Naomba msaada wa Dawa ya kuua (bedbugs) kunguni

Zuia Sayayi

Zuia Sayayi

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2011
Messages
843
Points
225
Zuia Sayayi

Zuia Sayayi

JF-Expert Member
Joined Mar 28, 2011
843 225
Naombeni mnisaidie dawa itakayo maliza kunguni maana wamevamia chumba changu
na pia nimeckia ile dawa ya RUNGU spray yaweza ua kunguni je hii ni kweli?

Msaada please namna ya kuwatoa hawa wadudu!
fb_img_1530639563871-jpg.801832

Jamani kunguni wamevamia kitanda changu leo siku ya tatu.... yaani usiku wa jana sijalala kabisa wamenishambulia vibaya mno... hapa mwili wote umevimba,unawasha na unauma..
mwenye dawa ya kuua kunguni na wasirudi tena anitajie maana nshatumia dawa kibao bila mafanikio...
msaada wenu wakuu maana daaaah hawa wadudu watanitoa roho mwaka huu... wananitesa sana,nashindwa kufurahia maisha hasa inapofika usiku.
Baadi ya michango ya wadau;

Kwan upo mkoa gani mkuu?
Hawa wadudu siwapendi katka maisha acha tu! Na hawa wadudu wanatabia moja unaweza kuwa unang'atwa kila siku lkn usiwajue labda uwe na usingiz wa juujuu tu yaan uking'atwa ndo ushituke uwashe taa gafla ndo utawaona wanavyo toka nduki!
hii pia ni kwa wale ambao hamna kungun kwao kuna vimende vidogo dogo vinapenda giza sana na huwa vinapenda sana maeneo ya kabati la vyombo, jikon jikon na ktk vyombo tena kukiwa giza, ukiwasha taa au kufungua mlango wanasambaa kurudi viti,makoch, kabatin na kwenye mbao za kitanda! Ilishawi tokea wife kaenda sehem wenyej ni smart na masista duu mbaya lkn hawan time na vitanda sijui walikuwa ni walalafi usiku wanang'atwa hawajielewi sjui? Ndo kuanza kuwasaidia!!

tuachane na hayo Mimi yameshawah kunikuta kiukweli nilitumia dawa nyingi sana baada kuwashtukia kuwa ndo wao wananipa vipele vimoja vimoja mgongon mi nikijua ni chunusi hapa nshang'atwa kama miez 6 hivi!!
Nenda ktk duka la dawa za mifugo,mimea au kilimo hasa duka la kilimo
nunua dawa moja inaitwa DEEP inanuka/nukia sana af pia ni sumu hata kwa binadamu, then utanunua hand sprayer Mf. Wake ni pale baada ya kunyoa saloon/babershop huwa tunapuliziwa maji fulan ya sabun.
Utachanganya maji lita 1:kifuniko 1 cha chupa ya dawa
hii dawa rangi yake kama maji lkn ina unjano kwa mbaali
ukiichanganya na maji tu inageka kuwa kama maziwa yaan nyeupe pee!
Hapo mkuu ukipuliza hata mbu akijipendekeza unamkuta chini
mimi kazi ilifanyika siku moja tu na mpaka nakuja kuoa mwaka jana sijawahi kuona hata mende ndani kwangu!!!

tumia hii dawa Mkuu utaleta feedback tu! Basi wamekulogelezea hao wadudu!!
Nenda kwenye duka la dawa za mifugo nunua dawa inaitwa nuvan mls 100. Sawa na ujazo wa chupa ndogo ya dawa ya kikohozi.ujazo huo changanya na maji lita kama tano tumia fagio kama huna pump ya kunyunyizia .nyunyiza nyumba nzima,kabati ,mabegi,vitanda.funga nyumba masaa kama matano hivi.kumbuka dawa ni sumu kali andaa maji ya kunawa vizuri baada ya kazi vyombo vya kulia aina yote ya chakula weka nje! Utanambia kama kuna kiumbe kitasimama
Uchafu sio sababu kubwa ya Kunguni hata kama ni pasafi/msafi kukiwa na mbegu ya Kunguni basi wataenea sana na athari ya Kunguni ni kwamba wanaleta Homa kali sana, LAKiNI njia ya kupunguza Kunguni ni kuweka nyumba ktk Hali ya usafi lkn kikubwa kama wapo kitandani au sehemu za kuta kwenye nyumba chemsha maji ya moto then mwagia sehemu hizo kama njia ya Kuwapunguza lkn nenda kwenye maduka ya madawa na mifugo utapata dawa elekezi
KUFIKIA katikati ya karne ya 20, ilionekana kwamba wanadamu wamefaulu kuwadhibiti kunguni. Watu fulani walifahamu kunguni kupitia tu wimbo wa zamani wa Kiingereza ulioimbwa na watoto wa shule za nasari (au chekechea) uliosema: “Usiwaache kunguni wakuume.” Hata hivyo, katika miaka ya 1970, nchi nyingi ziliamua kupiga marufuku matumizi ya dawa ya DDT—iliyokuwa dawa kuu ya kuua kunguni—kwa kuwa ilikuwa yenye sumu na iliharibu mazingira.

