Mfahamu mdudu kunguni (bedbugs) na jinsi ya kumuangamiza

Soma vizuri mkuu nilichoandika, unaweza ukawa msafi ila kuna wachafu wengine wametumika kuzalisha kunguni na ndio maana wakawa transfered kutoka kwa washikaji wako kuja kwako maana kama wangekuwa wanajielewa wewe usingewapata...ni sawa na tunapoambiwa ukiugua kipindupindu ni kwamba umekula mavi na sio wote wanaougua kipindupindu wamekula mavi directly bali alisalimiana na mgonjwa ama katika kumhudumia mgonjwa akajikuta ameukwaa ugonjwa kwa bahati mbaya. Ndivyo na kunguni hivyo hivyo kuna watu wamejenga mazingira ya kunguni kuwa sehemu ya maisha yao na mwisho wa siku wanafanya kuwahamisha...kunguni akiwepo ndani kwanza shuka tu zinachoka na kama mtu amekaa nao mpaka anakuletea wewe unadhani hilo gheto lake likoje mkuu kama sio chafu (uchafu sio lazima kuoga kila siku hata kurundika nguo, kuweka viatu ovyo nakadhalika
 
Jumla DAWA ya LARVA
 
hao jamaa kunguni - land rover 109, wako fasta ajabu.....yaani utoe kila kitu nje ndio upulize dawa....wanaenea kwa kasi ya ajabu..
 
Mkuu kanunue ddt ndio kiboko yao hutakaa uwaone tena maishani mwako. Cha kufanya ni hiyo dawa na vipimo vyake unaua hadi mayai kwishney hutawasikia tena hapo unapokaa. Kama wamezidi sana hiyo dawa paka kwenye hizo conner za vitanda na kabati kavu usidilute na maji paka hivyo hivyo habari yao utaimaliza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wakuu!. Naomba msaada kwa anayejua dawa ya kumaliza kunguni kwa haraka.

Msicheke nafanya usafi wote lakini bado nimepulizia rungu wapi, na sijui niliwatoa wapi nina wasiwasi na kwenye basi moja la mkoani.

=========




Kunguni ni wadudu wadogo wa familia Cimicidae katika oda Hemiptera ya nusungeli Pterygota (wenye mabawa). Mara nyingi huishi katika mazingira ya kificho na yenye mlundikano wa uchafu utokanao na taka mwili, hasa vitanda ambamo hufyonza damu ya watu au wanyama kama chakula chao, hasa usiku.

Spishi
Spishi muhimu sana ni kunguni wa Ulaya (Cimex lectularius). Inatokea duniani kote mahali ambapo watu wanaishi. Katika Afrika kuna spishi nyingine muhimu, kunguni wa Afrika (Cimex hemipterus). Spishi ya tatu, kunguni magharibi (Leptocimex boueti), inatokea Afrika ya Magharibi na Amerika ya Kusini na hupendelea damu ya popo, lakini hufyonza damu ya watu pia mara nyingi.

Biolojia
Kunguni hujilisha damu tu, lakini wanaweza kuishi mwaka mzima bila kula. Wapevu ni wa rangi ya hudhurungi hadi kahawianyekundu, wana umbo la duaradufu bapa na hawana mabawa ya nyuma. Mabawa ya mbele hayafanyi kazi na yamepunguzwa kwa miundo kama pedi. Wapevu hukua hadi urefu wa mm 4-7 na upana wa mm 1.5-3.

Wadudu hao wana hatua tano za maisha kama tunutu na hatua ya mwisho ya upevu. Huambua ngozi yao mwishoni mwa kila hatua, wakitupa kiunzi chao cha nje. Tunutu wakitoka mayai ni wangavu, wenye rangi isiyoiva na wanakuwa kahawia kadiri wanapoambua ngozi na kufikia upevu. Kunguni wanaweza kudhaniwa kuwa wadudu wengine, kama vile chawa-vitabu, mende wadogo au mbawakawa-zulia, lakini wakipata joto na kufanya shughuli, mwendo wao ni ule wa sisimizi, na, kama kunguni-mgunda wengi, wakisetwa hutoa harufu bainifu inayononga.

