Meya Boniphace Jacob amfungukia RC Makonda

Meya Boniphace Jacob amfungukia RC Makonda

Hivi neno UBASHITE limetumika kama UKILAZA!?! Nahisi kuelewa
 
Njia za kufikisha taarifa ziko nyingi na mojawapo ni mitandao ya kijamii. Ni jukumu sasa la mamlaka husika (Polisi, et. al.) kuzifanyia kazi tuhuma/taarifa hizi. Wananchi wametimiza wajibu wao; usiwape kazi isiyowahusu.

Mbona taarifa zimeshawahi kutolewa humu nyingi tu lakini hazijafanyiwa kazi eti kwa vile hakuna mlalamikaji? Yule jamaa Msemakweli aliwahi kutoa taarifa hazikufanyiwa kazi, watu wakadai kuwa Mwenyekiti Freeman alipewa nafasi Ihungo pasipo kupitia kidato cha nne hazikufanyiwa kazi. Ndio maana kwa ufahamu wako wa NECTA and what what what nikakushauri angalau utume malalamiko NECTA au polisi, sasa sijui huna uhakika na umbea unaoushabikia
 
Ndugu yangu
Dear
Daudi Albert Bashite.

Naanza na salamu na badala ya salamu ni kujua kama umeamka vizuri hapo kwako Masaki,na shemeji yetu naye natumaini ni mzima wa Afya.

Kwa uchache wa Muda naomba niende moja kwa moja kwenye dhumuni langu la kukuandikia ujumbe huu,hakika ujue sikupi pole sababu mambo Mengi umejitakia katika safari yako ya kisiasa,iliyo jaa vishindo na mbwembwe za kila aina.

Vijana wenzio tulibahatika kufanya kazi na wewe Daudi, kwakweli hatukuwahi kujua siri ya "kiburi" chako na "majivuno" yako uliyatoa wapi? Kwa jinsi ulivyokuwa kijana wa "Mission impossible" katika kila matendo ya vijana wa kaida yanayotarajiwa wewe ulitenda yale ambayo watu wasinge tarajia kuona,

Na hayo ndiyo yakawa maisha yako,hukujali wakubwa wanastahili heshima,hukujali kila binadamu anastahili staha,huku jali viongozi kama Mawaziri wa kuu au majaji wataafu walipaswa kulindwa na kuhifadhiwa.

Leo kabla Dunia haijaona mwanzo mpya au mwisho wa safari yako,kwakuwa Kwa namna yoyote vile tuta ulilokutana nalo Masihani mwako halitakuacha kama awali,utabadilika tuh utake usitake Hata kama mabadiliko yako yawe ya Nafasi au Nafsi yanakukuta kwa aibu na fedheha.

Walio karibu yako Daudi wanadai unawakati Mgumu,tukuombee,sitaki kuwa mnafki kwako,Daudi nikwambie tuh sitokuombea bali kabla ujamaliza kujutia Nafsi yako nikukumbushe tuh machache ili uyaingize kwenye sala ya toba.

1.Akilini kwako unamkumbuka baba wa watu? Mkurugenzi injinia mussa Natty,ulivyo muandama mpaka kusimamishwa kazi ulipokuwa DC KINONDONI? huku jali elimu yake aliyosomeshwa na wazazi wake masikini huko shinyanga,kwa UBASHITE WAKO ukamuumiza yeye na familia yake.

2.Je unawakumbuka wahandisi wa Halmashauri ya manispaa ya Kinondoni?,uliowasemea Mbele ya mheshimiwa Rais,siku ile Pale Biafra,wenzio wakasimamishwa kazi,na kuhamishiwa vijijini,hukujali elimu yao ya kweli si kama yako,waliyo ipata kwa shida wala familia zao masikini zilizo wategemea,Kwa UBASHITE WAKO ukawatokomeza na kuwaharibia majina na kazi zao.

3.Je unawakumbuka Maafisa ardhi? ukitoa amri wakamatwe kule Wazo mivumoni tuh kwa sababu walichelewa kufika eneo la tukio baada yako,hukujali Elimu zao na utaalamu wao wa ardhi waliosotea mashuleni na vyuoni ,kitichako kilikuwa na mamlaka ya kuwalaza wote sita mahabusu kituo cha mabatini KWA UBASHITE WAKO ukajiona wewe ni alpha na omega.

4.Je unamkumbuka yule dada Afisa ardhi uliye Muita "Tahira" kule kwenye mkutano wako mabwepande? Tena mbele za Tv na Radio zikiwa Mubashara,Hukujali mwenzio ana vyeti halali na amepimwa kwenye mitihani na amefaulu, KWA UBASHITE WAKO ukaona hakuna atakacho kufanya wala pakukimbilia.

