Mfahamu Mtemi Ngeleja wa pili.

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,136
4,297




Sanaa ya ushairi kwa zama za sasa ni sanaa ambayo licha ya muitikio kuwa mdogo kwa jamii yetu lakini bado watu wengi wanazidi kujikita katika kuikuza na kuendeza sanaa hiyo kwa ajili ya kizazi cha sasa na kizazi cha sasa na kizazi kijacho.
Watu wengi kwa sasa wanazidi kufanya kila njia kwa maendeleo ya sanaa hii kongwe kabisa dunia.
Mtemi Ngeleja ni jina maarufu katika mitandao ya kijamii hasa kwa wale ambao wanapenda sana kufuatilia sanaa yua ushairi watakubaliana name.

Ukiingia katika mitrandao ya washairi Tanzania utakutana na jina hili ambalo limebobea katika utunzi na umahiri wa mashairihasa yale yakimapokeo.
Mtemi ngeleja ni nani ?
Jina halisi anajulikana kama Baraka Nicholous Ngeleja ama kwa jina maarufu Mtemi Ngeleja likiwa ni jina analopendelea kujiita ili kujitambulisha katika jamii ya washairi.
Kila mshairi anakuwa na jina lake la ushairi na Baraka Ngeleja anapenda kujiita Mtemi Ngeleja II kama sehemu ya kumuenzi babu yake mzee Ngeleja ambae ni babu mzaa baba.

Mtemi Ngeleja alianza kuandika mashairi yake mnamo mwaka 2012 akiwa anaandika mashairi katika mfumo wa mashairi ya huru na miaka miwili baadae yani mwaka 2014 aliamu kubadilika kutoka katika mfumo wa mashairi ya huru na kuingia katika uandishi wa mashairi ya kimapokeo au mashairi yale yazingatiayo kanuni na sheria za ushairi.

Mtemi Ngeleja anasema anapenda sana kuandika mashairi ya kimapokeo kwa sababu yanaleta uimbikaji wake kuwa mzuri.
Ukitazma mgumo wa mashairi ya kimapokeo yanakuwa ni rahisi sana kuimbika kkwa sauti zaidi ya moja au zaidi ya kumi kuendelea na hali hiyo huleta raha kwa msomaji,msikilizaji na hata mtunz.
Mtemi Ngeleja anasema,watu wengi hupenda kuandika mashairi huru kwa kuwa ni rahisi kwani hayaangalii wala kuzingatia sheria za ushairi.
Mtemi anawashauri watu wengi kuwekeza katika ushairi wa kimapokeo kwa sababu ni aina ya ushairi unaovutia sana na una mamo mengi ndani yake tofauti na aina nyingine ya ushairi.
Mwaka 2017,Mtemi ngeleja aliamu kuanzisha kurasa maalumu kwa lengo la kuwakutanasha washairi na wapenzi wa ushairi duniani,kupena elimu na kusambaza kazi mbalimbali za washairi duniani.




Mtemi Ngeleja ni muaasisi wa page hiyo maarufu kwa jina la USHAIRI INITIATIVES & POEMS PROJECT au UPP ambayo mpaka sasas inawanachama toka sehemu mbalimbali duniani,ikiwemo Tanzania,Kenya,Rwanda,Nigeria,GhanaIndia na sehemu nyingine za duniani ambapo washairi hukutana na kubadilishana kazi zao.
Anasema,mbali na washairi kukutana katika UPP pia lengo lake nyingine ni kutaka ushairi upatikane katika mitandao yote ya kijamii.
Anasema lengo linguine kubwa la kuanzishwa kwa UPP ni kusaidia washairi kuchapa vitabu na mpaka sasa taratibu za kutoa kitabu cha mashairi zinaendelea ingawa mwaka wa jana 2017 alifanikiwa kutoa kitabu kwa lugha ya kingereza kiitwacho "THE TROPICAL SONGS"
Mtemi Nngeleja anasema mpaka sasa kupitia kazi yake ya ushairi amefanikiwa kupata marafiki wengi toka pande mbalimbali za dunia.
Anaendelea kusema kuwa hivi sasa kazi za ushairi zinapatika kwa wingi hivyo kuwaomba watanzania kuwaunga mkono kwa kusoma kazi zao ambao zinaelezea maisha yao halisi ya kila siku.
Nilimuuliza,NINI KIFANYIKE ILI KULETA MABADILIKO NA MAENDELEO KATIKA SANAA YA USHAIRI ?

Haya yalikuwa majibu yake :

WASHAIRI TUNAPASWA KUANDIKA MASHAIRI AMBAYO YANAIGUSA JAMII BILA KUSABABISHA MGONGANO ULIO WAZI NA TABAKA LOLOTE, LAKINI PIA JAMII INATAKIWA KUUNGA MKONO JITIHADA ZA WASHAIRI KWA KUNUNUA KAZI ZETU PAMOJA NABKUTOA USHAURI KIPI TUBORESHE ILI KUFANYA USHAIRI UWE NURU KWA JAMII ZETU. MWISHO, SIKU ZOTE NASISITIZA SANA UMOJA BAINA YA WASHAIRI, HII ITATUFANYA TUTAMBUANE NA TUGANYE KAZI KWA NGUVU ZOTE. ASANTE SANA.
Makala hii imeandikwa na Idd Ninga wa Arusha Tanzania.
+255624010160.
 
Back
Top Bottom