Mfahamu Salma Kikwete

Mfahamu Salma Kikwete

Aisee kumbe huyu mmama akosoma shule yangu ya Msingi Ligula shule aliyosoma Mh. Sugu, Dknob,Rehema Mwakangakale r.i.p na Nizar Khalfan..... a.k.a shule ya watukutu na wasiopenda kusoma
 
Weeee kikwete ana watoto kibaoooo je wa Vick kamataa
 
Kuna mmoja nasikia yupo huku maeneo ya kinondoni pia ni mtoto wa mshuwa
 
Salma Rashid (kikwete). alizaliwa katika wilaya ya Lindi Mjini, Novemba 30, 1963. Baba yake anaitwa Rashid Yussuf Mkwachu na mama yake ni Mwanapaza binti Shariff.

Kwa asili, baba yake anatoka Sarai, Rufiji mkoani Pwani na mama yake anatoka Lindi.
Katika familia , upande wa mama, walizaliwa watoto saba, wasichana watatu na wavulana wanne. Yeye akiwa ni wa sita, ila kwa baba ni wa pili, ana kaka yake na mdogo yake. Na pia ana wadogo zake wengine watatu ambao wanachangia baba, kati yao wavulana ni wawili na msichana mmoja.
Baba yake alikuwa mfanyakazi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyovunjika mwaka 1977 na kituo chake cha kazi kilikuwa Mtwara, wakati baba yake anafanya kazi, mama alibaki Lindi, hali ambayo ilimfanya apate elimu yake ya msingi kuanzia mwaka 1973 katika shule nne tofauti; Nnaida ya Mikindani, Mtwara, Rahaleo ya Lindi, Ligula (Mtwara) na Stadium, Lindi ndipo ambapo alimalizia elimu yake ya msingi.
Ingawa wakati ule nafasi za kujiunga na sekondari zilikuwa chache, ailikuwa miongoni mwa waliochaguliwa.

Kukutana na Kikwete.
Kila jambo hupangwa na Mwenyezi Mungu. alilikutana na atakayekuwa mume yake mwaka 1985 akiwa katika Chuo cha Ualimu Nachingwea, yeye akiwa ni Katibu wa CCM wa Wilaya ya Nachingwea.

Walipokutana kwa mara ya kwanza kitu ambacho alimwambia ni kwamba" nakupenda na nataka nikuoe" hakusema anataka awe rafiki yake au vipi, sijui kama huo ndio utaratibu wa kina baba wote, kwa sababu alimpenda, alimkubalia, ingawa uamuzi wake hakuutoa papo hapo.
Walifunga ndoa Machi 30, 1989 wakati huo yeye akiwa Naibu Waziri wa Maji, Nishati na Madini. Baada ya kufunga ndoa walifanya taratibu za uhamisho kwa mujibu wa taratibu za kikazi.
Kwa hiyo walihamia Dar es Salaam ambapo aliungana na mume wake na wakawa wanakaa Mikocheni mtaa wa Ursino.
Wamejaaliwa watoto watano kati yao wanne ni wa kiume na mmoja wa kike. Wote wanasoma, wa kwanza yuko kidato cha sita, wa pili cha nne, wa tatu cha pili, wa nne yuko darasa la tano na wa mwisho yuko darasa la tatu.

Lakini kwa ujumla wana watoto wanane, ikiwa ni pamoja na watatu ambao mume wake alipata na mke wake wa kwanza.

Hawa wakubwa mmoja ni mwanasheria, mwingine ni daktari na mwingine ni mtaalamu wa Teknohama (Teknolojia ya Habari na Mawasiliano).

Ila siku zote hupenda kusema wana watoto wanane kwa sababu hata wale wakubwa amewalea yeyetangu wakiwa na umri mdogo sana. Kwa hiyo wale ni watoto wake sawa sawa na aliowazaa yeye.

Ahsante kwa kusoma na kuelewa kwa makini.

Sasa yule aliechana nae na kuoa Housegirl ni Yupi?
 
Tujifunze kuepuka Michepuko katka ndoa ili ndoa zidumu 1989 mpk leo sio mchezo.

Kwa akili yko kati ya hawo wawili hawajawai kuchepuka ata siku moja!?

Hakuna mafunzo hapo ni promo tu ya kwenda kuchukua jimbo la lindi, subiri utasikia tuuuuu mara bp, shell oilcom kwa mb wa huko mara chaliiiiiiiiiiiiiiiiiiii

Elimika sasa.
 

Attachments

  • Kuu.jpg
    Kuu.jpg
    67.8 KB · Views: 941
si kweli.alimuoa bado akiwa mwari na siyo mjane,au umetumwa wewe.

Vitu vingine mkiwa mnavisema badala ya kuwasifia mnaowalamba miguu ili njia zenu za msalani zisiote nyasi mnakuwa mnawachafua zaidi!
We we na huyo aliyekupa wazo la kuandika hizi majitaka zenu humu wote sio wazima!
 
Safi. Ndiyo rais anapaswa awe hivyo. Sio mtu mzima anachumbia. Babu mzima eti ana mchumba afu mara alitaka awe padre. Afu mara amedivorce haileti maana kwa kweli
 
Kijana unapotaka kuhadaa uma jipange!! Umesema wamejaliwa kupata watoto watano,wanne wa kiume na mmoja wa kike wote wanasoma!!
Wa kwanza form six,wa pili form four,wa tatu form two,wa nne darasa la tano na last born la tatu!!!