Kwa sababu kunguni ni wafyonza damu shuruti, wana sehemu za kinywa ambazo zinakeketa ngozi na kuingiza mate yenye dutu dhidi ya mgando na viondoa maumivu. Kiwango cha hisia cha wanadamu kinatofautiana kutoka athari mbaya ya mzio hadi kutokuwepo kwa athari yoyote (karibu 20%). Kwa kawaida umo hutoa uvimbe bila doa nyekundu, lakini wakati kunguni wengi hujilisha kwenye eneo dogo, madoa mekundu yanaweza kuonekana baada ya uvimbe kupungua. Kunguni hupendelea ngozi wazi, haswa uso, shingo na mikono ya mtu aliyelala.

Kunguni huvutiwa na vidusiwa wao kwa dioksidi ya kaboni hasa, kisha kwa joto, na pia kwa kemikali fulani. Kunguni wa Ulaya hujilisha kila siku tano hadi saba tu, ambayo inadokeza kuwa hatumii muda mrefu sana wa maisha yake kutafuta kidusiwa. Kunguni akiwa na njaa, huondoka makazi yake na kutafuta kidusiwa. Anarudi kwenye makazi yake baada ya kujilisha vizuri au ikiwa anakabiliwa na mwanga. Kunguni wa Ulaya hujumuika kwa hatua zote za maisha na hali za kukomaa. Kunguni wanachagua kujumuika labda kwa sababu ya umbuai, nguvu kinzi dhidi ya ukaushaji na fursa zaidi za kupata mwenzi. Feromoni zinazotumwa na hewa zina jukumu la jumuiya.

Mweneo

Uingiaji wa kunguni mahali papya husababishwa na ukosefu wa usafi mara chache tu. Kwa kawaida uhamisho kwa maeneo mapya huwa katika vitu vya binafsi vya wanadamu ambapo wanajilisha. Makazi yanaweza kuingiliwa na kunguni kwa njia tofauti, kama vile:
  • Wadudu na mayai yaliyoletwa kutoka kwa makazi mengine yaliyokuwa nayo kwenye mwili wa mgeni au mavazi au mizigo yake;
  • Vitu vilivyo na kunguni (kama vile samani, haswa vitanda na kochi, mavazi au shanta) vinavyoletwa katika nyumba au jengo la biashara;
  • Ujirani wa makazi yaliyo na kunguni, ikiwa njia rahisi za kupitia zinapatikana, k.m. mifereji au dari bandia;
  • Wanyama-mwitu (kama vile popo au ndege) walio na kunguni au spishi ndugu kama kunguni-popo.
Ingawa kunguni watajilisha juu ya wanyama vipenzi nafasi ikitukia, hawaishi au kusafiri kwenye ngozi ya vidusiwa wao na wanyama vipenzi hawafikiriwi kuwa sababu ya kuenezwa kwao.

Ishara na dalili

Ngozi
Athari za binafsi za maumo hutofautiana na kwenda kutoka kutokuonekana kwa athari (20-70%) hadi madoa madogo na hata vivimbe pamoja na mwasho mkali unaoweza kudumu siku kadhaa. Maumo yapo katika safu mara nyingi. Doa la kati litoalo damu linaweza kuwapo kwa sababu ya kufeleti kwa dutu dhidi ya mgando katika mate ya mdudu.

Dalili labda hazionekani mpaka siku kadhaa baada ya maumo kutukia. Athari zinakuwa kali zaidi baada ya maumo mengi kwa sababu inawezekana kama protini katika mate ya kunguni huhisisha ngozi. Athari ya ngozi hutukia kwa kawaida katika eneo la umo ambalo mara nyingi sana ni mikono, mabega na miguu kwa sababu imefiduliwa usiku kwa kawaida. Maumo mengi yanaweza kusababisha ugonjwa wa mabaka ngozini.

Elimunafsia
Uwepo wa mashambulio tele na ya kudumu yanaweza kusababisha wasiwasi, dhiki na kukosa usingizi. Inawezekana mtu aanze kufikiri kwamba vidusia wapo lakini hawapo kwa kweli, kwa sababu anafikiria sana kunguni kila wakati.

Nyingine
Dalili nyingine kadhaa zinaweza kutukia kwa sababu ya maumo ya kunguni au kusikia harufu yao. Anafilaksisi iliyosababiswa na uingizaji wa protini za mate ya kunguni imeripotiwa kwa nadra. Kwa sababu kila umo linachukua kima kidigi cha damu, uwepo wa kudumu wa kunguni wengi unaweza kusababisha anemia.

Ambukizo la ngozi na bakteria linaweza kutukia kwa sababu kujikuna kunaweza kufungua ngozi na hii inaweza kusababisha kusumu damu kote ikiwa kuna maumo mengi sana.

