mcTobby
JF-Expert Member
- Feb 16, 2018
- 6,499
- 18,166
Ilikuwa ni siku ya jumatatu ya mwezi wa 9 mwaka 1983. Siku ambayo anga lilikuwa angavu na bluu ikimaanisha hali ya joto kiasi ndani ya makao makuu ya nchi ya marekani Washington d.c. Hakika siku na tarehe hii ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa na watu wengi na sio tu wamarekani bali karibia kila kona ya dunia. Watu waliamini kabisa historia mpya inaenda kuandikwa upya haswa kutokana na migogoro ya muda mrefu ikiwemo vita ,ugaidi pamoja na mauaji ya koholela pale mashariki ya kati . Na hususani mgogoro wa muda mrefu baina ya Israeli na Waarabu/wapalestina huenda ulikuwa unaandika historia mpya kabisa ya mapatano ya amani.
Sasa siku hii hapo Washington d.c kulikuwa bize sana maafisa wa ngazi za juu, waandishi wa habari na wageni maalumu walikuwa wakisubiri kutiliwa saini makubaliano ya kumaliza mgogoro kati ya Israeli na palestina.
Haya yakiendelea huko Washington d.c, siku hii pale kwenye viunga vya makao makuu ya CIA Langley Virginia yupo mmoja wa afisa wa ngazi za juu wa Shirika hilo aliwahi kufika ofisini siku hiyo kuliko kawaida akiwa ana mchanganyiko wa upweke,hasira na hali ya kuboeka. Afisa huyu hakuwa mwingine bali ni Frank Anderson mwenye umri wa miaka 51. Huyu afisa wa CIA alikuwa mkuu wa kitengo cha Clandestine operations( operesheni za siri za kijasusi)kwenye eneo la nchi za kiarabu na alikuwa na sababu ya kutabasmu kutokana na kufanikisha zoezi hili lililoratibiwa kule Washington d.c la kutia saini makubaliano ya kusitisha vita baina ya Israeli na Waarabu, lakini alikuwa hana furaha hata kidogo.
Siku hii ni kwamba rais Bill Clinton alikuwa amewaalika wageni zaidi ya 2000 kwenye ikulu ya whitehouse kwa ajili ya kushuhudia Yitzhak Rabin waziri mkuu wa Israeli na kiongozi wa kundi la kipalestina la PLO bwana Yasser Arafat wakitia saini mkataba wa amani.
Sababu hii iliyomfanya huyu Anderson kutokuwa na furaha siku hii ni kutokana na ukweli kwamba kati ya wageni hawa waalikiwa, Hakuna afisa wa CIA aliyealikwa katika hafla hii. Anderson aliamini mpango huu wa makubaliano ya amani ilikuwa ni operesheni ya kijasusi ya CIA iliyoanzishwa takribani miaka kumi iliyopita pale mashariki ya kati. Anderson aliamini whitehouse haikufanya fair katika kutotambua mchango wa CIA katika mafanikio haya.
Yaani mpaka ifikie hatua ya kusaini makubaliano ya amani kati ya Israeli na palestina halikuwa zoezi jepesi hata kidogo. Katika mchakato huu wa amani hadi kufikia hapo uliratibiwa kwa kiasi kikubwa na afisa wa CIA aliyejulikana kama Robert clayton Ames miaka ya nyuma hadi mauti ilipomkuta akiwa kazini huko Beirut Lebanon tarehe 18 April mwaka 1983.
Kivipi?
Tukirudi nyuma hadi hivi mwaka 1983.kulitokea shambulizi la kigaidi ndani ya mji wa Beirut Lebanon kwenye ubalozi wa marekani ambapo gari aina ya pickup iliyokuwa imebeba bomu kuendeshwa hadi kwenye viunga vya jengo la ubalozi wa marekani hapo Beirut na baada ya muda mfupi kulipuka. Ames siku hii alikuwa mmoja wa wahanga wa huu mkasa . Tunaweza kusema alikuwa wrong place at a wrong time. Tukio hili la kigaidi liliua wamarekani 16 ambapo saba kati yao walikuwa maafisa wa CIA(Ames akiwa mmojawapo). Pia liliua zaidi watu wengine 46 wakiwa raia wa Lebanon. Shambulizi hili lilikuwa la mara ya kwanza kwa Shirika la CIA kupoteza staff wake wengi kwa wakati mmoja ( maafisa 7).
