MEYA Jerry Silaa asema SIASA za UJAMAA na KUJITEGEMEA ni MBAYA, NYERERE alituharibu...

- Wale wale Mwalimu Compromise, mko radhi kuandika anything kumtetea kwamba alikuwa Malaika wa Mungu, huyu jamaa amendika mavitabu weeee!! lakini anaishia kujificha majuu njoo bongo utekeleze hizi empty theory zenu uone kama inawezekana, maneno mengi ya kiingereza hizi theory zenu ziliwahi kufanikiwa nchi gani Duniani? Cuba? ha1 ha!

SALUTE TO THE MAYOR JERYY SILAA!!

LE MUTUZ

Nina uhakika unapotembelea miradi ya Jumuiya wa wazazi unakutana na mambo mengi aliyoayaasisi Mwalimu; pamoja na chuki zenu binafsi dhidi ya Mwalimu ukweli utabaki kama ulivyo; hakuwahi kujiita nabii wala kujiona mkamilifu na alikiri hilo wazi; na hakuwahi kuwa sultan wala mfalme kuna watu walifanya naye kazi wakiwa kama makamu wa Raisi na makamu wenyeviti upo uwezekano mkubwa failures za Mwalimu ni kutokana na kufanya kazi na watu wasio na uwezo sasa inakuwaje lawama hizi mnakimbilia kumtupia mtu mmoja na kuwaacha wahusika wengine? Na suala kama ni kweli kama mnavyodai eti aliacha misingi mibovu kwanini msijenge misingi mipya? Mwalimu hayupo madarakani karibu miaka 30; kama hoja ya misingi mibovu Brazil iliwachukua karibu miaka 20 kusimamisha misingi mipya matokeo leo Brazil wamepiga hatua kubwa sana kiuchumi; sasa je nyie mnasubiri Mwalimu afufuke aseme misingi basi ili muachane nayo? Inaeleweka wazi hizi ni siasa za maji taka nakumbuka wengi wenu humu wakati mh. Jakaya anaingia kwenye kiny'ang'nyiro cha uraisi mlikuwa mnashinda kwenye mitandao kumtukana matusi ya nguoni ambayo hata kuyarudia kuyasema ni aibu lakini leo hii mmekuwa vinara wa kutafuta kupiga picha naye; haters hata mkikesha usiku na mchana historia ya Mwalimu hamuwezi kuibadili itaendelea kuwepo tu kweli yapo mapungufu aliyafanya na yapo mema mengi sana aliyafanya kama kiongozi na ndio sababu watanzania tunaendelea kumuenzi!
 
Ng'wamapalala
Mwalimu alikiri wazi makosa yake kama kiongozi wala hakuona vibaya kulisema hilo; unataka ktupa lawama ambazo hazina msingi ni mara ngapi wakati Mwalimu IMF na WB ziligomea kutoa mikopo kwa Tanzania? Mara nyingi aliweka maslahi ya taifa hili mbele hizi rasimali mnazodai zinaibiwa hivi sasa zilikuwepo wakati Mwalimu alijua kulinda ili zinufaishe watanzania hakuangalia maslahi yake binafsi kama mtawala; mataizo makubwa ya nchi za dunia ya tatu kiuchumi yalitokana na structural adjustment programme iliyoasisiwa na IMF na WB hakuna hata nchi moja ya dunia ya 3 iliyonufaika nayo; Brazil walijitoa kwenye SAPII walibuni mpango wao kiuchumi kwa kutumia rasimali zake na hiyo iliyoleta mapinduzi ya kiuchumi tunayoyaona leo; acheni viongozi wanaojinadi kwa kutumia mema ya Mwalimu hayo ndiyo yanayotupa ushindi CCM; hivi ulitaka wajinadi kwa kutumia wizi na ubadhirfu uliopo sasa?Mnaposema hayo mapungufu msiishie hapo toeni na solution yaani hamuoni hata aibu miaka 30 bado mnahubiri mapungufu lini mtaanza kuwapa wanachi majibu sahihi ya kiuchumi tuliyonayo? Nina uhakika kama Mwalimu angepewa fursa angalau ya 25% tu ya favor za mikopo ni wazi tungekuwa mbali sana bahati mbaya sana western donors walimuona kama adui yao kwasababu alikataa kuizachia rasimali kwao; kuhoji mapungufu sio kosa kosa ni pale mnaposhindwa kuja na ufumbuzi yakinifu ya nini kifanyike
 
