuu lakini hupendelea sana kula pweza na fisi maji.

POMBOO ANA SIFA ZAKE ZA KUSTAAJABISHA

1. Ni samaki lakini anazaa na kunyonyesha.
2. Pamoja na huzaa kwake lakini anapozaa huanza kumtoa mtoto mkia na si kichwa.
3. Ana kasi kubwa sana majini.
4. Hupendelea kucheza muda mwingi
5. Mdomoni ana meno yapatayo 100
6. Wana namna yao ya kuwasiliana kwa lugha tena kwa sauti.
7.Ni kiumbe mpole na mwenye akili sana

URAFIKI WAKE NA MWANADAMU UKOJE SASA ?

NI ngumu sana kwa viumbe kukuta wana urafiki baina ya wanyama ya makundi tofauti mfano hakuna urafiki baina ya carnivores na herbivorous !

Walioliweza hili ni mamba na kiboko tuu, lakini hapa anajitokeza jamaa yetu POMBOO, huwezi kufa maji kama jamaa huyu anakuona unatapatapa ni samaki mwokozi kabisa, lakini pia huwezi kuzuliwa na samaki wakali kama papa, POMBOO akakuacha watakurinda kwa hali na mali.

Inapotokea umedumbukia majini na akakuona haraka sana hukufikia, kisha atakukumbatia na kwa spidi kubwa atakuwa anakupeleka nchi kavu, atakapofika jirani atakachokifanya ni kukurusha huko sasa msaada wake huwa unaishia hapo, ukitua kwenye jiwe, mwamba,michongoma, mtini shauri yako yeye kazi yake ashamaliza, pole utapewa na wengine huko.

Upo ushahidi pia kuonesha ya kwamba samaki POMBOO ashasaidia watu katika mazira mbambali kama hayo, mfano POMBOO pia meli zinapopita katika ukanda wao hupendelea kuzifuata, nahodha mmoja alipotambua POMBOO wanafuatilia chombo chake alimua kusimama ili aweze kuwatizama vyema, michezo waliyofanya POMBOO wale nahodha alihamasika kuingia majini ili aoge nao.

Unajua wezentu wazungu tena akimuona POMBOO anarudi kinyumenyume, anavua shati mwiso wa muda akajumuika nao majini, pasina ya kujua eneo hilo lilikuwa samaki mkorofi papa, hata hivyo pamoja na kujeruhiwa POMBOO walihakikisha wanamlinda nahondha huyo kwa kumzingira kisha wakawa wanatoa sauti za kutangaza hatari kwa papa, mpaka papa huyo alipoondoka kwa hasira, POMBOO wakamaliza kazi kwa kumrudisha nahodha huyo katika chombo chake kisha wao wakaendelea na mambo yao.

#KWA_TAARIFA_YAKO

1. POMBOO ndiye mnyama mwenye akili kuliko wote baada ya binadamu.
2. Kwa lugha yetu ya kiswahili POMBOO sio jina maarufu na hata nisingekutajia kwa kingereza kwamba ndiye samaki aitwaye #Dolphin ungebaki kujiuliza tuu huyu POMBOO ndio nani ?
3. Wanasayansi walibaini ya kwamba samaki POMBOO wanatambua ala za mziki na wakiusikia wanaweza kabisa kuucheza, na kuna kipindi kuna mipango ilianza kuwafungia sound za mziki wa blues ili waweze kuzaliana zaidi.
4. POMBOO ni samaki anayelindwa na umoja wa mataifa hivyo chunga sana matamanio yako, usijemuona pwani ya bongo ukamvua kudhani ni Mali ya nchi yako, utakuja kubebwa na jet za waamerika jioni ya siku hiyo hiyo.
5. Pamoja na wema wote huu wa POMBOO kwa mwanadamu lakini majangiri humuwinda na kumwuua.

6. POMBOO huwasaidia wavuvi katika shughuri zao za uvuaji wa samaki, kwa mfano ili wavuvi wapate samaki POMBOO hutumia mkia wake kuwapiga samaki wakubwa na yote hii hufanya kwa mapenzi aliyonayo kwa mwanadamu.

Kazi kwenu mnaotembea na selfie stick siku ukiwa majini ukamuona usisite kumfuata kwa ajili ya selfie, ni jamaa zetu hawa tena very friend, wapole na wakarimu kinoma, nikutakie maandalizi mema ya selfie.
FB_IMG_1558608943833.jpeg




 
Tunashukuru mkuu ila naomba niweke sawa hapo kwenye urafiki wa mamba na kiboko hawa jamaa sio marafiki ila wanajikuta wako pamoja kwa kuwa wote wanayahitaji maji na mamba anaujua mtiti wa boko ila mamba huwa anawatamani watoto wa niko

Kingine dolphin ni mammalia kutokana na sifa ulizozitaja
 
Kuna uzi mmoja walionusulika kifo cha maji ndo utajua maji si mchezo, huyo Dolphine atambe huko huko.
 
Huyu samaki anaweza kuishi kwenye maji baridi??

Several times namuona katika swimming pools wakicheza na wazungu au zile swimming pools zimewekwa maji ya baharini??
 
Ndio mkuu
huyu samaki anaweza kuishi kwenye maji baridi??

several times namuona katika swimming pools wakicheza na wazungu au zile swimming pools zimewekwa maji ya baharini??
 
kwamba wana akili kuliko binadamu sijakuelewa, labda sijui unavoielezea akili, ninachokijua ni kwamba wanatumia asilimia kubwa sana ya ubongo wao... kitu kinachowawezesha kutafsiri vitu ambavyo binadamu hatuwezi...
mfano, paka ana ubongo mdogo na anatumia asilimia kubwa ya huo ubongo wake kitu kinachomuwezesha kuwa na uwezo mkubwa wa kuhisi... na anaweza kuona vitu ambavyo wewe kama binadamu huwezi kuona ndicho kilichopo kwa dolphin..

by the way asante kwa maada nzuri
 
kwamba wana akili kuliko binadamu sijakuelewa, labda sijui unavoielezea akili, ninachokijua ni kwamba wanatumia asilimia kubwa sana ya ubongo wao... kitu kinachowawezesha kutafsiri vitu ambavyo binadamu hatuwezi...
mfano, paka ana ubongo mdogo na anatumia asilimia kubwa ya huo ubongo wake kitu kinachomuwezesha kuwa na uwezo mkubwa wa kuhisi... na anaweza kuona vitu ambavyo wewe kama binadamu huwezi kuona ndicho kilichopo kwa dolphin..

by the way asante kwa maada nzuri
amesema ni mnyama mwenye akili nyingi baada ya binadamu, matumizi ya kiwango kikubwa cha akili baada ya binadamu
 
nimekuelewa sana mkuu, naonaga wakipiga picture na binadamu najiuliza inakuaje kumbe wapo vzr ivyo.
 
Back
Top Bottom