Meya mbaroni kwa tuhuma za mauaji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Meya mbaroni kwa tuhuma za mauaji

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by MziziMkavu, May 22, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  [​IMG] Ahusishwa na mauaji ya kada wa CCM
  [​IMG] Akamatwa baada ya kushuka kwenye ndege  [​IMG]
  Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Leonard Bandiho Bihondo (64).  Jeshi la Polisi limemtia mbaroni Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Leonard Bandiho Bihondo (64), kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Kata Isamilo, jijini Mwanza, Bahati Stephano (46).
  Bihondo ambaye ni Diwani wa Kata ya Isamilo kupitia CCM ni mtuhumiwa wa nne kukamatwa tangu marehemu Bahati alipofariki dunia kwa kuchomwa kisu kifuani Mei 14, mwaka huu saa 6: 30 mchana.
  Taarifa za kukamatwa kwa Meya huyo zilitolewa jana na Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Simon Sirro, wakati akizungumza na waandishi wa habari.
  “Kama nilivyowaeleza awali siku zilizopita, ni kwamba upelelezi wa mauaji ya Katibu wa CCM Kata ya Isamilo unaendelea ambapo Jeshi la Polisi tumemkamata Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Leonard Bandiho Bihondo (64),” alisema Kamanda Sirro.
  Kamanda Sirro alisema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa katika uwanja wa ndege wa Mwanza akireja jijini humu kutoka Dar es Salaam.
  Kamanda Sirro alisema kuwa Meya Bihondo alikamatwa kutokana na kutajwa tajwa na watuhumiwa watatu ambao tayari wamekwisha kukamatwa kuhusiana na tukio hilo.
  Kamanda Sirro alifafanua kwamba Meya Bihondo alikamatwa muda mfupi baada ya kushuka kwenye ndege, akitokea jijini Dar es Salaam.
  “Tukithibisha kwamba ama amehusika au amekula njama, itabidi tumfikishe mahakamani,” alisema Kamanda Sirro.
  Tukio la mauaji ya Bahati lilizua mjadala mkubwa huku mauaji hayo yakihusishwa na masuala ya kisiasa.
  Inadaiwa kuwa hivi sasa makundi yanayohasimiana ndani ya CCM yanachuana kwa ajili ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 31, mwaka huu.
  Waliokwisha kukamatwa ni pamoja na Jumanne Oscar (30) ambaye anatuhumiwa kumchoma Bahati kwa kisu sehemu za tumboni na kwenye titi na kusababisha kifo chake. Oscar alikamatwa muda mfupi baada ya mauaji hayo.
  Watuhumiwa wengine waliokamatwa kabla ya kukamatwa kwa Bihondo jana, ni Baltazar Shushi ambaye mwaka 2009 aligombea uenyekiti wa mtaa wa Isamilo Kaskazini B kwa tiketi ya CCM na kubwagwa na mgombea wa Chadema.
  Kada mwingine aliyekamatwa kwa kuhusishwa na mauaji hayo ni pamoja na Abdul Ausi aliyewahi kuwa Katibu Mwenezi wa CCM Kata ya Isamilo kabla ya uchaguzi wa 2007.
  Tukio hilo limesababisha idadi ya makada wawili CCM kufariki dunia jijini hapa, kwa kuchomwa visu katika mazingira ambayo yanaibua hisia kuwa ni chuki za kisiasa.
  Tukio la kwanza lilitokea Mei 5, mwaka huu Katibu wa CCM wa Tawi la Isesa katika Kata ya Sangabuye wilayani Ilemela, Lazaro William, ambaye alichomwa kisu na kufariki dunia wakati akikimbizwa hospitali ya Rufaa Bugando kwa matibabu.
  Jiji la Mwanza limekuwa na historia ya mashambulizi ya kudhuriana kutokana na sababu za kisiasa, mojawapo ya matukio mabaya kuwahi kutokea jijini humo ni lile la kumwagiwa tindikali kwa aliyekuwa Mbunge wa Mwanza Mjini (CCM), Said Shomari, akiwa ofisini miaka ya tisini mwishoni.
  Mbunge huyo alijeruhiwa vibaya shingoni kwa kuunguzwa kwa tindikali iliyokuwa imenuiwa kumwagiwa usoni mwake.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #2
  May 22, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Heee siasa zina mambo! Mpaka na kutoana roho kabisa. Hapo tutapofika kwenye siku ya mahesabu ya mwisho kwa kweli Mwenyezi Mungu atakuwa na kazi kubwa. Kuhukumu kesi za mauaji ya ujambazi, siasa, tamaa, wazinifu na wengi wengine!
   
Loading...