Mfadhili wa CCM ajiunga na CHADEMA

mzee shelali mmiliki wa safari master bus service toka enzi za mwalimu (rip) baba wa taifa , mfadhili wa hawa magamba toke enzi ya mh said mtaki(rip) , na kabla ya hapo , hakuna mwana ccm wa mpwapwa ambaye atafurahi kupoteza mtu kama shelali , labda aulizwe mh lubeleje anajua umuhimu wa shelali kwa mustakabali wa siasa za mpwapwa , wazee maarufu wa mpwapwa wengi hivi sasa, wameshatangulia mbele ya haki, sasa inapo tokea mzee kama shelali kujivua gamba naona mabadiliko ya kweli yanakuja mpwapwa,

nawapongeza chadema kwa kumleta kamanda baharia , aje kuchukua kiti cha kwanza cha mabadilko ndani ya mji wa mpwapwa, magamba wamekosa mtu hadi wamlete yule mmiliki wa iliyo kuwa hazina stars football club iliyo kuwa na wachezaji wezi wote na wakabaji wa mpwapwa , na elimu yake isiyo na cheti ya msingi , mgombea wa magamba ndio atakuwa mgombea udiwani wa 1 kuchakachua cheti cha std 7, shukrani ziende kwa kaka ake (rip) aliye kuwa dereva wa ujenzi kwa kumrudisha mjini baada ya ile issue ya kampuni ya ujenzi wa barabara moro to dom , pale dumila,

shime wana mpwapwa, kikombo, nghambo, igovu, mwanakianga,ilolo,hazina ,vinghawe,kota, 1 way, majengo,mazae,kikombo road, mji mpya, fanyeni mabadiliko elimu ni muhimu kwa maendeleo ya mji wenu

n;b, hakimu wa mahakama ya mwanzo alikalia kiti cha ubunge alichowaletea ni nn au ndio ule mtaa pale manaseh walipo jenga wabunge woote mlio wachagua,ingawa kumbu kumbu zangu zinaonyesha eneo lile nila wazi na ushahidi kulikuwa na uwanja wa mpira ,kamanda baharia ukipata anza na hawa wavamizi wa eneo la wazi
 
Hizo ni propaganda za kitoto. Huyu wanayemwita mfadhili wa ccm ni kituko kwa wanaofahamu ukweli. Mbona mkutano wanjaa watoto na vivulana kama kawa
 
Nimeguswa sana na tukuio hili ahsante sana Kemcho Bay naona umeamua kujikomboa nakusihi uwahamasishe na ma kemcho wengine pia!!!
attachment.php
Mzee Shelali akipewa bendera ya CHADEMA
attachment.php
Bendera ya CCM ikishushwa nyumbani kwake
attachment.php
Watoto wakiichana bendera ya CCM iliyoshushwa
attachment.php
Baada ya kukabidhiwa kadi ya CHADEMA Makamanda jana Tulikuwa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma kwenye mkutano wa hadhara wa kumnadi mgombea udiwani kata ya Mpwapwa kamanda Baharia.

Mkutano huo ulikuwa na umati mkubwa sana watu. Shangwe, hoihoi na nderemo vililipuka pale mfadhili mkubwa wa CCM mkoani Dodoma ndugu Shelali alipoamua kujivua gamba na kujiunga na CHADEMA. Alipopewa nafasi ya kusema chochote kwa umati ule ndugu Shelali alisema amekuwa mfadhili wa CCM tangu mwaka 1983.

Katika kuthibitisha hilo alikuja na nakala za barua za kuombwa fedha na mzee Malechela pamoja na tuzo nyingi za heshima kutoka CCM. Mzee Shelali alisema ameamua mwenyewe kujiunga na CHADEMA kwani ndicho chama pekee kinachoonyesha nia ya dhati ya kuikomboa Tanzania na kuwaomba wananchi wa Mpwapwa kujiunga na Chadema.

Katika mkutano huo ngugu Shelali alijitolea kuwanunulia kadi za CHADEMA wananchi wote watakaotaka kujiunga na CHADEMA wilayani mpwapwa. Baada ya mkutano huo wananchi na viongozi wa CHADEMA walielekea nyumbani kwa shelali kushusha bendera ya CCM na kupandisha ya CHADEMA ambapo mzee Shelali alijitolea kuipa CHADEMA ofisi.

Katika mkutano huo wananchi wa Mpwapwa walichanga zaidi ya sh. laki tano kwa ajili ya kusaidia kampeni.

Kilichonifurahisha ni kitendo cha wananchi kuingia barabarani licha ya kuzuiwa na polisi waliojaribu kuzima maandamano yao.

Mkutano huo ulihutubiwa na Benson Kigaila, Diwani Ali Issa Biringi na Kamanda Nicholaus Ngowi.[/QUOTE]
 
Kuhama chama ni jambo jema kwa kuwa hayo ni mapenzi na imani ya mtu mwenyewe, kitendo cha kuchana bendera siyo cha kiungwana hata kidogo na hilo ni doa tosha kwa muhusika. Leo huyo bw. amechana bendera ya CCM, siku anahamia chama kingine atachana ya CHADEMA, JE sina uhakika hao ambao leo tunaoshabikia kitendo cha kuchoma bendera siku ikichomwa ya kwetu tutaweka maneno gani. Yapo yanayohitaji ushabiki na yapo ambayo ni busara na utu zaidi.
 
Hizo ni propaganda za kitoto. Huyu wanayemwita mfadhili wa ccm ni kituko kwa wanaofahamu ukweli. Mbona mkutano wanjaa watoto na vivulana kama kawa

shelali kituko inaonekana humjui ww nikusaidie kidogo ukivuka daraja baada ya bank (nmb) upande wako wakulia ndio nyumbani kwa shelali hicho kituko unachosema ww ni nn labda tujuze tukusidie
 
Huyu ndio mwanachama wa ukweli sio wale wanaoingia then wanataka kuwa viongozi kama Samuel Sitta ati ee bana eeee kama nikijiunga na Chadema chama cha ukweli si nitagombea urais kaambiwa mwee Ke..ng..e mkubwa kama ni hivyo baki huko huko kwa wenzako Magamba yr not qualify hapa.
Karibu Chadema kuwa mwanachama mtiifu then uongozi unakuja wenyewe tu kutoka kwa wananchi kwani chama chetu ni cha wananchi thus why we use to say Peoples Power
 
Back
Top Bottom