Meya wa Kinondoni: Wafanyabiashara 45,000 wamefunga biashara zao kwa muda wa miaka 5 iliyopita

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
118,177
219,321
Akichangia hoja kwenye sakata la kuwapanga wamachinga, Meya Songoro Mnyonge amedai kwamba wafanyabiashara elfu 45 wa Manispaa hiyo waliacha maduka yao na kugeuka wamachinga katika muda mfupi wa miaka mitano tu, hakueleza sababu hasa ya jambo hilo kama ni kufa kwa uchumi wa nchi au kuenea kwa wamachinga kila mahali.

Amedai mpaka sasa zaidi ya maduka 150 hufungwa kila mwezi kutokana na ugumu wa biashara.

Chanzo : Global Publishers

Mytake: Nchi hii ilipofikia kiuchumi inahitaji kufunga na kuomba.
 
Serikali itakuwa na hii namba lakini haiwezi kuiweka hadharani kwa aibu ya jinsi walivyoangusha uchumi kwa sera zao MUFILISI na uporaji.

Hio ni Kinondoni. Kwa haraka haraka, Tanzania nzima idadi ya waliofunga biashara au kufilisiwa inafika ngapi kwa kipindi cha miaka 5 ndugu mwandishi wa uzi?

CCM walikua wanajifanya hamnazo mwanzo na kukana malalamiko ya watu kufunga biashara. Sasa akili zimeanza kurudi.
 
Meya Songoro mwanaCCM kindakindaki hatimaye naye aweka hadharani hali ya kiuchumi ilivyo kwa miaka 6 yaani 2015-2021 ya kuanzia utawala wa hayati (the late) mwendazake (revered)John Pombe Joseph Magufuli RIP huku CCM wanadai kazi hiyo iendelee.
 
Kuna kada mmoja kijana,anasema serikali ya awamu ya tano imetengeneza mazingira rafiki kwa wafanyabiashara,awamu ya sita ndio itafaidika zaidi kiuchumi,kwa kauli iyo lakini wapi kuna watu watasema huyo meya ni upinzani
 
Back
Top Bottom