Meya wa CHADEMA: Una deni kubwa Dar la kujenga mnara wetu wa saa

2kimo

JF-Expert Member
Jan 23, 2014
2,029
2,072
Mstahiki meya wa jiji la Dar, tunakuomba ulipe deni ambalo wananchi wa jiji hili tunadai halmashauri zetu!

Ni juu ya mnara wa saa, hii ndio symbol kuu ya kutawazwa rasmi mji huu kuwa jiji miaka 55 iliyopita!

Kwa maana yeyote ile, mnara Mkuu wa utambulisho wa jiji ambao unapaswa uwe chini yako mstahiki meya huu mnara wa saa, ule wa picha ya askari unaweza kuwa wa makumbusho ya taifa!

Hali ni mbaya ktk hiki kitovu cha mji ambapo ndio kitovu cha umbali kwa njia ya barabara kuelekea popote! Yaani ukisema Bunju ni 40km toka city centre, hii ndio reference point,hata tunaposema morogoro ni km 180 sijui point of reference ndio hapa, kama ule mnara wa saa wa Arusha!

Kwa minajiri hiyo huu mnara ni muhimu kwa kumbukumbu lakini pia ndio kitovu cha jiji!
Hali yake ni mbaya na hauna hadhi yeyote! Meya wa CCM aliyeondoka alitawanya mabati mjini ya makatuni mbalimbali lakini hakugusa kabisa mnara huu!

Please meya mpya wa UKAWA, hebu chukua credit kwa kuurejeshea hadhi mnara wetu, uwe wa kisasa zaidi labda regime yako nayo tutaikumbuka milele!
 
Kati ya madawati na mnara kipi kianze?
Kimoja sio substitute ya mwenzake!
Vyote vinapaswa viwepo!
Kwani si tulijenga daraja, uwanja wa taifa, BRT na vyote hivyo vilikuta shida za madawati! Au hili tatizo la madawati ni la mwaka 2016?
Mnara wa saa ni kitu muhimu sana kwa jiji la Dar!
Jiji linauwezo wa kuzalisha vya kutosha, Dar tunapesa kuliko majiji yote nchini yakiwa combined, hiyo lazima iwe reflected ktk symbols za jiji! Kama Paris, New York, London, Nairobi etc, na ni lazima ujue hapo pesa hakuombwa Magu tumemuomba mstahiki meya wetu!
Hata ule mnara uliopo sasa kimeandikwa kuwa umetengenezwa na watu wa DSM kama kumbukumbu ya kufanywa jiji/mji Mkuu wa nchi! Mnara ni prioirty ktk jiji na inapaswa uingie ktk budget ya jiji au kama bado basiniwe reallocated kwa ajili hiyo!
 
Back
Top Bottom