- HA! HA! my bro, unaweza kuruka kulia na kukaa chini, lakini huwezi kubadili ukweli kwamba USA leo inatokana na foundation iliyowekwa na Baba wa Taifa lao George Washington, so is us haya ndio matunda ya Foundation iliyowekwa na Mwalimu, na ni mapungufu yake ndio yanatutesa mpaka leo!!

- Mpaka mtakaporuhusu mijadala huru ya mapungufu ya Mwalimu ndio taifa hili tutaweza kujirekebisha!!

Le Mutuz


Oh, Yeah the FOUNDATION ya US pamoja na wewe kuzisifia aliimarisha UTUMWA alikuwa na MTUMWA hadi BAFUNI KWAKE...

Aliwanyima Uhuru na NGUVU za KIUCHUMI Wazawa wa USA ambao ni AMERICAN INDIANS na kuwaweka kwenye CONCENTRATION CAMPS for the sake of them WHITES to rule and take over the LAND

Yeah, kila kitu walijua watatumia LABOR ya aina GANI --- WATUMWA BLACKS.... Wana MISULI; WAKUBWA; WANATISHA ukiwapa MLO wa SIKU MBILI wanabeba JIWE zito kujenga MAHAKAMA; MADARAJA; SHULE; HOSPITALI; KULIMA MASHAMBA... oh yeah bring them slaves will do anything na saa nyingine wakifanya vibaya SHOT DAMN BASTARDS...

Yeah, Kwako wewe AMERICA iliprosper na haukuona KOSA LOLOTE sababu kulikuwa na VITENDEA kazi na pia UNYANYASAJI wa hali ya JUU....

** Sasa ANGALIA JIRANI ZETU KENYA.... Kabila ambalo ni la HALI ya na MALI ni WA-KIKUYU; wao ndio wana ELIMU kupita Makabila Mengine; Wana Utajiri; Wana ARDHI BORA; Maviwanda; Mabenki Almost all Major Means of PRODUCTION ziko Mikononi Mwao....

What ARE you going to tell them? Ukiangalia URAIS na UMAKAMU wa URAIS ni always the KIKUYUS...

*** UKIANGALIA UGANDA; Milton Obote alichezacheza na Uongozi wake akaingia a REAL DICTATOR; akaanza kuchanja Wanaadamu kama KUNI; hakujali uko pale kumtetea au la; itikadi zako au la; yeye ni na waganga na vipusa... Sasa nadhani na yeye kaiachia UGANDA raha za kuongelea?

**** Tunakuja kwa KIONGOZI tunayemlaumu... Yeye pamoja na kuwa na MAKABILA 5 Makubwa... alienda kwenye MOJA ya kabila lililoko NYUMA kabisaaa kimaendeleo akachagua NDUGU wawili JOHN MALECELA na JOB LUSINDE ???

Nyerere aliondoa UCHIEF; UMANGI, sababu hizo ni MOJA ya MATABAKA ya kuabudu Mwanadamu ndani ya JAMII ingeendelea sidhani kama NCHI yetu ingekuwa salama kama ilivyo sasa hivi; pamoja na matatizo madogo yaliyoanza karibuni...

Pamoja na kuwa alitaifisha SHULE wengine ambao ni tayari walikuwa MIDDLE CLASS or UPPER CLASS hawafurahii hatua hiyo sababu; Kama wewe Mzee Malecela alikuwa ameisha soma tayari na sidhani kama wewe kama MWANAE ungefurahia kusoma na watoto wanaokwenda shule na KANDAMBILI... Ulikuwa Different Class... Different HEAD... lakini aliondoa hiyo na wengi walisoma... TATIZO NI KUWA WENGI WAKISHA PATA ELIMU WANAJIDAI KUSAHAU WALIKOTOKA and they ERASE THEIR OLD MEMORIES...