Umesema wa kike ndo mwanaisha!! Sasa mwanaisha ndo yuko form ngapi?? Maana form four mwaka 2012 alipata four!! Ina maana alirudia form four?? Kama yuko six kafikaje?? Maana kama ka reseat mwaka jana 2013 and matokea ndo yametoka mwezi juzi tu hapa!! Kajipange kwanza!! Unapenda kufagilia familia za wanene ili upewe ulaji?? umekosea sasa na hzo buku saba leo hupati

ni 2011 alipata 4
 
phoca_thumb_l_salma-kikwete.jpg

Mama Salma kikwete

MAMA SALMA ;

Swali: Ni ipi historia fupi ya maisha yako?
Jibu: Mimi naitwa Salma Rashid. Nilizaliwa katika wilaya ya Lindi Mjini, Novemba 30, 1963. Baba yangu anaitwa Rashid Yussuf Mkwachu na mama yangu ni Mwanapaza binti Shariff.

Kwa asili, baba yangu anatoka Sarai, Rufiji mkoani Pwani na mama yangu anatoka Lindi.

Katika familia yetu, upande wa mama, tulizaliwa watoto saba, wasichana watatu na wavulana wanne. Mimi ni wa sita, ila kwa baba ni wa pili, nina kaka yangu na mdogo wangu. Nina wadogo zangu wengine watatu ambao tunachangia baba, kati yao wavulana ni wawili na msichana mmoja.

Baba yangu alikuwa mfanyakazi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyovunjika mwaka 1977 na kituo chake cha kazi kilikuwa Mtwara, wakati baba anafanya kazi, mama alibaki Lindi, hali ambayo ilinifanya nipate elimu yangu ya msingi kuanzia mwaka 1973 katika shule nne tofauti; Nnaida ya Mikindani, Mtwara, Rahaleo ya Lindi, Ligula (Mtwara) na Stadium, Lindi ambapo nilimalizia elimu yangu ya msingi.

Ingawa wakati ule nafasi za kujiunga na sekondari zilikuwa chache, namshukuru Mwenyezi Mungu nilikuwa miongoni mwa waliochaguliwa.

Swali: Wewe unatoka Lindi na Mheshimiwa Rais anatoka Pwani, mlikutana wapi na mlifunga ndoa lini?

Jibu: Kila jambo hupangwa na Mwenyezi Mungu. Nilikutana na mume wangu mwaka 1985 nikiwa katika Chuo cha Ualimu Nachingwea, yeye akiwa ni Katibu wa CCM wa Wilaya ya Nachingwea.

Tulipokutana kwa mara ya kwanza kitu ambacho aliniambia ni kwambanakupenda na nataka nikuoe kusema kweli hakusema anataka awe rafiki yangu au vipi, sijui kama huo ndio utaratibu wa kina baba wote, lakini nasema kutoka moyoni, hicho ndicho alichoniambia na mimi kwa sababu nilimpenda, nilimkubalia, ingawa uamuzi wangu sikuutoa papo hapo.

Tulifunga ndoa Machi 30, 1989 wakati huo yeye akiwa Naibu Waziri wa Maji, Nishati na Madini.

Swali: Baada ya kufunga ndoa ikawaje?

Jibu: Baada ya kufunga ndoa nilifanya taratibu za uhamisho kwa mujibu wa taratibu za kikazi. Kwa hiyo nilihamia Dar es Salaam ambapo niliungana na mume wangu na tukawa tunakaa Mikocheni mtaa wa Ursino.

Swali: Katika miaka yenu hii 20 ya ndoa mmejaaliwa kupata watoto wangapi na wako wapi?

Jibu: Tunamshukuru Mwenyezi Mungu tumejaaliwa watoto watano kati yao wanne ni wa kiume na mmoja wa kike. Wote wanasoma, wa kwanza yuko kidato cha sita, wa pili cha nne, wa tatu cha pili, wa nne yuko darasa la tano na wa mwisho yuko darasa la tatu.

Lakini kwa ujumla tuna watoto wanane, ikiwa ni pamoja na watatu ambao mume wangu alipata na mke wake wa kwanza.

Hawa wakubwa mmoja ni Mbunge, mwingine ni daktari na mwingine ni mtaalamu wa Teknohama (Teknolojia ya Habari na Mawasiliano).

Ila siku zote napenda kusema tuna watoto wanane kwa sababu hata hawa wakubwa nimewalea mimi tangu wakiwa na umri mdogo sana. Kwa hiyo hawa ni watoto wangu sawa sawa na hawa niliowazaa mimi.

Swali: Una mipango gani ya baadaye?

Jibu: Kwa jumla mipango yetu katika taasisi ya WAMA ni mikubwa sana. Sasa ndio tumeanza, tuna shule moja tu, lakini tunatarajia kuongeza shule nyingi zaidi katika maeneo tuliyoyakusudia kwa sababu watoto wanaohitaji msaada wako wengi sana.
 
bora ungeweka yote hapa hapa, kuna kitu kinaitwa kaymu na tigo hata uzitoe vipi zinaziba maandishi
 
Back
Top Bottom