Sasa basi siku hii bwana Anderson baada ya kufika makao makuu ya CIA saa tatu kamili asubuhi , moja kwa moja alihudhuria kikao cha wakubwa wake kwa ajili ya kupeana daily briefings za siku husika. Siku hii ilipangwa kwamba baadhi ya maafisa wangetembelea makaburi ya walipozikwa maafisa wa CIA waliokufa katika ubalozi wa marekani huko Beirut ikiwemo kaburi la Ames ambaye alikuwa kama shujaa aliyefanikisha mchakato huu wa amani.
Na kweli saa nne na nusu asubuhi kwenye geti mojawapo la kuingilia makao makuu, basi lilikuwa tayari limepaki kwa ajili ya kuwabeba maafisa wa CIA na baadhi ya staff karibia arobaini wa hapo makuu kwa ajili ya kuelekea kwenye makaburi ya Arlington kutoa heshima zao ya kuwaenzi mashujaa hao ingawaje wao waliona white house haikuwatendea haki katika kuwaenzi maafisa hao wa CIA waliofanikisha mchakato wa amani hususani kwa bwana Ames.
Na kweli msafara huu ulipofika kwenye makaburi ya Arlington yaliyopo karibu na Potomac river , majira ya 5 na dakika 43 asubuhi walitazama ng'ambo ya mto huu kwa umbali kiasi ilipo ikulu ya whitehouse . Waliamini Hafla iliyokuwa ikiendelea huko ilifanikishwa kwa kiasi pakubwa na mashujaa kadhaa ndani ya CIA wakiwemo miongoni mwa waliozikwa kwenye makaburi ya mashujaa ya Arlington. Na ni muda huo ndani ya white house zoezi la makubaliano ya kusitisha vita na kutiliana saini za kusitisha mapigano yaliyodumu kwa muda mrefu lilikuwa likiendelea.
Maafisa hawa wa CIA walitoa heshima zao akiambatana na sala ya kimya kimya kwa hawa mashujaa waliozikwa kwenye makaburi hayo. Walianza na kaburi la Robert Ames lililokuwa limeandikwa maneno haya;
" Robert Clayton Ames, Central Intelligence Agency of the United States of America, March 6, 1934–April 18, 1983" na kuliwekea maua juu yake. Frank Anderson alitoa hotuba fupi kuhusiana na huyu ames jinsi alivyoweza kujenga uhusiano na Ali Hassan salameh kiongozi wa kundi la wanamgambo wa PLO na pia mkuu wa kitengo cha ujasusi cha kiongozi wa palestina Yasser Arafat. Uhusiano uliopelekea viongozi hasimu yaani yithzak Rabin na Yasser Arafat kuamua kusaini mkataba wa amani ili kumaliza mgogoro baina yao na pia kuundwa kwa serikali ya palestina inayojitawala.
Pia walitembelea na kuweka shada la mauahadi kwenye kaburi la Afisa mwingine wa CIA aliyeitwa William Buckley ambaye alikuwa CIA station chief huyu aliuawa mwaka1984 baada ya kuteswa na magaidi akiwa hapo mashariki ya kati.
Waliozikwa hapo Arlington national cemetery ambapo hawa maafisa wa CIA wakiongozwa na Frank Anderson waliweza kuwakumbuka na kuwawekea mashada ya maua ni pamoja na James na monique Lewis ambao pia walikufa pamoja na Ames kwenye mkasa wa kulipuka kwa bomu kwenye ubalozi huo wa Marekani hapo Beirut . Hawa wote walikuwa waajiriwa wa CIA.
Na mwisho walizuru kaburi la Kenneth Haas ambaye naye alikuwa CIA station chief wakati mkasa huu unatokea na mwishowe kabisa walimaliza kuweka shada la maua kwenye kaburi la Frank Johnston anbaye naye alikuwa mwajiriwa wa CIA. Ilikuwa ni siku ya huzuni sana kwa hawa maofisa wakiongozwa na Frank Anderson. Hii ilikuwa ni idadi kubwa kabisa kwa Shirika la CIA kupoteza maofisa wake kwa wakati mmoja. Lakini hii yote ni gharama ambapo marekani waliilipa kutokana na kutaka kusuluhisha vita kati Israeli na palestina . Marekani aliamini sasa Mwisraeli na mpalestina wataishi kama ndugu.. lakini haikuwa hivyo mpaka sasa mgogoro haukuwahi kuisha. Na la zaidi ni kwamba hata Waisraeli wenyewe hawakukubaliana na hili swala la kupatana na mahasimu wao.. Lakini huyu Robert Ames ni nani na mchango wake ulikuwaje katika haya yote mpaka kuwa na urafiki na kiongozi wa ugaidi Ali Hassan salameh a.k.a the red prince?