naomba mnisaidie na hii
"hakuna masika yasiyo na mbu"
Mimi sioni kama methali au misemo hii ya kiswahili ina kinzana kwa sababu kila mmoja husemwa au uliasisiwa kutokana na mazingira tofauti, mfano namba 1 hapo juu: Mtaka nyingi nasaba hupata mingi misiba mazingira ya uasisi wake (kwa ufahamu wangu) imelenga katika kumuonya mtu anaetaka kuwa na mahusiano na watu wengi na maana yake ajiandae pia kupatwa na matatizo mengi yatakayotokana na uhusiano huo, lakini Atangae sana na jua hujua, hain uhusiano wa moja kwa moja na ile ya kwanza (y a nasaba), hii imelenga katika kumchagiza mtu asiyechoka katika kutafuta (hasa elimu) kidogo inafanana na "Achumiae juani hulia kivulini" au "Baada ya dhiki Faraja".Ukiangalia ile ya 4 pia, imejengwa katika mazingira ya kuonya pia kuwa mtu anapokatazwa jambo na bado akawa mbishi basi ni heri kumuacha ili ajifunze madhara yake, kwa namna yoyote ile haikinzani na "mchuma janga hula na wakwao" hii ya mchuma janga inaonya jamii kuwa siku zote watu wa kwanza kuathirika na madhara yatokanayo na kutokumuonya mwanajamii mmoja wao ni wanajamii wenyewe; hii inafanana na "Asiye funzwa na mamaye hufunzwa na Ulimwengu" au pia "mkubwa ni jalala kila uchafu hutupiwa yeye" namba Tano inatufunza kuwa "Tusipende kuwa tendea watu jambo tusilopenda sisi wenyewe kutendewa, lakini ile ya upande mwingine "Ukupigao ndi ukufunzao" inatufunza kuwa binadamu hujifunza madhara ya kitu baada ya kumpata ni sawa na "Aisifue mvua imemnyea" na wala hizi hazikinzani.
- mtaka nyingi nasaba hupata mwingi msiba vs atangae sana na jua hujua
- kozi mwana mandanda kulala na njaa kupenda vs za mwizi 40
- ya kale ni dhahabu vs mavi ya kale hayanuki
- mtoto akililia wembe mpe vs mchuma janga hula na wakwao!
- mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu vs ukupigao ndio ukufunzao!
- mchawi mpe mwana alee vs adui yako muombee njaa!
- hakuna marefu yasiyo na mwisho vs elimu ni bahari!
- samaki mkunje ...vs mtoto akililia wembe....
...
- Chelewachelewa utakuta mgeni si wako...