Meya wa Dar akataa nyumba ya Serikali, Kuendelea kuishi kwenye makazi yake Vijibweni

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,906
2,885
Meya wa jiji mashuhuri hapa Tanzania yaani Dar mheshimiwa Charles Mwita tokea kambi ya UKAWA amegoma kuhamia kwenye nyumba ya serikali ambayo ni maalumu kwaajili ya meya na kudai kuwa ataendelea kubakia kwenye makazi yake Vijibweni huko Kigamboni

Ingawa haijaelezwa sababu za kuikataa nyumba hiyo. Je, hatua hiyo yaweza kuwa na tija gani kwa taifa?

Chanzo: Mtanzania
 
Hamna tija yeyote kwa taifa ila ina lengo baya ya kuharibu mali ya umma kwani nyumba isipotumika huchakaa na kuharibika kabisa.

Ningemuona mjanja kama nyumba isingekuwepo na wakamwambia wamjengee akatae lakini kwa vile ipo na kaikataa ni mharibifu.
 
meya wa jiji mashuhuri hapa tanzania yaani dar mheshmiwa charles mwita tokea kambi ya ukawa amegoma kuhamia kwenye nyumba ya serikali ambayo ni maalum kwaajili ya meya na kudai kua ataendelea kubakia kwenye makazi yake vijibweni huko kigamboni. ingawa haijaelezwa sababu za kuikataa nyumba hiyo je hatua hiyo yaweza kua na tija gani kwa taifa? source gazeti mtanzania
ni uamuzi wa kishujaa uliojaa tahadhari zenye maono ndani yake , ccm si wa kuaminika kabisa , hongera Mstahiki Meya .
 
Hamna tija yeyote kwa taifa ila ina lengo baya ya kuharibu mali ya umma kwani nyumba isipotumika huchakaa na kuharibika kabisa.

Ningemuona mjanja kama nyumba isingekuwepo na wakamwambia wamjengee akatae lakini kwa vile ipo na kaikataa ni mharibifu.
kwa kweli kafanya jambo la maana sana, aibadili kuwa clinic ya wajawazito na watoto. Angekuwa maalim saif angehamia holiday inn akisubiri ukarabati wa nyumba ukamilike.
 
Hamna tija yeyote kwa taifa ila ina lengo baya ya kuharibu mali ya umma kwani nyumba isipotumika huchakaa na kuharibika kabisa.

Ningemuona mjanja kama nyumba isingekuwepo na wakamwambia wamjengee akatae lakini kwa vile ipo na kaikataa ni mharibifu.
ushauri wangu hiyo nyumba wapewe walimu wa Makonda wenye shida ya mahali pa kulala .
 
Meya wa jiji mashuhuri hapa tanzania yaani Dar mheshmiwa Charles Mwita tokea kambi ya UKAWA amegoma kuhamia kwenye nyumba ya serikali ambayo ni maalumu kwaajili ya meya na kudai kua ataendelea kubakia kwenye makazi yake Vijibweni huko Kigamboni

Ingawa haijaelezwa sababu za kuikataa nyumba hiyo je hatua hiyo yaweza kua na tija gani kwa taifa?

Chanzo: Mtanzania
Hana jipya huyo
 
Mjanja anataka alipwe posho kwa kuwa hakai nyumba ya serikali.Hizo pesa za posho ya nyumba angekaa nyumba ya serikali zisingelipwa zingeenda kwenye matumizi mengine kama kununua madawati nk
 
Hamna tija yeyote kwa taifa ila ina lengo baya ya kuharibu mali ya umma kwani nyumba isipotumika huchakaa na kuharibika kabisa.

Ningemuona mjanja kama nyumba isingekuwepo na wakamwambia wamjengee akatae lakini kwa vile ipo na kaikataa ni mharibifu.
Kwa hiyo bora ichakae ya kwake aliyojenga kwa gharama zake eti eeh!!
 
Mjanja anataka alipwe posho kwa kuwa hakai nyumba ya serikali.Hizo pesa za posho ya nyumba angekaa nyumba ya serikali zisingelipwa zingeenda kwenye matumizi mengine kama kununua madawati nk
na gari akatae ni la kifahari mno.
 
ni uamuzi wa kishujaa uliojaa tahadhari zenye maono ndani yake , ccm si wa kuaminika kabisa , hongera Mstahiki Meya .
Ushujaa wapi mbwembwe tu. Haina tija yoyote kwetu labda wangekuwa wanataka kujenga mpya sawa lakini nyumba imeshajengwa. Sio kila kitu kushadadia tu nyingine Sanaa tu hizo
 
Back
Top Bottom