Mfadhili wa CCM ajiunga na CHADEMA

Kila kitu/jambo lina mwisho 2015 ni gharika kwa chama cha magamba kwani siku zinavyozidi kusonga mbele ndivyo watanzania wanavyozidi kuelimika na kugundua uovu na dhuluma ya magamba
 
Katika mkutano huo ngugu Shelali alijitolea kuwanunulia kadi za CHADEMA wananchi wote watakaotaka kujiunga na CHADEMA wilayani mpwapwa.

Mtu anatakiwa ajiunge na chama kwa mapenzi yake mwenyewe na sio kununuliwa card na mtu! Hili sio sahihi.
 
Nimefungua huu uzi kwa kasi ya ajabu kumfahamu huyo mfadhili wa CCM nilidhani Sabodo, kumbe jamaa wa Mpwapwa.

Mkuu kule Moshi mpakani na Arusha karibu na Karatu upande wa Kaskazini kuna kimtaa kinaitwa Mpwapwa ndiko anakotokea huyo mfadhili. Ha ha ha ha ha! Pole kaka.
 
huyo ajipange tu, tutafunga tubiashara twake sasa hivi, ngoja TRA waende kwanza kumfanyia tathmini ya kodi alizokuwa anakwepa
awaulize kina kishimba wa mwanza, mmliki wa kwanza wa rock beach, na kina imalaseko
tunakukaribisha katika umaskini
 
Du huyu mzee ana pesa, amekifadhili chama tangu mwaka wangu wa kuzaliwa? Sasa ataendelea kukifadhili na chadema? Tunamkaribisha kwa mikono miwili.

Lakini tuangalie; kwani ilishatabiriwa kuwa moja ya mbinu waliyo nayo CCM ni kuweka vibraka wao ndani ya chama CDM, kisha watagombea uongozi, kitakachofuata ni kuleta mgawanyiko ndani ya CDM.

Si busara kupokea Magamba bila ya kuyachunguza.

MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
Makamanda jana Tulikuwa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma kwenye mkutano wa hadhara wa kumnadi mgombea udiwani kata ya Mpwapwa kamanda Baharia.

Mkutano huo ulikuwa na umati mkubwa sana watu. Shangwe, hoihoi na nderemo vililipuka pale mfadhili mkubwa wa CCM mkoani Dodoma ndugu Shelali alipoamua kujivua gamba na kujiunga na CHADEMA. Alipopewa nafasi ya kusema chochote kwa umati ule ndugu Shelali alisema amekuwa mfadhili wa CCM tangu mwaka 1983.

Katika kuthibitisha hilo alikuja na nakala za barua za kuombwa fedha na mzee Malechela pamoja na tuzo nyingi za heshima kutoka CCM. Mzee Shelali alisema ameamua mwenyewe kujiunga na CHADEMA kwani ndicho chama pekee kinachoonyesha nia ya dhati ya kuikomboa Tanzania na kuwaomba wananchi wa Mpwapwa kujiunga na Chadema.

Katika mkutano huo ngugu Shelali alijitolea kuwanunulia kadi za CHADEMA wananchi wote watakaotaka kujiunga na CHADEMA wilayani mpwapwa. Baada ya mkutano huo wananchi na viongozi wa CHADEMA walielekea nyumbani kwa shelali kushusha bendera ya CCM na kupandisha ya CHADEMA ambapo mzee Shelali alijitolea kuipa CHADEMA ofisi.

Katika mkutano huo wananchi wa Mpwapwa walichanga zaidi ya sh. laki tano kwa ajili ya kusaidia kampeni.

Kilichonifurahisha ni kitendo cha wananchi kuingia barabarani licha ya kuzuiwa na polisi waliojaribu kuzima maandamano yao.

Mkutano huo ulihutubiwa na Benson Kigaila, Diwani Ali Issa Biringi na Kamanda Nicholaus Ngowi.

Was there any traditional Music Mkuu?