Kusikia harufu ya kunguni kunaweza kuchokonoa shambulio la pumu kwa sababu ya vizio katika hewa, ingawa ithibati ya mwungano huu ni ndogo.

Hakuna ithibati ya kwamba kunguni wanaeneza magonjwa ya kuambukiza, hata ingawa wanaonekana kuweza kubeba pathojeni na uwezekano umechunguzwa. Umo lenyewe linaweza kuleta uchungu ambao unasababisha usingizi mbaya na utendaji mbaya wa kazi.

Mithili ya wanadamu, wanyama wa kipenzi wanaweza kuumwa na kunguni pia. Ishara zilizoachwa na maumo ni sawa na kisa ya watu na dalili zinafanana (kuwasha ngozi, kujikuna n.k.).

Utambuzi
Utambuzi dhahiri wa athari za kiafya zinazosababishwa na kunguni unahitaji kutafuta na kuona wadudu katika mazingira ya kulala kwani dalili siyo maalum ya kutosha. Kwa kawaida kunguni hufanya safu ya maumo yanayoitwa kimazungumzo "kiamshakinywa, chakula cha mchana na chakula cha jioni". Pia kwa nadra hujilisha kwenye kwapa au nyuma ya magoti ambayo inaweza kusaidia kuwatofautisha na wadudu wengine wanaouma.

Dalili hizi zinaweza kuchanganywa na hali za afya zifuatazo: upele (unaosababiswa na matitiri ya watu na ya ndege), athari za mzio, maumo ya mbu na buibui, tetekuwanga na maambukizo ya ngozi yanayosababishwa na bakteria.

Ugunduzi
Kunguni wanaweza kuweko peke yao, lakini huwa hukusanyika ikiwa wamelowea. Ingawa ni vidusia madhubuti, hutumia sehemu ndogo tu ya maisha yao wakishikamana kimwili na vidusiwa. Mara kunguni akimaliza kujilisha, huhamia mahali karibu na kidusiwa anayejua, kwa kawaida katika au karibu na vitanda au kochi kwenye vikundi vya wapevu, wachanga na mayai, ambapo bingwa wa wadudu huita maeneo ya bandari au bandari tu ambapo mdudu hurudi baada ya kujilisha akifuata nyayo za kemikali.

Maeneo haya yanaweza kutofautiana sana katika muundo, pamoja na mizigo, ndani ya magari, katika samani, katikati mparaganyo kando ya vitanda, hata ndani ya soketi za umeme na katika tarakilishi za karibu. Kunguni zinaweza kukaa pia karibu na wanyama ambao wameweka kiota ndani ya makazi, kama vile popo, ndege au panya. Pia wanaweza kuishi juu ya paka na mbwa wa kipenzi, ingawa binadamu ndiye kidusiwa anayependelewa na kunguni wa Ulaya.

Ikiwa idadi katika nyumba ni kubwa, harufu tamu na chungu inaweza kusikiwa ambayo inafanana na harufu ya rasiberi zinozooza. Mbwa wagundua kunguni hufunzwa ili kuonyesha mahali kamili pa uwepo wao, ambayo ina kiwango cha ugunduzi kati ya 11% na 83%.

Uzuiaji
Ili kuzuia kuleta kunguni nyumbani, wasafiri wanashauriwa kuchukua tahadhari baada ya kutembelea mahali palipoathiriwa: kwa ujumla hii ni pamoja na kuangalia viatu wakati wa kuondoka mahali hapa, kubadilisha nguo nje ya nyumba kabla ya kuingia na kuweka nguo zilizotumiwa katika kikausha nguo nje ya nyumba. Wakati wa kutembelea nyumba mpya ya kulala, inashauriwa kukagua kitanda kabla ya kuleta masanduku katika eneo la kulala na kuweka sanduku juu ya jukwaa ili kupunguza uwezekano wa kuingia ndani kwa kunguni.

Inapaswa kutundika nguo au kuziacha katika sanduku na kamwe kuziacha kwenye sakafu. Mwanzilishi wa kampuni iliyojitolea kuangamiza kunguni alisema kwamba 5% ya vyumba vya hoteli alivyochukua vilikuwa vimeathiriwa. Alishauri watu wasikae chini kwenye usafiri wa umma, wakague viti vya ofisi, viti vya ndege na magodoro ya hoteli, na waangalie vizuri vitanda vya nyumbani na kuvipigia kivuta vumbi mara moja kwa mwezi.