Angalia; Hadi leo USA sio kila STATE kila MTU anaweza kuishi FREELY bila kuulizwa maswali au kubaguliwa; ANGALIA TANGANYIKA; unabeba virago vyako UNAHAMIA MBOZI, MBEYA hakuna anayekuuliza au kukutishia sababu ya JINA lako la MWISHO... THE PEACE the BREATH of FRESH AIR

Lakini watu hatuoni hayo; Tunataka tujilinganishe na JIJI LA NEW YORK; TOTO's MOVIE STARS; FASHION SHOWS kila siku...

We really have the Problems... Umeona NYERERE BANK ACCOUNT YAKE USWISI haikuwa na DOLA BILLIONI 40; ilikuwa 0 na Madini aliyaacha ARDHINI Mpaka hapo tutakapokuwa tayari sisi wenyewe...

Hauoni hiyo ilikuwa inatosha?????

Kuna MSEMO wa Wazungu Unasema;
The best and most beautiful things in the world cannot be seen or even touched. They must be felt with the heart.
 
Nani alikudanganya China ilikuwa Wajamaa? kumbuka ujamaa na ukomunisti ni vitu viwili tofauti.

Wachina wamezaliwa na DNA ya Kibepari. Angalia Singapore, Macau, Hong Kong. Kwao China walipopewa uhuru wa biashara tu, wakatajirika haraka haraka na kujenga nchi yao baada ya Deng Xiaoping kutoa rukhsa na kusema "getting rich is glorious". Mpaka sasa milioni mia tatu ya Wachina wametoka kwenye umasikini na kuingia kwenye utajiri wa kati (middle class). Mchina kama Mjapani, katika miaka 20, kaende kujisomesha na kurudi kwao na kuunda vitu vya kuuza kwa kukopi na sasa hivi anatengeneza magari, simu na kadhalika. Sisi tumefanya nini tangu kupewa rukhsa na Mwinyi? Hii ndio tofauti kubwa baina yao an sisi: uchapaji kazi. Tanzania Mhindi atatoa ajiira ya watu watano: Kuwasha taa, kufunga kufuli duka, kufagia duka, kuweka vitu vya mteja katika mifuko na kumtilia Bosi chai kikombeni. Mchina atafanya kazi hizo na familia yake nzima huku akiwasomesha watoto wake pembeni mwa duka,iwe Tanzania, Malaysia, Fiji au Marekani. Nilipokuwa chuoni Marekani, Mwanafunzi wa Kichina alikuwa anafua nguo zake chooni na kuzianika chumbani badala ya kutumia mashine za kufulia na kukaushakwa kulipa senti 25 (Quarter) kwa nusu saa. Leo ana kiwanda cha nguo. Sisi tunawasubiri watujengee uwanja wa mpira, treni, chuo cha kijeshi na kutukopesha. Kama Mwalimu alikuwa kiongozi bora kama anavyosifiwa basi Tanzania ingekuwa kama Singapore leo. Sisi leo tunaenda kwao kufundishwa namna ya kufanya biashara au kutibu wakati sisi tulikuwa matajiri kuliko wao tulipopewa Uhuru. Pia, badala ya kulalamika kuwa migodi yetu inaibiwa na wazungu au serikali yetu inasaini mikataba mibovu na wageni, kwa nini asijitokeze Mtanzania na kwenda kuchimba kama ana elimu ya kutosha na uwezo? Action speaks better than words! Tusikae an kulalamika tu na kukubali status quo, nenda katoe jasho kama mwenzako halafu lalamika.
 
Mjadala huu umekuwa VERY INTERESTING!
Sijui dogo sliyeamsha mizimu ya utaifa wa Tanzania ana fuatilia lakini?
 
Nisaidieni wakuu.
1. Katiba ya ccm inasema nini juu ya falsafa ya uchumi?

2. Je, mkulima mdogo (a peasant) na mfanyakazi analindwaje na 'uharamia' wa ubepari hasa soko huria?

3. Ni kweli Mwalimu alikosea kuhusu uchumi, kipi mlichopatia?

4. Machinga akiwa Mtwara ni muhaini, muhalifu na mhuni, akiwa Dar ni mzururaji na mfanyabiashara 'haramu'. Je, ccm inafanya nini kukuza wigo wa ajira kwa vijana?