Hata hivyo, kemikali nyingine zilipotumiwa ilionekana kwamba kunguni walikuwa sugu na hazikuwaua. Pia watu walianza kusafiri mara nyingi zaidi na bila kujua walihama pamoja nao. Matokeo yakawaje? Ripoti moja ya mwaka wa 2012 kuhusu kuwadhibiti wadudu hao inasema: “Katika miaka 12 ambayo imepita kunguni wameanza kuonekana tena nchini Marekani, Kanada, Mashariki ya Kati, nchi kadhaa za Ulaya, Australia, na katika sehemu fulani za Afrika.”

Huko Moscow, Urusi, katika mwaka mmoja hivi karibuni, ripoti za kutokea kwa kunguni ziliongezeka mara kumi kuliko ilivyokuwa hapo awali. Wakati huohuo, upande ule mwingine wa ulimwengu, huko Australia, kumekuwa na ongezeko la asilimia 5,000 la kunguni tangu mwaka wa 1999!

Watu fulani hubeba kunguni bila kujua wanapoenda dukani, kwenye kumbi za sinema, au hotelini. “Upende usipende utabeba kunguni,” anasema meneja fulani wa hoteli nchini Marekani. “Maadamu hoteli inapata wateja lazima kunguni wataendelea kuwapo.” Kwa nini ni vigumu kiasi hicho kuwamaliza kunguni? Unaweza kujilindaje? Kunguni wanapovamia nyumba yako, unaweza kuchukua hatua gani zinazofaa ili kuwaondoa na kuwazuia wasirudi tena?

Wadudu Wasiokufa kwa Urahisi

Kwa kuwa wadudu hao ni wadogo kama mbegu ya tofaa na wana mwili bapa, kunguni wanaweza kujificha mahali popote pale. Wanaweza kujificha katika godoro lako, fanicha zako, sehemu ya ukutani ya kuunganishia vitu vya umeme, au hata kwenye simu yako. Kwa kawaida kunguni hupenda kujificha mita tatu hadi sita kutoka kwenye vitanda na maeneo ya kuketi. Kwa nini? Ili wawe karibu na chakula chao, yaani, wewe!*

Mara nyingi, kunguni huwauma watu wanapolala. Hata hivyo, watu wengi hawahisi wanapoumwa kwa sababu mdudu huyo humdunga mtu kitu kinachogandisha kinachomwezesha kuendelea kula kwa dakika kumi hivi bila kukatizwa. Na ingawa kunguni wanaweza kula kila juma, imesemekana kwamba wanaweza kuendelea kuishi bila kula kwa miezi mingi.

Tofauti na mbu na wadudu wengine, inaonekana kwamba kunguni hawaenezi magonjwa ya kuambukiza. Hata hivyo, wanapomuuma mtu wanatokeza mwasho na baadaye sehemu hiyo inavimba, na watu wengi huathiriwa kihisia. Watu walioumwa na kunguni wanaweza kupoteza usingizi, kuaibika, na hata kufikiri kwamba kunguni amewauma muda mrefu baada ya wadudu hao kutoweka. Jarida moja nchini Sierra Leone linasema kuwa kunguni “ni wasumbufu sana na wanawakosesha watu usingizi” na linaonya kuhusu “aibu inayohusianishwa na kunguni.”

Kuwadhibiti Kunguni

Kunguni wanaweza kumsumbua mtu yeyote. Ni rahisi kuwadhibiti ukitambua mapema kwamba wapo. Kwa hiyo, jifunze kutambua ishara za kwamba wapo nyumbani na unaposafiri. Chunguza fanicha zako na vitu vingine vya mbao pamoja na mizigo, uone ikiwa kuna mayai madogo yanayofanana na mbegu ndogo nyeusi au alama za damu. Tumia tochi unapowatafuta kunguni ili uweze kuwaona.

