method mogella 'fundi'

Jamaa alikuwa Fundi haswa,mimi namkumbuka kwa jambo 1 tu miaka ile alipokuwa anacheza kwa kiwango cha juu nalo ni kuwaongoza Wachezaji wa Simba kutia mpira kwapani(kugomea mechi baada ya halftime), nakumbuka ilikuwa mechi dhidi ya Yanga.
 
Mogela alikua six yetu umiseta kanda ya kusini. ebwana jamaa namkumbuka kwa mengi wakati nakamata fullback ya kushoto mwanagu yuko shavu la kati. wanaokumbuka fainali ya mwaka 89 kusini na magharibi mtasema jinsi tulivyokua. acha tu mogela alikua na skills za mpira sana
 
Hebu jaribu kukumbuka vizuri, Method hakucheza Umisseta mwaka 1989. Mimi nilikuwa naye JKT Oljoro mwaka 89/90 baada ya yeye kumaliza TCA May 1989.
 
ni vizuri kuwaenzi wanamichezo wetu.nimepewa taarifa za umahiri wa method mogella uwanjani.
 
Ki ukweli ni mikasi tu ndie mchangiaji aliekuwa sahihi kuitoa story nzima ya marehemu Method mogella jamaa alijiover dose na alikuwa mgonjwa alirudishwa toka Abu dhab alipokuwa amekwenda na Costantine Kimanda deal liliofanikishwa na Mpondela castro ila cha kuongezea tulipokwenda kuaga mwili wa marehemu Msimbazi center alizikwa na mkufu mkubwa wa Dhahabu wa msalaba kitu kilichopelekea kufukuliwa mwili wake na vibaka ikabidi asubuhi watu wanapita makaburi ya Buguruni wanaukuta mwili wa marehemu upo nje akazikwa tena cha ajabu kifo chake kiliwagusa saana watu ambao nao sasa ni marahemu pia mziray.gaga.bambaga.boli zozo.kizota.stephe mussa na issa athuman ambaye mleta mada anamchanganya kifo chake na method issa athuman mgaya yeye ndie aliefia afrika kusini na kwa taarifa yako tu marehemu wote ukiacha kizota wanasadiiwa walikufa kwa upugufu wa kinga zinazopambana na maradhi nyemelezi
 

Mourad77 umenifurahisha sana kwa maelezo yako, coz katika wote hao ni KIZOTA tu ndiye aliyekufa kwa ajali
 


From Left; Hamisi Thobias Gaga(marehemu), Saidi Mwamba Kizota (marehemu), David Mwakalebela, Method Mogella (marehemu) Abeid Mziba, Ken Mkapa(captain) na Salum kabunda Ninja(marehemu).
 


From Left; Hamisi Thobias Gaga(marehemu), Saidi Mwamba Kizota (marehemu), David Mwakalebela, Method Mogella (marehemu) Abeid Mziba, Ken Mkapa(captain) na Salum kabunda Ninja(marehemu).

Hii ni picha nzuri ya ukumbusho, na imeugusa moyo wangu! Thanks!
 
Mwenye dvd za huyu jamaa nione ufundi wake ani inbox plz
 
Mogela, alikuwa na uwezo wa kucheza namba zote isipokuwa kipa, l used to love him, nilisikitika sana niliposikia kafa kwa goma
Ulimpima ukathibitisha kuwa alikufa kwa ngoma...tujaribu kuwa considerate hasa kwenye rumours.
 
Hakuna.midfielder mzuri ambaye tanzania imewahi kua nae kama marehem method, kwa sasa unaweza mfananisha na inesta
 
Hakuna.midfielder mzuri ambaye tanzania imewahi kua nae kama marehem method, kwa sasa unaweza mfananisha na inesta

Hussein Marsha,Athuman China,Razack Yusuph...hao wote walikuwa kimeo au? Sikatai kuwa Method alikuwa mzuri lakini usiseme kuwa hakuna kama yeye TZ!
 
Hussein Marsha,Athuman China,Razack Yusuph...hao wote walikuwa kimeo au? Sikatai kuwa Method alikuwa mzuri lakini usiseme kuwa hakuna kama yeye TZ!

Hawakua kimeo ila kwa upande wangu Method was something else kaka,
 
Acha masikhara bhana, kwani we ni mgeni na wabongo kwenye records keeping?

Mkuu kipindi kile tvt walikuwa wanarecord kama sikosei siamini kama hakuna kabisa zitakuwepo sema za ubora hafifu
 
Hussein Marsha,Athuman China,Razack Yusuph...hao wote walikuwa kimeo au? Sikatai kuwa Method alikuwa mzuri lakini usiseme kuwa hakuna kama yeye TZ!
Mkuu hao jamaa walikuwa wazuri lakini sio kwa kiwango cha mogella.
Pia kuna kiungo wa yanga aliitwa steven musa alikuwa kama iniesta.
 
Hapo kwenye nyekundu,hivi ni kweli Thom Kipese aliahamia Yanga akitokea Simba eeeh! mkuu acha utani ukweli alitokea Yanga kwenda Simba. kwa kuongezea, Method alichukuliwa Arusha na Meja Rashid Makame ( marehemu) akamleta JKT Pwani na kisha akampeleka katika timu aliyokuwa akiipenda (Makame) Simba lakini moyoni Method hakuwa na mapenzi na Simba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…