Messi moto; Aweka rekodi mpya UCL

Messi moto; Aweka rekodi mpya UCL

na katika la liga by single season messi ndie anae ongoza ana goals 50 season 2011-2012
 
mkuu SEMBO umeona hapo kwa season ni ronaldo ndiye top score . na nafikiri umeona hapo record aliyoeweka messi top score kwa season 4 mfululizo top score from 2008-2012 hakuna mpaka sasa aliekua kwa mara nne zilizofatana c.ronaldo ni x2 tu sijui mwaka huu umenielewa?

Nimekusoma Mkuu ila bado nasisitiza hii ligi ya CR7 na Messi ni ndefu sana tuvute subira mana pumba na chuya zitajitenga.
 
C.ronanldo itamchukua mda kuzivunja record alizoweka messi na umri wa messi bado ni mdogo
 
Hayo magoli 17 ya ronaldo msimu huo messi alikua majeraha takriban miezi 2 hakua katika gem ndio hapo c.ronaldo akajifaragua
 
We jamaa vipi? Mi nazungumzia magoli aliyofunga CR7 tangu aanze kucheza mpira, na magoli aliyofunga Messi tangu aanze kucheza mpira. Hujaelewa kipi sasa? Au ndo umeamua kubisha tu? Alafu kwani CR7 ameanza kucheza la liga lini? Na Mesi kaanza lini?

tumechoka na habari zenu huyu akija na data hizi huyu anakuja na zile, we umeleta magoli mwingine atasema nani kachukua tuzo nyingi za mwanasoka bora wa dunia
 
Ronaldo amefunga hayo magoli kwa miaka 12, sio 10 kama ulivyosema. Kama Messi hatopata majeruhi ya muda mrefu atakuwa na magoli zaidi ya 300 ya ligi kwani kwake kufunga goli 25 za ligi kwa msimu 1 sio issue. Pia wakati Gaucho na Deco waking'aa Barca, Messi bado hakuwa na play time ya kutosha pale.

Kwa miaka 5 aliyoichezea la liga Ronaldo amefunga magoli zaidi ya nusu ya yale ya Messi ambayo ametumia 10 years
 
Twende mbele turudi nyumabmmCL ni motto! .
 
Kwa miaka 5 aliyoichezea la liga Ronaldo amefunga magoli zaidi ya nusu ya yale ya Messi ambayo ametumia 10 years

Na messi kafunga magoli mengi kushinda cr7 champions league na katika mechi chache zaidi, huku akiwa na penalty chache zaidi
 
Vyovyote iwavyo messi amechuja with just 27. Nawahakikishia CL will be crowned king in January 2015
 
Vyovyote iwavyo messi amechuja with just 27. Nawahakikishia CL will be crowned king in January 2015

Messi amechuja? Are u serious?

Katupia jana 3 katika Ushindi wa 5-1!

CR7 katupia 3 katika ushindi wa 3-0.

Katika mechi Nne au tano za hivi karibuni Messi ana hattrick 3 mfululizo wakati CR7 anazo mbili tena za penalt kiki ndani yake! Lion will still remain as a Lion.
 
aje england tuone hayo magoli

EPL mnapenda sana kui-overate tu wakati hamna kitu.

Mbona alishawapiga Arsenal hat-trick + 1? Mbona alishawapiga Man U kirahisi tu, tena moja ya magoli ilikuwa kwa kichwa mbele ya "watu murefu na yenye mabavu" Rio & Vidic?

Ona Diego Costa anavyosasambua. Ona Aguero anavyonyanyasa - wote hawa walitokea La Liga lakini hawakuwa top scorers kule!

Mfano mwengine ni wa Suarez ambaye juzi juzi tu hapa kwenye EPL alikuwa anapiga magoli kama hana akili sawasawa lakini tangu amekwenda La Liga umemsikia? Au Gareth Bale?

England kuna mibeki iliyojaa mibavu tu lakini brainless. Mchawi Messi akienda pale atakuwa anateleza tu kama kumsukuma mlevi.
 
CR7 bhana goli 200 katika gemu 178 za La Liga. Ana hat trick 23, katulia hana presure. Long Live CR7.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom