Mfahamu Dkt. Zakir Naik

bigmukolo

JF-Expert Member
Mar 6, 2012
486
1,000
(MAZINGE WA INDIA)

Dk Nazik.jpg

Dr. Zakir Naik
Dr. Zakir Naik kwa wale watazamaji wa TV iitwayo Peace Tv inayo endesha vipindi vya dini sio sura ngeni kwa mtaalamu huyu.

Dr. Naik ni mwanaharakati wa dini ya Kiislamu nchini India, aliejizolea umaarufu mkubwa sana kwa yeye kuzunguka nchi mbalimbali za bara la Ulaya na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwasilimisha Wazungu wengi kupitia hoja mbalimbali.

Dr. Naik allah kamjaalia elimu ya dini Masha Allah na elimu ya Mazingira, ni Muhindi aliefanya kazi kubwa mno nchini kwao, kwani India ndio nchi inayoongoza duniani kwa watu wake kuabudia vitu visivyokuwa na mashiko na kuviita ndio Mungu.

Dr. Naik alipoliona hilo akaanzisha mijadala kama ya kina Mazinge kuhusu dini wanazoabudia na miungu wanayoabudia huko nchini India.

Basi hapo ndipo alipoanza kujizolea umaarufu duniani kwa kupambana vikali na wahindi wenzie kwa kuwapa hoja nzito nzito kuhusu Mungu wa kweli ambae ni Allah subhanahu wataala.

Dr. Zakir Naik alianza kazi zake za ulinganiaji kwa kukutana na upinzani mkubwa sana nchini kwake, kwani ilifikia kipindi mpaka kunusurika kuuwawa mara kadhaa na kuitwa gaidi haswa kwa daawa anazozifanya nchini kwao.

Dr. Zakir aliamua kufungua shule haswa ya kutengeneza vijana ambao watakaoifanya kazi hii huko mbeleni, kwani aliamini yeye ni binaadam ipo siku anaweza akaumwa au akaondoka duniani haswaa.

Na katika hilo amefanikiwa Masha Allah kwani ana vijana wa kiume na wakike ambao amewatengeneza kwa ajili ya kuuhami Uislam kwa hoja nzito nzito.

Katika kanuni alizojiwekea katika maisha yake na kupitia kipaji alicho nacho ni kuhakikisha kila sehemu anayo tembelea na kufanya mihadhara yake ni furaha kwake kuhakikisha anawasilimisha watu na kuwaingiza ktk dini tukufu ya kiislamu.

Dr. Zakir Naik amekuwa mwiba mkubwa sana kwa watu wasio Waislamu kwa kuwaonyesha kwa maandiko upotovu walionao katika miungu wanayoabudia.

Kuna baadhi ya nchi kama vile Uingereza alipigwa marufuku ya kuingia nchini humo kwasababu ya kuwasilimisha wazungu wengi kupitia hoja mbalimbali za kwenye vitabu vitakatifu.

Dr. Zakir Naik huanzisha mijadala yenye mashiko popote pale anapokuwepo, iwe kwenye treni, ndege, daladala mpaka mitaani. Ama kweli Dr. amejitoa zaidi kwaajili ya Uislamu.

Dr. Zakir Naik alitoa mchango wake mkubwa sana kipindi Quran inatafsiriwa kwa lugha ya Kihindi, ikiwa Dr, Allah kamjaalia kuzungumza lugha kuanzia tatu yani Kiarabu, Kiingereza na Kihindi na baadhi ya lugha kwa uchache.

Tosheka na historia fupi ya mwanaharakati wa Kiislam.
 

bigmukolo

JF-Expert Member
Mar 6, 2012
486
1,000
Huyu jamaa ni muongo sijwahi pata kuona. Yani kinachompaisha ni kwamba audience yake nyingi ni watu gullible wasioenda kufuatilia anachosema.

Angalia YouTube video Dr Zakir Naik makes 50 mistakes in a five minutes speech.
Ngoja nimsome vizuri
 

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,310
2,000
Huyu jamaa ni muongo sijwahi pata kuona, yani kinachompaisha ni kwamba audience yake nyingi ni watu gullible wasioenda kufuatilia anachosema.

Angalia YouTube video Dr Zakir Naik makes 50 mistakes in a five minutes speech.
Anawaumiza sana mashetani.

 

bhachu

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
5,896
2,000
CP aliomba Debate na Zakir Naik, akaambiwa akitaka Debate aje na watu 20,000 na wafanyie Debate Bangladesh.
 

wakurochi

JF-Expert Member
Dec 4, 2017
1,978
2,000
Huyu ni macho ku mchuzi tu sawa sawa na yule mtaalam wa kutengeneza mafuta ya watu kukanyaga. Wote macho kumchuzi na wanapiga hela ndeeeeefu.
 

Redpanther

JF-Expert Member
Feb 23, 2019
1,126
2,000
DrnZakor Naik mchochezi yule, ndio maana hadi sasa India ilimuondoa nchini mwake anaishi uhamishoni Malaysia


Happy dude
 

Dunamist

JF-Expert Member
Aug 13, 2018
345
1,000
Kuna mwana wakuitwa Pastor T. Mwangi wa hapo 254. Ni genius, natamani one day apate bato na huyu Jamaa kipenzi cha Mtume Muhammad S.A.W
 

Cherenganya

JF-Expert Member
Jan 21, 2018
1,628
2,000
Huyu ni mwamba kweli kweli, mwamba haswaa mwenye kujua kujenga hoja mtaalamu wa comparative religion yaani hoja moja anaizungusha katika vitabu vitatu na anakuja ku conclude katika Qur'an.

Ni mifano ya kina Imam Hanbal, Abu Khanifa, Malik na Shafii katika muktadha wa elimu.
 

Dalmine

JF-Expert Member
Sep 8, 2016
4,199
2,000
Huyu jamaa ni muongo sijwahi pata kuona. ..yani kinachompaisha ni kwamba audience yake nyingi ni watu gullible wasienda kufuatilia anachosema...
Angalia youtube video dr zakir naik makes 50 mistakes in a five minutes speech.

Unachekesha 😁😁 unataka kushindana na Dr zakir wewe! huyo mwache kabisa, huna cha kufanya kavune mpunga tu kaka huu ndio msimu wake
 
Top Bottom