Udhibiti
Tiba inahitaji kuzuia mtu asiumwe tena na tena na labda kutumia antihistimini na kortikosteroidi kidalili (ama kwa mahali au kupitia mfumo wa damu). Lakini hakuna ithibati kwamba dawa zinaleta matokeo mazuri zaidi na kwa kawaida dalili zinaisha bila matibabu katika wiki 1-2.

Kuzuia maumo kunaweza kuwa ngumu, kwa sababu kunahitaji ukomeshaji wa kunguni katika nyumba au ofisi. Hii ni ngumu mno kwa vitendo na kwa kawaida inahitaji mchanganyiko wa njia za viuawadudu na njia bila viuawadudu. Vile vilivyoonwa kufaa zamani vinajumuisha piretroidi (dawa zifananazo na pareto), dichlorvos na malathion, lakini nguvu ya kukinza dawa imezidi sana sasa na matumizi yao yana athari mbaya kwa afya. Sikuhizi hakuna kiuawadudu kinachofaa.

Njia za umakanika, kama vile kutumia kivuta vumbi na kuwekea magodoro joto au kuyafunika kabisa, zinafaa mara nyingi. Muda wa saa moja kwa nyuzijoto ya 45ºC au zaidi ama muda wa masaa mawili kwa chini ya -17ºC unaua kunguni. Kikausha nguo cha nyumbani au stima ya kibiashara zinaweza kutumiwa. Kuwanyimia kunguni chakula hakufanyi kazi kwa sababu wataendelea kuishi muda wa siku 100 hadi 300 kulingana na nyuzijoto.
 
Mkuu dawa ya kunguni sio dawa za kununua madukani... hawa wadudu hawarespond na hizo dawa hata kidogo.

Solution ni kuchemsha maji ya motoooo then mwagia chaga na kitanda chote kwa ujumla.

Then chukua godolo ulipige pasi(ule moto wa mwisho kabisa) .
Then fua mashuka kwa maji ya motooo sana..

Rudia hio procesure kil weekend kwa mwezi mmoja utakuwa umewamaliza kunguni woote
 
Habari wakuu!. Naomba msaada kwa anayejua dawa ya kumaliza kunguni kwa haraka. Msicheke nafanya usafi wote lakini bado nimepulizia rungu wapi, nasijui niliwatoa japo nna wasiwasi na kwenye basi moja la mkoani.
Nunua mafuta ya taa weka kwenye chupa tupu ya maji,toboa pale juu halafu nyunyuzi kila eneo unaloona watakuwa wamejificha kitandani kwenye Kona toa godoro pia uangalie kama ni mayai yapulizie,Fanya hivyo kila asubuh angalau Kwa siku 3 uangalie matokeo
 
Habari wakuu!. Naomba msaada kwa anayejua dawa ya kumaliza kunguni kwa haraka. Msicheke nafanya usafi wote lakini bado nimepulizia rungu wapi, nasijui niliwatoa japo nna wasiwasi na kwenye basi moja la mkoani.
Mkuu wakati mwingine kabla hujaanzisha thread ebu jaribu kusearch kwa kichwa cha habari kinachofanana na thread yako uloikusudia, kwa sababu unaweza kuona kama unaleta thread mpya kumbe imejadiliwa mda mwingi huko nyuma.

Search thread ya kunguni ipoo humu utajifunza mengi huko..
 
Hiyo kazi kubwa dawa yao mafuta ya taa
 
Kuna bobi aliwahi kusema haya mafuta ya kula haya.

Unayapaka kwenye sehemu unapohisi wapo mkama kitandani unapaka kama unapiga banish vileeee.

Hapo unawaondoa kabisa
 
Habari wakuu!. Naomba msaada kwa anayejua dawa ya kumaliza kunguni kwa haraka. Msicheke nafanya usafi wote lakini bado nimepulizia rungu wapi, nasijui niliwatoa japo nna wasiwasi na kwenye basi moja la mkoani.
 
Hiyo kazi kubwa dawa yao mafuta ya taa
Mkuu trust me kunguni humuui kwa chemicals.
Wale wadudu ni wagumu kufa sijapata kuona...mimi nimepambana na kunguni kwa njia zote nimekuja kuwapiga kwa njia ya maji ya moto tu
 
Mkuu trust me kunguni humuui kwa chemicals.
Wale wadudu ni wagumu kufa sijapata kuona...mimi nimepambana na kunguni kwa njia zote nimekuja kuwapiga kwa njia ya maji ya moto tu
Dah ulifanyaje sasa..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…