5. Zoba na 'dhaifu' wa uchumi Mwalimu alihifadhi na kulinda raslimali za nchi zitumike kwa uangalifu na kizazi elevu kijacho. Kizazi 'kilichotayari' cha Wajanja, Mkapa na Kikwete wamegawa mashirika ya umma yote, wanagawa na kugawana madini kwa bei chee, watoa gesi kwa mikataba ya 'kificho', wanawalinda wafanyabiashara wakubwa, wagawa na kugawana ardhi ya wananchi, na wanajitajirisha wakiwa madarakani. Je, ni lipi tujifunze toka kwao hawa kizazi kipya cha viongozi?
 
Mjadala huu umekuwa VERY INTERESTING!
Sijui dogo sliyeamsha mizimu ya utaifa wa Tanzania ana fuatilia lakini?

Mkuu sidhani kama anafuatilia kwasababu angekua smart enough na kwa nafasi aliyo nayo ktk CCM hasinge zungumza ujinga kama huu. Watu kama huyu wamepataje hizi nafasi?

Nani kamwambia Tanzania ya Nyerere watu walikua wanakaa vijiweni kama sasa?! Kule vijijini ilikua lazima kila kaya kuwa na shamba la kaye na kila kijiji kilikua na shamba la kijiji! Kulewa pombe asubuhi ilikua marufuku. Sasa hawa madogo wameshindwa kuongoza wana mkejeli Mwalimu Nyerere!
 
Ng'wamapalala
Mwalimu alikiri wazi makosa yake kama kiongozi wala hakuona vibaya kulisema hilo; unataka ktupa lawama ambazo hazina msingi ni mara ngapi wakati Mwalimu IMF na WB ziligomea kutoa mikopo kwa Tanzania? Mara nyingi aliweka maslahi ya taifa hili mbele hizi rasimali mnazodai zinaibiwa hivi sasa zilikuwepo wakati Mwalimu alijua kulinda ili zinufaishe watanzania hakuangalia maslahi yake binafsi kama mtawala; mataizo makubwa ya nchi za dunia ya tatu kiuchumi yalitokana na structural adjustment programme iliyoasisiwa na IMF na WB hakuna hata nchi moja ya dunia ya 3 iliyonufaika nayo; Brazil walijitoa kwenye SAPII walibuni mpango wao kiuchumi kwa kutumia rasimali zake na hiyo iliyoleta mapinduzi ya kiuchumi tunayoyaona leo;

Mkuu chama naomba unielewe kuwa sijasema kuwa hawa viongozi wetu wamefanya mazuri sana na wanastahili pongezi au hawa viongozi wetu wa sasa hawana mapungufu. la hasha na haiwezi ikatokea binadamu au taasisi isiyo na mapungufu hapa duniani.

Katika maisha yangu sijawahi na sitawahi kuwa mpenzi au mfuasi wa siasa za IMF and World Bank na hata kama ukifuatilia mabandiko yangu hapa JF utagundua niko against policies zake.

Mwl.Nyerere kukataa msaada kutoka IMF and World bank bila kutafuta dawa ya matatizo aliyoyasabisha ambayo yalikuwa yanaikabili nchi wala haikusaidia hata kidogo kwa sababu nchi iliendelea kudidimia kiuchumi kutokana na siasa zake mpaka alipozinduka kwenye fikra halisia na kuamua kuficha uso kwa 'kung'atuka'. Kwa nini asubiri mpaka nchi itake kuwa bankruptcy ndiyo 'anag'atuke' wakati alikuwa ni 'visionary leader'. Nini kilimfanya akaendelea kufikiria kama mtazamo wake kiuchumi utaliondoa taifa katika umasikini. Huwezi kumpongeza mgonjwa kwa kukataa kunywa dawa yenye athari mwilini na pia ukaendelea tena kumpongeza pale alipoamua kunywa dawa ambayo ameendelea kunywa kwa muda mrefu bila kupata nafuu zaidi ya kuendelea kudhoofu kiafya.

