Mfadhili wa CCM ajiunga na CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mfadhili wa CCM ajiunga na CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by NGOWILE, Oct 20, 2012.

 1. N

  NGOWILE JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 454
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  [​IMG]Mzee Shelali akipewa bendera ya CHADEMA[​IMG]Bendera ya CCM ikishushwa nyumbani kwake[​IMG]Watoto wakiichana bendera ya CCM iliyoshushwa[​IMG]Baada ya kukabidhiwa kadi ya CHADEMA Makamanda jana Tulikuwa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma kwenye mkutano wa hadhara wa kumnadi mgombea udiwani kata ya Mpwapwa kamanda Baharia.

  Mkutano huo ulikuwa na umati mkubwa sana watu. Shangwe, hoihoi na nderemo vililipuka pale mfadhili mkubwa wa CCM mkoani Dodoma ndugu Shelali alipoamua kujivua gamba na kujiunga na CHADEMA. Alipopewa nafasi ya kusema chochote kwa umati ule ndugu Shelali alisema amekuwa mfadhili wa CCM tangu mwaka 1983.

  Katika kuthibitisha hilo alikuja na nakala za barua za kuombwa fedha na mzee Malechela pamoja na tuzo nyingi za heshima kutoka CCM. Mzee Shelali alisema ameamua mwenyewe kujiunga na CHADEMA kwani ndicho chama pekee kinachoonyesha nia ya dhati ya kuikomboa Tanzania na kuwaomba wananchi wa Mpwapwa kujiunga na Chadema.

  Katika mkutano huo ngugu Shelali alijitolea kuwanunulia kadi za CHADEMA wananchi wote watakaotaka kujiunga na CHADEMA wilayani mpwapwa. Baada ya mkutano huo wananchi na viongozi wa CHADEMA walielekea nyumbani kwa shelali kushusha bendera ya CCM na kupandisha ya CHADEMA ambapo mzee Shelali alijitolea kuipa CHADEMA ofisi.

  Katika mkutano huo wananchi wa Mpwapwa walichanga zaidi ya sh. laki tano kwa ajili ya kusaidia kampeni.

  Kilichonifurahisha ni kitendo cha wananchi kuingia barabarani licha ya kuzuiwa na polisi waliojaribu kuzima maandamano yao.

  Mkutano huo ulihutubiwa na Benson Kigaila, Diwani Ali Issa Biringi na Kamanda Nicholaus Ngowi.
   

  Attached Files:

 2. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #2
  Oct 20, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,132
  Trophy Points: 280
  big Up CHADEMA
   
 3. Miwatamu

  Miwatamu JF-Expert Member

  #3
  Oct 20, 2012
  Joined: Oct 2, 2012
  Messages: 1,453
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 133
  Hao ndio wanatakiwa kuimalisha uhai wa chama, si wale wanaokuja kwa kutaka kupewa vyeo. Big up DOM kwani mmelala sana wakati mkoa huo ndio kitovu cha SIASA.
   
 4. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #4
  Oct 20, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,036
  Likes Received: 3,067
  Trophy Points: 280
  chama kilizaliwa kimekua na sasa kinawajibika kwa ajiri ya jamii nzima ...al the best!
   
 5. MR. ABLE

  MR. ABLE JF-Expert Member

  #5
  Oct 20, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,476
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Safi sana nimefarijika sana moyoni kusikia hivyo. M4C forever
   
 6. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #6
  Oct 20, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kimezeeka, kimeota magamba, kinang'atuka, hongera ssm kwa uamuzi wa busara wa kung'atuka
   
 7. Goodluck Mshana

  Goodluck Mshana JF-Expert Member

  #7
  Oct 20, 2012
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 1,167
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Hakuna kurudi nyuma makamanda...ningefuahi zaidi kama Mh. Sabodo angefanya hivi na yeye kwani keshaonesha kuchoshwa na magamba..M4C daima.
   
 8. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #8
  Oct 20, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 1,115
  Trophy Points: 280
  madhara ya mabomu ya machozi hayo.
   
 9. Jakubumba

  Jakubumba JF-Expert Member

  #9
  Oct 20, 2012
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 1,627
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Du huyu mzee ana pesa, amekifadhili chama tangu mwaka wangu wa kuzaliwa? Sasa ataendelea kukifadhili na chadema? Tunamkaribisha kwa mikono miwili.
   
 10. G

  Getwa Anicet Ally Member

  #10
  Oct 20, 2012
  Joined: Jan 13, 2012
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Big up benson! Aluta continua!
   
 11. Frank King

  Frank King JF-Expert Member

  #11
  Oct 20, 2012
  Joined: Oct 7, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 339
  Trophy Points: 180
  ishia hapo hapo acha kejeli zako!!
   
 12. l

  lerai Member

  #12
  Oct 20, 2012
  Joined: Oct 6, 2012
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  safi sana makamanda mna onesha ni kwa jinsi gani mna ishambulia dodoma na ku teka wilaya za dodoma safi wana mpwapwa kwani walisha zoea ku ifanya wilaya hio kuwa pango la wala rushwa na sehemu ya wenyewe ku tajilika safi mzee wangu shelali kwa kuwa onesha njia wezio na kuwa toa wenzio uwoga wame baki waoga wachache apo mpwapwa ,!,
   
 13. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #13
  Oct 20, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Love you CHADEMA
   
 14. washa

  washa JF-Expert Member

  #14
  Oct 20, 2012
  Joined: Oct 8, 2007
  Messages: 476
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Kamanda tunaomba utupie picha!..Pipoz.....................hadi kieleweke
   
 15. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #15
  Oct 20, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Hicho kijamaa kimechemka big tyme kujiunga na chama mfu soon!!!
   
 16. M

  Mea2 Member

  #16
  Oct 20, 2012
  Joined: Sep 5, 2012
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  safi sana makamanda
   
 17. M

  Mjenda Chilo JF-Expert Member

  #17
  Oct 20, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 1,425
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Chadema kongwa na mpwapwa mkiweza nitaamini maana kwa kumbukumbu zangu za karibu inawezekana Ccm ndo chama maarufu ambacho ukiacha wabunge JK alipata over 90% ya kura zote. Ngoja tuone
   
 18. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #18
  Oct 20, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,420
  Likes Received: 259
  Trophy Points: 180
  Ccm chama kikuu na makini by 2016 and forever!
  ANGALIZO kwa wanachadema hawa makuhadi ,mafisadi na wezi wa ccm wakijipenyeza na kujiunga chadema kwa jinsi tunavyowashabikia itakuweje?
   
 19. N

  Ningu Member

  #19
  Oct 20, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 75
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  nimekubali....peoplezzzzzzz!
   
 20. M

  Masterproud JF-Expert Member

  #20
  Oct 20, 2012
  Joined: Sep 14, 2012
  Messages: 442
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Ni kweli jana pia nilikuwepo Mpwapwa Mkutano ulifanyika ktk uwanja wa mashujaa na ulifana sn. Pia CCM walikuwa na mkutano wao Eneo wanaita Kikombo na ulikuwa na watu wachache sn.
   
Loading...