Usiruhusu kunguni wawe na sehemu nyingi za kujificha. Ziba nyufa zote ukutani na kwenye viunzi vya milango. Ingawa kunguni hawaletwi na uchafu, itakuwa rahisi zaidi kuwatambua na kuwadhibiti ikiwa unasafisha nyumba kwa ukawaida na kupunguza vitu vilivyorundamana. Ukiwa hotelini, unaweza kupunguza uwezekano wa kubeba kunguni kwa kuepuka kuweka masanduku yako sakafuni na kitandani.

Kunguni Wanapovamia Nyumba Yako

Ukipata kunguni nyumbani au hotelini, huenda ukawa na wasiwasi au hata ukaaibika. Dave na mke wake waliumwa na kunguni walipokuwa likizoni. Dave anasema: “Tuliaibika sana. Tulijiuliza tutawaambia nini watu wa familia na marafiki tutakapofika nyumbani? Je, wakati wowote wanapojikuna au kupatwa na mwasho wa ngozi wangejiambia ni kwa sababu walitutembelea?” Hata ingawa ni kawaida kuwa na maoni kama hayo, usiache aibu ikuzuie kutafuta msaada. Wizara ya Afya ya Mwili na Akili ya New York City inatoa uhakikisho huu: “Ni vigumu, lakini inawezekana kuwaangamiza kunguni.”

Chunguza uone kama kuna kunguni kisha uchukue hatua za kuwazuia wasijifiche nyumbani kwako
Hata hivyo, usifikiri kwamba ni rahisi kuwamaliza kunguni. Kunguni wakivamia nyumba yako, unaweza kupata msaada kutoka kwa mtaalamu wa kuwadhibiti wadudu wasumbufu. Ingawa kemikali zilizotajwa awali hazitumiwi tena, wataalamu hao hutumia mbinu kadhaa zinazofaa ili kuwaangamiza kunguni. Dini M. Miller, mtaalamu wa wadudu anasema hivi pia: “Kuwadhibiti kunguni kunahitaji ushirikiano mkubwa sana kati ya wakaaji wa nyumba, wamiliki wa nyumba yenyewe, na kampuni ya kuwadhibiti wadudu wasumbufu.” Kwa kufuata mwelekezo wa mtaalamu na kuchukua tahadhari zinazohitajika, unaweza kutimiza sehemu yako na ‘kutowaacha kunguni wakuume’!
 
BAGAH

BAGAH

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2012
Messages
4,533
Points
1,225
BAGAH

BAGAH

JF-Expert Member
Joined Jan 17, 2012
4,533 1,225
toa mashuka na kitanda nje...
fanya usafi wa jumla katika chumba chako...
kunguni ni rafiki wa uchafu...
nahisi hapo kwako ni kama stoo!!

sijui nimetoa dawa?
 
Erickb52

Erickb52

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2010
Messages
18,520
Points
1,250
Erickb52

Erickb52

JF-Expert Member
Joined Oct 31, 2010
18,520 1,250
toa mashuka na kitanda nje...
fanya usafi wa jumla katika chumba chako...
kunguni ni rafiki wa uchafu...
nahisi hapo kwako ni kama stoo!!
sijui nimetoa dawa?
Tena dawa ya kudumu BAGAH
 
Last edited by a moderator:
Erickb52

Erickb52

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2010
Messages
18,520
Points
1,250
Erickb52

Erickb52

JF-Expert Member
Joined Oct 31, 2010
18,520 1,250
Ni wazi kabisa Erickb52 hawa wadudu walishatokomea hasa mijini....Hii si dalili nzuri ..ngoja nisiendelee....
labda yuko bushi
 
Last edited by a moderator:
Dena Amsi

Dena Amsi

R I P
Joined
Aug 17, 2010
Messages
13,120
Points
1,250
Dena Amsi

Dena Amsi

R I P
Joined Aug 17, 2010
13,120 1,250
Dah!!! Kunguni hivi bado wapo??? Aisee hii makitu ya kitambo sana sijaisikia
 
Zuia Sayayi

Zuia Sayayi

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2011
Messages
843
Points
225
Zuia Sayayi

Zuia Sayayi

JF-Expert Member
Joined Mar 28, 2011
843 225
Hv zile dawa za kupulizia zinaweza kutatua tatizo kweli?
 
