Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,498
- 9,279
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge amesema kwa miaka mitano au sita iliyopita kumekuwa na wimbi la wafanyabiashara wengi ambao wanafunga biashara rasmi na kuhamia umachinga.
“Kinondoni huwa tunapokea taarifa ya biashara zinazofungwa ambapo kila mwezi ni biashara 150 zinafungwa na hii ni kwa zaidi ya miaka mitano iliyopita.
“Kwa hesabu za Kinondoni, zaidi ya wafanyabiashara rasmi 9,000 wamekuja kutoa tamko la kufunga biashara ili wasitambulike kwenye mfumo.
“Wanapofunga biashara wanapeleka tamko Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Lakini tumebaini wafanyabiasharta hawa wanakwenda kuwa wamachinga.
“Nimeuliza mameya wenzangu hali ni hiyohiyo. Tulikuwa tunachukua takwimu za mkoa mzima na kubaini mpaka sasa ni zaidi ya wafanyabiashara 45,000 waliokuwa kwenye mfumo rasmi wamebadilika na kuwa wamachinga,” amesema.
Aidha, aliwaonya viongozi wenzake ambao wanadaiwa kuingia kwenye biashara ya kuleta wamachinga kutoka mikoani na kuwaleta jijini Dar es Salaam.