Kitu ambacho labda ungejiuliza, kama kweli Mwl. Nyerere alikuwa such 'visionary leader' kwa nini nchi alifikia kwenye hatua ya kutaka kuwa bankruptcy ikiwa mikononi mwake na kuanza kutafuta misaada kwa donor agencies ili kujinasua kwenye tope la kiuchumi alilolisabisha mpaka kukumbana na masharti ya IMF, World Bank and 'big boys'.

Maswala ya kiuchumi ya Brazil huwezi kuyalingamisha na Tanzania. Ni rahisi sana kuangalia nchi fulani na kusema kwa nini na sisi tusingekuwa hivi. Historia ya taifa, changamoto na wananchi wake ni angalizo kuu katika kujinasua kwenye tope la umasikini. Tanzania haiwezi kuwa kama Brazil na Brazil haiwezi kuwa kama Tanzania kutokana na angalizo nililolisema ikichukuliwa Brazil ilipata uhuru wake 1823 (kama niko sahihi)

acheni viongozi wanaojinadi kwa kutumia mema ya Mwalimu hayo ndiyo yanayotupa ushindi CCM; hivi ulitaka wajinadi kwa kutumia wizi na ubadhirfu uliopo sasa?Mnaposema hayo mapungufu msiishie hapo toeni na solution yaani hamuoni hata aibu miaka 30 bado mnahubiri mapungufu lini mtaanza kuwapa wanachi majibu sahihi ya kiuchumi tuliyonayo?

Mapungufu ya Mwl. Nyerere lazima tu tuyaseme na tutaendelea kuyasema kama njia ya kujitambua kwa sababu chanzo cha changamoto ambazo tunakumbana nazo kwa sasa zilianzishwa na policy za Mwl.Nyerere. Hutuwezi kumwita Baba wa taifa kwa mazuri peke yake bali lazima pia awe Baba wa taifa kwa mabaya aliyoyafanya nchini hasa kiuchumi.

Nina uhakika kama Mwalimu angepewa fursa angalau ya 25% tu ya favor za mikopo ni wazi tungekuwa mbali sana bahati mbaya sana western donors walimuona kama adui yao kwasababu alikataa kuizachia rasimali kwao; kuhoji mapungufu sio kosa kosa ni pale mnaposhindwa kuja na ufumbuzi yakinifu ya nini kifanyike
Huoni kama point yako hapa unajichanganya.

Mikopo haina favor na haipata kuwa na favor. Tumelazimika kuchukua mikopo kwa sababu hatukuwa na njia nyingine ya kukabiliana na changamoto zilizokuwa zinahitaji jibu la haraka. Kama mikopo ingekuwa na hiyo favor basi Mwl. Nyerere angeichukua hiyo mikopo kwa maana nyingine pamoja na uji-'genius' wake hakuona kama kuna favor ndani yake ambazo ungependa kwa sasa awe ni yeye kwenye usukani wa maendeleo.

Huwezi kuniambia Tanzania ya leo ni Tanzania amabayo aliiacha Mwl. Nyerere ambapo hata hati ya kusafiria ilikuwa ni BIG DEAL huku majani ya miti yakiwa ni sabuni za kufuria na dawa ya meno ikiwa ni majivu.

Kama nilivyosema, ni rahisi sana kuona mapungufu ya utawala kuanzia kwa Rais Mkapa na Rais Kikwete kwa sababu milango ya habari iko wazi. I wish, milango ya habari kama hii ingekuwa hata kipindi cha Mwl. Nyerere.

Don't even start.
 
You can never get a loan if you are unable to repay. Simpo rule.
Faiza - have you ever heard of 'Bad Debts' in accountancy where debtors fail to repay their loans? And therefore the debts are written off. Ni mara ngapi Tanzania imesamehewa madeni na wadaiwa wake wa kimataifa madeni. Ni juzi juzi tu hapa Brazil wame isamehe Tanzania madeni yake! Labda tu kwenda mbele kidogo; hilo deni la Taifa ambalo muda si mrefu litafikia TZS 30 Trillion ita guarantee royalty ya 3% indefinitely kwenye mauzo ya madini yote yaliyopo na yatakyo vumbuliwa ambayo wewe uniapigia chapuo bila kujua tume rudi utumwani!
 