5.Je unakumbuka ile kauli yako kwamba wewe ufanyalo Dar es salaaam,na kuliamua juu yake ni kwamba ameamua Mungu,Hata watu walipo toa miguno ya kulewa kwako madaraka hukuwahi kujutia kijivika utukufu wa Mungu,wala kujifananisha naye au kujipa unabii juu ya Dar es salaam,KWA UBASHITE WAKO ulidhani na yeye Mungu alipata zero? Au Mungu alinunua vyeti?

6.Je unaikumbuka ile kauli yako ya mara kwa mara uliyopenda kuitoa kwamba "Mimi nimbabe wa vita" ulimaanisha vita vya kufeli na kufanya "manuva" vita ya kutorudia au kukariri Darasa? Na ukazani umevishinda vita kwa kununua jina jipya, KWA UBASHITE WAKO,Ukasahau kuwa wazungu wanasema "There is no short cut in alife" isipokuwa wewe ukazani umeyapitia Denge maisha,wenzio wasome wafaulu,wewe ufeli ujekuwa boss wao.

7.Je unakumbuka Ile kauli yako ya kuwa ofisi ya mkuu wa mkoa Dar es salaam nzima inawafanyakazi 4,wengine wote ni mizigo? ,sasa utawaonea wivu hao mizigo kwakuwa wenzio wanavyeti na walifaulu wapo kihalali serikalini basi huenda utawaacha hapo na wewe mzigo namba moja utaondoka badala yao.KWA UBASHITE WAKO uliona kila mtu aliyesoma vigezo siyo kusoma ila ujanja kama uliotumia wewe.

Na mengine Mengi sababu ya Muda Nikuache na hayo,Niwache na boss wako muamue Mpangiane kazi gani nyingine,na kwa bahati mbaya mfumo wa nchi yetu,mwenye division zero,hastahili kuwa hata Dereva serikalini.

Fedheha na aibu imepanda gari lako la kifahari,imeingia ndani ya jumba lako hapo masaki,walinzi wote polisi na wanajeshi wameshindwa kuizuia,ipo mpaka sebuleni na sasa ujue Dar es salaam haitokubali itawaliwe na kuongozwa na KILAZA.......KUSOMA RAHA SANA

Na
BONIFACE JACOB
Senior councilor ubungo
Mstahiki meya
Manispaa ya ubungo
Ndugu yangu Meya na wewe umeingia ktk malumbano ya hoja au habari za udaku za kusoma mitandaoni.

Ni kweli hayo aliyofanya ktk utumishi wake lakini si sababu kuwa kigezo ni vyeti.

Hayo angeweza kufanya hata mwingine yoyote yule.

Mbeya Fanya kazi achana na maneno ya udaku hayo yatakuvunjia heshima yako.
 
Kumbe ni mwajiriwa wa nani???? Hebu tutajie jina lake basi ni nani???? acha kutetea kitu usichokijua.Kwa hiyo kwenye zoezi la vyeti waliohukumiwa tuwafanyeje????

Duuuh, kumbe tuna watu humu wasiofahamu namna hii, halafu eti great thinkers. Haya basi, Mkuu wa Mkoa ni mwajiriwa wa serikali.
 
Huyu Daudi Bashite anastahili kunyongwa kwa wizi wa cheti. Kusoma asome mwengine then yeye aje kula matunda asiyofanyia kazi. Haiwezekani hata kidogo.
 
Duuh! Ila najua nakuamini kuwa Bwana Daudi alitumia muda wake mwingi kutengeneza idadi kubwa ya maadui ambayo sasa imemshika pabaya..

Nikusihi Bwana Daudi tubu tu dhambi yako maana uliyokuwa umeyaficha hayafichiki tena, kama ni choo chemba yake imevunjika sasa halafu ya mavi ni kila kona.
 
