Meya Arusha: Aibu tupu!

Meya huchaguliwa na madiwani siyo wananchi wore.

hata kama anachaguliwa na madiwani, lakini anaongoza wananchiwote wa manispaa. Madiwani wanachagua kwa niaba ya wananchi wanaowawakilisha, kwa hiyo, suala la kukubalika kwake miongoni mwa wananchi ni la muhimu sana kwa utekelezaji wa kasi wa wa ajenda za maendeleo
 
Ni maumivu na manyanyaso makubwa wame2sababishia,wapo nduguze2 wamepoteza maisha,vilema vya kudumu nawengine uharibifu wa mali na yote hii ni kwasababu ya kulinda maslahi yao na hiki kim2 chao anyway wacha tu watuone mafala ila siku moja namba itasoma jamaangu.A_town juuuuuuuu......

mauaji ya kujitakia!
 
Hii nimeipenda watz tunazidi kuonesha msimamo kwa vitendo na sio maneno. Aluta continua kwa wana Arusha na kote harakati zinakoendelea.
 
Madiwani ni wawakilishi wa wananchi, huwezi kuwakwepa kwa namna yoyote. ni kwamba hakubaliki full stop, hata kama angejifungi namna gani!
 
Ikiisha CDM itafanya kazi gani?

avatar38074_1.gif
Mawazo yako yanafana na avatar yako. Hebu tuonyeshe na downstairs na mibangili hiyo
 
Huyu ni meya wa wanaccm, sio wa watu wa Arusha. Cha kusikitisha hapa ni tabia hii ya kukaidi matakwa ya wananchi inayojengwa na ccm. Naohofia matokeo yaweza kuwa kama ya Lybia, Yemen, na Syria watu wakichoka kiasi cha kufikia hatua ya no-return.
Jana kulikuwa na fainali za shindano la kuisaka bar inayochoma vizuri chini ya udhamini wa TBL.

Muda wote tulipokuwa pale palikuwa shwari na kazi ilikuwa ni kula nyama na bia. Mara MC akatangaza mgeni rasmi wa ile shughuli ni 'meya' wa Ar, eti Gaudence Lyimo, yule Diwani wa Moshono (CCM) alisababisha damu ya watu kumwagika! Hali ilibadilika, uwanja ukageuka wa siasa na ikawa ni malumbano na wengi wakisema Arusha bado hatuna meya.

Kwa kifupi ilikuwa ni zomeazomea na shughuli iliharibika! Nikawanajiuliza huyu anaona kabisa kwamba watu wasivyo mkubali, kwanini asikae pembeni? Nani anamsapoti wakati wananchi hawamtaki?

Nawasilisha
 
Meya huchaguliwa na madiwani siyo wananchi wore.kwa vile Chadema Ina madiwani 14 na CCM inao madiwani 16, Lyimo ndiyo meya wa Arusha. Kwamba anakataliwa katika hafla
ya nyama choma siyo hoja ya msingi. Munawapotezea wananchi wa Arusha kutafuta maendeleo Yao bure.Hilo ni jambo la kisheria mwenyewe ni Tundu lissu na siyo.
Maandamano wa mkutano wa hadhara.p

Mazungumzo siyo idadi ya madiwani; kinachozungumzwa ni meya mteule kuipata fresh ya wana arusha akiwa mgeni rasmi. Kwa vile ni kilaza kama baadhi ya wachangiaji somo halitapanda ila msg sent kwa vilaza wote na chama chao
 
hii ni kazi ya chama. Nadhani muda si mrefu wataelewa. Masikio yao yameanza kusikia uluzi...... Mkali. Eti wanajaribu kuzima changes.. How,... Wataelewa tuu
 
Meya huchaguliwa na madiwani siyo wananchi wore.kwa vile Chadema Ina madiwani 14 na CCM inao madiwani 16, Lyimo ndiyo meya wa Arusha. Kwamba anakataliwa katika hafla
ya nyama choma siyo hoja ya msingi. Munawapotezea wananchi wa Arusha kutafuta maendeleo Yao bure.Hilo ni jambo la kisheria mwenyewe ni Tundu lissu na siyo.
Maandamano wa mkutano wa hadhara.p
Jiulize hv? Yule Kivuyo wa TLP alikuwa na wenzake wa TLP wangapi kwenye uchaguzi? mbona alishinda nafasi ya pili(Unaibu meya?) nani aliyempigia kura? ukipata jibu ndio useme CHADEMA wasingeshinda kwa sababu wana madiwani 14. vinginevyo uko upande wa uongo au hujui nn kinaendelea katika nchi hii.
 