Mkuu Chama - huu ni wito tosha. Nimegundua true Leadership Qualities ni zaidi ya academic qualifications..
 
Mkuu chama kwa wana CCM ambao kwa kweli wanaamini misingi ya kiutu iliyowekwa na Mwalimu, statements za huyu kijana J Slaa inaonyesha jinsi chama kinavyozidi kukosa connection na wenye chama, watu wa kawaida.

There is something definately wrong na CCM!
Siyo uongo kuwa kama Mwalimu au kiongozi mwingine yeyote wakati wa uhuru , ange anza na sera za kibepari, nina uhakika kuwa viongozi WOTE waliopo wasimgekuwepo.
Na sehemu zilizokuwa political/economic power centres kabla tu ya uhuru zinafahamika. Nyerere alizivunja centres hizo na kuleta umoja na amani ambayo naona wengine wetu tumeikinai.
 
Last edited by a moderator:
Hata mimi nilipokuwa mjinga nilikuwa na mawazo kama yake na baadhi yenu...ila nilipojua ukweli ni nikafahamu kiasi gani Siasa ya ujamaa na kujitegemea imesaidia nchi hii...kwa taarifa tu kwa wale ambao wanafurahi maisha yao sasa basi hayo ni matunda ya dhana hiyo...
Dhana ya ujamaa na kujitegemea ni pana sana, ni mjinga tu ndio atakuwa haino...

Ila going forward lazima tuwe na philosiphia yetu, ikiwezekana tuitengeneze
 
Ng'wamapalala
Nakujibu kwa ufupi alichokataa Mwalimu ni mataifa ya nje kuja kujitekea utajiri wetu ni kutuacha masikini na mikopo haijawa siri ya mafanikio ya nchi yoyote uligusia structural Aadjustments programme maarufu kama SAP nenda kaispme tena ndipo utakapojua siri ya mikopo nakupa nchi kaangalie NIGERIA kwenye hiyo SAP walikopo kiasi gani na wanalipa kiasi gani hadi leo hii na hakuna kilichofanyika; Mwalimu alikuwa sahihi pamoja na huo umaskini mnaodai alituacha nao hataukufikia hatua ya kama baadhi ya nchi ulaya hivi sasa baada ya wakoloni kulikosa bara la Afrika wameanza kulana nyama wenyewe kwa wenyewe kwa maana hiyo hata UBEPARI haujwa mfumo sahihi kwa maisha ya mwanadamu; hivi sasa Spain; Ureno; Greece; France kila siku ni maandamano mfumo umegoma; kabla hujamshtumu kiongozi wako ambaye bado anaheshimika na walio wengi duniani fuatilia siasa za dunia; kama utapata nafasi nenda Library of Congress kuna speech amabayo aliitoa Mwalimu Cancun alipokuwa msemaji wa nchi masikini raisi Reagan aliomba kukutana na Mwalimu yule mtu alikuwa kihwa mtakesha sana kuharibu na kuchafua jina lake lakini duniani anafahamika sana na hadi leo hii ndiye anayelibeba jina la Tanzania.
 
Faiza - have you ever heard of 'Bad Debts' in accountancy where debtors fail to repay their loans? And therefore the debts are written off. Ni mara ngapi Tanzania imesamehewa madeni na wadaiwa wake wa kimataifa madeni. Ni juzi juzi tu hapa Brazil wame isamehe Tanzania madeni yake! Labda tu kwenda mbele kidogo; hilo deni la Taifa ambalo muda si mrefu litafikia TZS 30 Trillion ita guarantee royalty ya 3% indefinitely kwenye mauzo ya madini yote yaliyopo na yatakyo vumbuliwa ambayo wewe uniapigia chapuo bila kujua tume rudi utumwani!

Kusamehewa madeni si kigezo cha kupewa mkopo. Kigezo cha kupewa mkopo ni kimoja tu, kuwa una uwezo wa kulilipa. Kumbuka hilo.
 