SIM

SIM

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2011
Messages
1,685
Points
2,000
SIM

SIM

JF-Expert Member
Joined Oct 25, 2011
1,685 2,000
Tafuta dawa inayoitwa DAIZNON niyakuchanganya na maji lakini ukichanganya na mafuta ya taa itakua kali zaidi. kumbuka kunguni unaweza kuwaangamiza wote lakini kukawa kumebakia mayai, jitahidi kuwa msafi
 
Comi

Comi

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2011
Messages
3,335
Points
1,500
Comi

Comi

JF-Expert Member
Joined Oct 2, 2011
3,335 1,500
Du wana jf naombeni mniambie kungunu wanaumwaga ugonjwa gani? Maana mimi nijuavyo tunapulizaga sumu kuwatokomeza sasa leo mnatafuta dawa ya kuwatibu


loh! Mmenikumbusha mbali sana enzi zile unatumwa dukani unasemwambia muuzaji akupe dawa ya mswaki badala ya kusema dawa ya meno
 
Dotworld

Dotworld

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2011
Messages
3,940
Points
1,250
Dotworld

Dotworld

JF-Expert Member
Joined Aug 10, 2011
3,940 1,250
toa mashuka na kitanda nje...
fanya usafi wa jumla katika chumba chako...
kunguni ni rafiki wa uchafu...
nahisi hapo kwako ni kama stoo!!

sijui nimetoa dawa?
Tena dawa ya kudumu BAGAH
.
BAGAH & Erickb52 + Zuia Sayayi

Cleanliness (
Usafi) is not really the cause for bed bug (Kunguni) infestation
. There is no specific cause for its origination.

They move from one place to another through clothing, baggage, old furniture, mattress and other items. Bed bugs infest where there is maximum human occupation. Even the clean hotels have the population of bed bugs. These insects survive on animals and birds as well


These Bed bugs are human parasites. They live on human blood. They have a very good strategy to suck the blood. You never feel pain when it is sucking ,you feel a red blood mark and pain after it leaves off.


The recent studies say that these bedbugs are good carriers of leprosy, oriental sore, Q-fever, and brucellosis(Krueger 2000) .

So one should be careful , detect them and get rid of them in earlier stages. Always approach pest control experts for permanent solution for bed bugs.​
 
BAGAH

BAGAH

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2012
Messages
4,533
Points
1,225
BAGAH

BAGAH

JF-Expert Member
Joined Jan 17, 2012
4,533 1,225
.
BAGAH & Erickb52 + Zuia Sayayi

Cleanliness (
Usafi) is not really the cause for bed bug (Kunguni) infestation
. There is no specific cause for its origination.

They move from one place to another through clothing, baggage, old furniture, mattress and other items. Bed bugs infest where there is maximum human occupation. Even the clean hotels have the population of bed bugs. These insects survive on animals and birds as well


These Bed bugs are human parasites. They live on human blood. They have a very good strategy to suck the blood. You never feel pain when it is sucking ,you feel a red blood mark and pain after it leaves off.


The recent studies say that these bedbugs are good carriers of leprosy, oriental sore, Q-fever, and brucellosis(Krueger 2000) .

So one should be careful , detect them and get rid of them in earlier stages. Always approach pest control experts for permanent solution for bed bugs.​
ni kweli mkuu...hapo nilimuonea huyu jamaa!
 
gambachovu

gambachovu

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2011
Messages
1,865
Points
0
gambachovu

gambachovu

JF-Expert Member
Joined Dec 29, 2011
1,865 0
Kuna wanaochanganya kama si kuchanganyikiwa na Kunguni na Chawa... Nawaona wengi humu ndani..
 
Erotica

Erotica

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2012
Messages
2,514
Points
0
Erotica

Erotica

JF-Expert Member
Joined Apr 24, 2012
2,514 0
Niliona thread kama hii Invisible alirusha. mei bi anajua dawa yake.

ila nina hakika Rungu spray inapiga tu rungu jitihada. haiwezi kuua.
 
sinafungu

sinafungu

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2010
Messages
1,436
Points
2,000
sinafungu

sinafungu

JF-Expert Member
Joined Feb 13, 2010
1,436 2,000
diazon...........hii ni kiboko ila sina hakika kama ck hizi zipo madukani.
 

Forum statistics

Threads 1,335,065
Members 512,185
Posts 32,494,774
Top