hahaaa yaani meya anaenda kuwa mgeni rasmi kwenye mishemishe za shindano la kuchoma nyama?kweli kazi ipo mwaka huu
 
Kwa mwenye taarifa naomba nieleweshwe huenda kuna wengine pia hawafaham;
1. Utetezi wa Lema kuhusu PM ulikuwaje, kuthibitisha kweli PM alidanganya? Ni kipi alidanganya na ukweli ni upi?
2. Kama uchaguzi itaamliwa urudiwe, CDM wana grounds zipi wanazoamini wanaweza kushinda? Yule wa TLP aliyeshinda najua ni janja ya ccm kuonyesha kulikua na uchaguzi huru na wa haki hata ikatokea baadhi ya wana ccm walimpigia kura TLP (kiini macho) lakini siamini sana kama itatokea hivyo kwa CDM hasa ukizingatia na jinsi sura ya tukio lenyewe ilivyo kwasasa.

Naomba mwenye majibu anihabarishe.
 
Namuonea huruma huyu meya wa kuchongwa na CCM na TAMISEMI. Wewe siyo kiongozi wa watu. Ungekua, ungeshangamua wanakuuza hao aibu hizi zitakuandama daima mpaka utapotia akili
 
Jana kulikuwa na fainali za shindano la kuisaka bar inayochoma vizuri chini ya udhamini wa TBL.

Muda wote tulipokuwa pale palikuwa shwari na kazi ilikuwa ni kula nyama na bia. Mara MC akatangaza mgeni rasmi wa ile shughuli ni 'meya' wa Ar, eti Gaudence Lyimo, yule Diwani wa Moshono (CCM) alisababisha damu ya watu kumwagika! Hali ilibadilika, uwanja ukageuka wa siasa na ikawa ni malumbano na wengi wakisema Arusha bado hatuna meya.

Kwa kifupi ilikuwa ni zomeazomea na shughuli iliharibika! Nikawanajiuliza huyu anaona kabisa kwamba watu wasivyo mkubali, kwanini asikae pembeni? Nani anamsapoti wakati wananchi hawamtaki?

Nawasilisha

Aaaaaaa kumbe kumzomea tu na kisheria anatambulika, hilo halina shida , na ni upuuzi kwani ushuru anakusanya na wao wenyewe ndio wanao jicheleweshea maendeleo yao wenyewe
 
'meya' wa Ar, eti Gaudence Lyimo, yule Diwani wa Moshono (CCM)

Gaudence Lymo ni Diwani wa Kata ya Oloirien na siyo wa Moshono.
Kuna umuhimu wa katiba kubadilishwa kuhusu chaguzi za mameya. Mfumo huu wa sasa wa madiwani kuchagua mameya umeshapitwa na wakati. Nchi nyingi duniani (hata Africa Mashariki) meya huchaguliwa na wakazi wa jiji au mijina na sio madiwani wachache ambao ni rahisi kuwahonga, ili apatikane mtu wao. Ziko tetesi kwamba huyu Gaudence alichangiwa hela nyingi ili aweze kuwa meya. Tunatakiwa kujiuliza, ni kwa sababu gani alichangiwa hizo hela? Atarudishaje fadhila kwa hao waliomchangia? Itakuwa ni vigumu sana yeye kujiuzulu kwa sababu lazima hizo hela alizochangiwa zirudi. Kingine ni huu mtindo uliozuka wa vijana kuwa madiwani au mameya. Nchi karibu zote duniani, madiwani na mameya ni watu wazima.. miaka hamsini na kuendelea. Huku kwetu wanaojitokeza ni vijana wadogo sana ambao bado wanatafuta maisha na kamwe hawatakuwa na nafasi ya kuhudumia jammii kwa sababu wao wenyewe hawajakaa sawa kimaisha au kiuchumi. Huyu Gaudence ni bado kijana na kazi yake ni contractor, mbaya zaidi kuna conflict of interest na shughuli nyingi za jiji... kwa hiyo ni dhahiri kwamba alitaka kuwa meya wa jiji kwa sababu zake binafsi na siyo kuwatumikia wananchi wa Arusha.


 

Similar Discussions

Back
Top Bottom