Faiza - have you ever heard of 'Bad Debts' in accountancy where debtors fail to repay their loans? And therefore the debts are written off. Ni mara ngapi Tanzania imesamehewa madeni na wadaiwa wake wa kimataifa madeni. Ni juzi juzi tu hapa Brazil wame isamehe Tanzania madeni yake! Labda tu kwenda mbele kidogo; hilo deni la Taifa ambalo muda si mrefu litafikia TZS 30 Trillion ita guarantee royalty ya 3% indefinitely kwenye mauzo ya madini yote yaliyopo na yatakyo vumbuliwa ambayo wewe uniapigia chapuo bila kujua tume rudi utumwani!

Kuna tofauti ya ku default kwa kuwa huwezi kulipa deni , kusamehewa deni kwa sababu za kisiasa na urafiki na kuomba mkopo open market. Nchi yoyote ikiwa masikini na uchumi wake mdogo inategemea serikali rafiki nje kukopa. Na hapo mara nyingi riba ipo chini kuliko riba ya soko, pia kwa sababu ya urafiki na siasa, Kama nchi inashindwa kulipa deni, wanasamehewa au wanapunguziwa deni. Tanzania haiwezi kukopa open market kwa sababu ya umaskini wetu. Dubai , USA, au Singapore anaweza kukopa anavyotaka kwa kuwa Uchumi wao unaruhusu. Unaweza kuona deni letu ni kubwa sana lakini kuna projects nchi za kutajiri wanakopa kiasi hicho kwa kulipia project Moja tu! Bahati nzuri Mchina ni tajiri sasa na ni rafiki wa TZ,ndio maana tunakopa billioni Moja dola hapa na pale ambayo kwa nchi tajiri ni pesa ndogo sana. Dubai kuna Wakati walidaiwa dola bilioni 80, na Abu Dhabi ikamsaidia mkopo huo ndugu yao. ilikuwa wa default. Wangefanya hivyo benki ingewapa mkopo kwa riba kubwa sana. Kama nchi imebanwa kukopa open market, hawawezi kujenga nchi haraka. China akibadili roho kesho, Tanzania tumekwisha. Na uchumi wote Afrika, tulipeleka bakuli Beijing kujengewa HQ ya Umoja wa Afrika huko Addis Ababa kwa gharama ya milioni 300 kwa Mchina. So, hapa hamna utumwa, ni siasa na biashara tu. Kama huna ubavu, utakopeshwa na washikaji hela mbuzi (kwa kiwango cha mahitaji ya nchi). Kwa kukuonyesha jinsi $10 billion ni hela mbuzi japokuwa sisi bado tunashindwa kulipa hilo deni miska sasa, serikali ya Marekani inatumia kiasi hicho kwa siku MOJA katika bajeti yake. Kiasi hicho pia ni msaada wa kijeshi kwa nchi moja, Isreal. Nadhani unaona picha jinsi tulivyo nyuma kiuchumi.
 
Kusamehewa madeni si kigezo cha kupewa mkopo. Kigezo cha kupewa mkopo ni kimoja tu, kuwa una uwezo wa kulilipa. Kumbuka hilo.
Hivyo Kwa mtazamo wako viongozi wa leo ambao wamelitishwa Taifa deni karibia TZS 30 Trillion ni BORA kuliko Mzee Kambarage ambaye aliacha nchi na deni SIFURI?
 
Tutakuwa hatuwatendei haki hayati Mwl Nyerere na Mstahiki Meya Bw Slaa kama tutawashambulia/tutawajadili wao kama watu binafsi.
Hawa ni binadamu na si malaika na wote wana mapungufu yao kama binadamu.
Suala lilikuwa ni Ujamaa na ubaya wake na jinsi ulivyosababisha Watanzania tukawa wavivu na wategemezi.
Pengine ni mwafaka mashabiki wa Ujamaa wautetee Ujamaa na Kujitegemea na wale wa Ubepari wafanye hivyo na si ushabiki kati ya Nyerere na Slaa.
 