Utaratibu wakati mwingine unaweza ukawa si kitu unachokipenda lakini ndio utaratibu. Na kufikiri kwamba unachokipenda wewe ni utaratibu mzuri nako si sahihi. Mfano, Mh Freeman Aikaeli Mbowe anatuhumiwa kuwa hajamaliza kidato cha nne. Inawezekana katika fomu za kuomba uongozi CHADEMA katika vyeo vingine kuna kigezo cha elimu. Kuna watu wanaenguliwa na kamati kuu kwa kigezo hicho. Japo Mh Mbowe hajamaliza kidato cha nne kwa kuwa katika nafasi aliyoishika hicho si kigezo hatuwezi kumuhoji kwa nini Mh inaonekana ulisoma kidato cha tano na sita wakati hukumaliza kidato cha nne na wewe ni chairman? Huwezi, utaratibu hauko hivyo, utaratibu hauruhusu. Hilo ni jambo la msingi, kufahamu taratibu ya kitu kabla hujaamua kukipenda au kukishiriki. Labda kama Makonda kamdanganya Rais, vinginevyo ni kelele tu za mlango!
Kwani na mbowe anacheti feki au Bashite tu!?
 
Kila liendalo hurudi,kila kitu kina matokeo yake,na ukweli ndio huo,mwisho wa ubaya ni aibu.
 
Mbona ya mbowe hamsemi ? Mti wenye matunda ndio hupigwa mawe makonda piga kazi achana namaneno yawakosaji

Kwani ndiye Daud Albert Bashite anayeongelewa hapa?" Mkuu, angalia usije akaisaidia polisi maana wewe unakuja kumtaja Mh. wakati hakuna alipotajwa katika uzi hapo juu..
 
Usipoteze mjadala kwa kuanza ku personalize ishu! Utumishi wa umma ukoje? Ukaguzi wa vyeti kwa watumishi wa umma unawahusu wakuu wa mikoa? Hayo ndio mambo mimi nimeona uyafahamu, kwangu makonda sio ishu, ishu na uelewa wako juu ya utumishi wa umma. Ungefahamu taratibu zilizvyo kwanza ndipo ungekuwa na uwanja mpana wa kujadili au kukiwasilisha hicho ulichotaka kukiwakilisha. Kuwakilisha jambo ambalo hulifahamu sawasawa si vyema, pengine ulikuwa na mawazo mazuri lakini kwa kuwa hufahamu vitu fulani fulani basi uwasilishaji wako ukavizwa. Makonda ni muda tu, nae atapita lakini taratibu zetu za kuongoza nchi zikoje basi? Zina ubora na uimara kiasi gani? Je kwanza tunazifahamu uzuri?

Mkuu, kwani Mkuu wa Mkoa si Mtumishi wa Umma? Hebu tuelimishe vizuri....
 
Ni kweli barua hii ya Meya wa Ubungo imeegemea kwenye chuki na hasira aliyonayo kwa mheshimiwa mkuu wa DSM. LAKINI kama kweli hayo yaliyoandikwa pale ni kweli. Mkuu wa Kaya DSM unabidi ujiondoe tu hakuna namna kujifananisha na Mungu ni kosa Kubwa. ...
Kuna kaukweli fulani hivi! Unakumbuka tabia ya mh. ya dharau kwa viongozi wa Ukawa wanapoaliakwa/jialika kwenye shughuli mbalimbali za kitaifa? Jamaa alikuwa anawaruka wakiwemo mameya wala hawatambulishi. Kibinadamu haitegemewi Meya Boniface asiwe na hasira; that was too much. Heshima (kwa viongozi wenzio) na unyenyekevu hata kama una mamlaka kiasi gani ni tabia njema na muhimu kwa kiongozi.
 
25.Unakumbuka ulivyomnanihii Mzee Warioba?
Af je Bashite anakumbuka alivosababsha kifo cha mzee wetu mkurugenzi wa Jiji letu Pale Kigamboni bridge??? Dadadeki msumeno ukate pote[emoji123] [emoji123] [emoji123]
 
kweli hayo ni maneno ya mstahiki meya.kijana hajakomaa kisiasa.na wewe bashite jiuzuru acha kujikinga kwenye mwamvuri wa madawa ya kulevya.
 
Yaani hii yote ni Kwasababu anapambana na madawa sasa mlitaka watu waangamie na madawa ndio furaha yenu, Makonda pambana na madawa wataje wote waizaji na mateja bila kificho, nyoko zao wanaharibu watoto wa watu kwa madawa halafu mnajitia kuja juu na nyie wote wauzaji wakubwa mtaishia kudhalilika nyau nyie
 
Punguzeni mapovu mmeshapata sehem husika ukupeleka kero zenu pelekeni ili hatua sitahiki zichukuliwe
 
Kwani na mbowe anacheti feki au Bashite tu!?

Wote wawili wanatuhumiwa, lakini Mbowe hatakiwi kujiuzulu ila Bashite yeye anatakiwa kwa kuwa ni mtumishi wa umma na kiongozi wa upinzani bungeni ni mtumishi wa umma!
 
Back
Top Bottom