Roho yangu inaipenda sana Dodoma. Naipenda Saaaana Dodoma. Na ukipasua moyo wangu ujue sababu ni nini hasa mapenzi haya, utakuta sababu ni zile zeze, marimba, ngoma na sauti nzuri za wale mabinti, watanzania wenzetu waishio Dodoma! Such a gifted tribe! Asante kwa taarifa yako nzuri Mkuu.
 
huyo ajipange tu, tutafunga tubiashara twake sasa hivi, ngoja TRA waende kwanza kumfanyia tathmini ya kodi alizokuwa anakwepa
awaulize kina kishimba wa mwanza, mmliki wa kwanza wa rock beach, na kina imalaseko
tunakukaribisha katika umaskini
Yale mambo ya vitisho kuwa ukiweka bendera ya shina yenye rangi ya kijani, ndiyo biashara yako itakunyookea, hizo propaganda zishapitwa na wakati, alianza Sabodo kufungua njia, na wengine wengi wanafuata nyayo, na biashara zao zinazidi kusonga mbele. M4C in full swing, magamba wanazidi kusambaratika!!
 
Jamaa kakaa CCM kabla ya mwaka 1983 na mwaka tajwa akaanza kuwa mfadhili wa ziada wa CCM mpaka 2012. Leo Chadema wao wanasherehekea kuwa wamelamba dume,Kimahesabu 2012 - 1983 = 29 Miaka. Tuchukulie kwamba ameanza ufadhili CCM akiwa na umri wa miaka 40 akili ikiwa angalau lakini angalia walipotufikisha na CCM akiwa mfadhili wake. Leo ana umri zaidi ya 69 anaonekana wa maana cdm na bila kuchelewa kaanza na kauli ya kadi bure ambayo inapingwa na wanacdm. yale yale kasoro siku tu na umri
 
View attachment 68781Mzee Shelali akipewa bendera ya CHADEMAView attachment 68783Bendera ya CCM ikishushwa nyumbani kwakeView attachment 68784Watoto wakiichana bendera ya CCM iliyoshushwaView attachment 68779Baada ya kukabidhiwa kadi ya CHADEMA Makamanda jana Tulikuwa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma kwenye mkutano wa hadhara wa kumnadi mgombea udiwani kata ya Mpwapwa kamanda Baharia.

Mkutano huo ulikuwa na umati mkubwa sana watu. Shangwe, hoihoi na nderemo vililipuka pale mfadhili mkubwa wa CCM mkoani Dodoma ndugu Shelali alipoamua kujivua gamba na kujiunga na CHADEMA. Alipopewa nafasi ya kusema chochote kwa umati ule ndugu Shelali alisema amekuwa mfadhili wa CCM tangu mwaka 1983.

Katika kuthibitisha hilo alikuja na nakala za barua za kuombwa fedha na mzee Malechela pamoja na tuzo nyingi za heshima kutoka CCM. Mzee Shelali alisema ameamua mwenyewe kujiunga na CHADEMA kwani ndicho chama pekee kinachoonyesha nia ya dhati ya kuikomboa Tanzania na kuwaomba wananchi wa Mpwapwa kujiunga na Chadema.

Katika mkutano huo ngugu Shelali alijitolea kuwanunulia kadi za CHADEMA wananchi wote watakaotaka kujiunga na CHADEMA wilayani mpwapwa. Baada ya mkutano huo wananchi na viongozi wa CHADEMA walielekea nyumbani kwa shelali kushusha bendera ya CCM na kupandisha ya CHADEMA ambapo mzee Shelali alijitolea kuipa CHADEMA ofisi.

Katika mkutano huo wananchi wa Mpwapwa walichanga zaidi ya sh. laki tano kwa ajili ya kusaidia kampeni.

Kilichonifurahisha ni kitendo cha wananchi kuingia barabarani licha ya kuzuiwa na polisi waliojaribu kuzima maandamano yao.

Mkutano huo ulihutubiwa na Benson Kigaila, Diwani Ali Issa Biringi na Kamanda Nicholaus Ngowi.

Hii ni habari njema. Ila tutarajie TRA na polisi kuanza kumuandama mzee Shelali
 
Huyu mzee akapimwe akili zake anajiunga chadema.Naona anataka afe na presha kwanza inaonekana halipi kodi huyu TRA fanyeni kazi yenu.
 
Huyu mzee akapimwe akili zake anajiunga chadema.Naona anataka afe na presha kwanza inaonekana halipi kodi huyu TRA fanyeni kazi yenu.
Kumbe ukiwa mwanachama wa CCM unaruhusiwa kukwepa kodi? Mkuu usipende kuropoka kama Gaidi Ponda na mwenzake Faridi
 
Goodwork cdm isipokuwa hii ya kuchana bendera yaweza kuwa kosa na hasa ukizingatia hao ni watoto huenda wakaingia kwenye misukosuko isiyo ya lazima
 
Back
Top Bottom