- Hela aliiba Meneja wa Gapex kutoka Musoma, enzi za Awamu ya kwanza alifanywa nini? Sasa ndio iwe EPA afadhali hao wanarudisha, SUKITA ilianza na kufa under nani? Air Tanzania ilianzishwa na kuuliwa under utawala wa nani? waliohusika walifanywa nini Mkuu? Waacheni wananchi alijadili Taifa lao bila kuwatisha, infact kuna muandishi wa habari aliyejaribu sana kufuatilia kufa kwa Gapex, akaishia kuitwa Ikulu na Butiku na kutishiwa sana na wiki iliyofuata akahamishiwa Ubalozini UK, please wacheni wananchi wazungumze,

- Jerry Silaa ni kichwa sana namuaminia sana na niliwahi hata kuandika articel kub wa sana kukitaka chama changu kimpe nafasi kubwa kwenye chama ninashukuru sana kwamba chama changu kilisikia, amesema anachoamini kuwa ndio tatizo na wewe sema lako sio kukubisha bisha bila hoja za msingi hapa, Mwalimu alikuwa binadam kama wengine wote kuna mtu mmoja hap anashauri nikasome kitabu cha kujikosoa cha Mwalimu huyo huyo aliyetuwekea foundation mbovu hili taifa, ndio huwa ninajiuliza sana hivi hili taifa tulilogwa na nani hasa? that we cant think right kila siku kutetea mediocre tu!!

Le Mutuz

Mkuu na mie ni sehemu ya wananchi ambao unasema waacheni wazungumze pia mie zibishani kwani hainisaidii chochote, hapa ni sehemu ya kujadiliana na mwisho wa siku kila mtu anatoka na lake kwani sifa kuu za binadamu ni kutofautiana hoja lakini mwisho wa siku kila mtu anakuwa ame-gain kutoka kwa mwenzake na ndio maana binadamu huwa tuna mikutano katika maeneo yetu kwani kichwa kimoja hakiwezi kutoa conclusin on behalf of others hivyo tuache tujadili hata kama tupo tofauti na wewe mwisho wa siku tunaweza kubadili msimamo kwani kila kitu kina mazuri na mabaya yake kwani mfumo ule ulitubeba sana sie tuliokulia kule vijijini Mahomajika kwa upande wa masuala ya elimu huko upande wa kiuchumi kiukweli kulikuwa kuna shida but bado chain ilikuwa ndefu mno kwani makosa ni ya wengi hata hao viongozi waliokuwa chini yake nao ni tatizo kwanini hawakukomaa kiasi kwamba mkuu wa nchi awe msemaji kuanzia serikali kuu au kule juu kwenye baraza la mawaziri mpaka huku chini kwa wenyeviti wa vijiji kama sio vitongoji
 
Tutakuwa hatuwatendei haki hayati Mwl Nyerere na Mstahiki Meya Bw Slaa kama tutawashambulia/tutawajadili wao kama watu binafsi.
Hawa ni binadamu na si malaika na wote wana mapungufu yao kama binadamu.
Suala lilikuwa ni Ujamaa na ubaya wake na jinsi ulivyosababisha Watanzania tukawa wavivu na wategemezi.
Pengine ni mwafaka mashabiki wa Ujamaa wautetee Ujamaa na Kujitegemea na wale wa Ubepari wafanye hivyo na si ushabiki kati ya Nyerere na Slaa.

Wewe ndio umemaliza kabisa na sidhani kama hivi vilivyoanzishwa vilikuwa vina nia mbaya kwani kinachotakiwa ni kukubali matokeo kama Ujamaa na Kujitegemea ulikuwa una shida kwenye maeneo flani basi tuboreshe katika maeneo flani hasa ukizingatia kwa nchi kama yetu hata huo ubepari tunaouzungumzia ni tofauti na nchi za wenzetu wa magharibi. Mie ninaamini kila kitu kina enzi zake na kwa kipindi kile ndio msimamo wa nchi ulikuwa hivyo whether ulikuwa ni maamuzi ya mtu mmoja or not, kulaumu mtu tena ambae hayupo kwenye ulimwengu wetu haitasaidia na ndicho kinachotufanya wakati mwingine tusisonge mbele maana Watz ni mabingwa wa kujadili mapungufu yetu bila kujadili way forward
 
Back
Top Bottom