Messi moto; Aweka rekodi mpya UCL

kipimo cha uchezaji bora sio magoli tu

messi anacheza mpira kutumia akili nyingi sana

​Wachezaji wote uwanjani wanacheza kwa kutumia akili, sijawahi kumuona mchezaji anayetumia makalio. Tafuta credit nyingine, hii sio.
 
Jamaa aliongea kule juu akamaliza kabisa, sasa hivi ukiwaweka sokoni CR7 na Messi, mabosi wa vilabu vikubwa wote chaguo lao la kwanza litakuwa Ronaldo.
 
"What messi can do, CR7 can do it better"

Kenda haipo mbali na kumi, na tusubiri hiyo J5 pale CR7 atakapoweka rekodi mpya.

Record Gani ambayo Messi ameweka na Ronaldo akavunja, ila uliza Rekod ambazo Messi kaweka na Ronaldo hajavunja.
 
Hawa Cr7 na Messi watakimbizana milele na milele yaani inabidi mmoja wao afe au avunjike mguu ili ligi hii iishe

Haina haja ya kufa, Ronaldo hataweza kufikia Rekod za Messi.
Kwa kumalizia. Messi hashindani na mtu na ameshasema kuwa yeye anacheza mpira kwa manufaa ya Barcelona tuu.
 
​Wachezaji wote uwanjani wanacheza kwa kutumia akili, sijawahi kumuona mchezaji anayetumia makalio. Tafuta credit nyingine, hii sio.

Kuna akili na akili nyingi
Hata ww umetumia akili kupost ila haimanishi una akili nyingi
 
Messi is two years younger than Ronaldo.. Ronaldo kaanza kucheza CL mapema zaidi ya Messi lakini cha kushangaza Messi ndiye anayeongoza.. Tukiweka ushabiki pembeni huyu andunje ni exceptional

Ahsante sana.
 
Jamaa aliongea kule juu akamaliza kabisa, sasa hivi ukiwaweka sokoni CR7 na Messi, mabosi wa vilabu vikubwa wote chaguo lao la kwanza litakuwa Ronaldo.

Huyo boss atakua ana kichaa labda.. Ama atamchukua Ronaldo kwasababu za kibiashara sio mpira..
 
Wachambuzi wa soka wangelikuwa kama wewe tusingelikuwa wasomaji wa makala za soka katu...

Kwa hiyo mchezaji bora ni yule anayefunga magoli mengi ya ligi alizocheza maishani mwake?

Vipi kuhusu assists, magoli katika mechi zote, uwiano wa mechi na magoli, ushindi wa vikombe na medali, msaada kwa timu n.k

Kutokana na dunia kuwa na wachambuzi kama wewe, ndo maana tunafatilia mpira.
 
We mtu? Si ni magoal ya la liga tuu hayo messi aliyofunga kwa misimu na kuvunja rekod ya zarra ya magoal 251, statistically messi kamzidi vibaya kwa magoal ronaldo. La liga 253, uefa 74, argentina....!! Usiongee vitu kama haujui au google

mwambie huyooo!!! hata ku-google kashindwa.
 
Jamaa aliongea kule juu akamaliza kabisa, sasa hivi ukiwaweka sokoni CR7 na Messi, mabosi wa vilabu vikubwa wote chaguo lao la kwanza litakuwa Ronaldo.

No money in the world can suffice ile talent ya messi

Messi is priceless kwa lugha nyingine hanunuliki
 
CR7 kazaliwa 1985 na Messi kazaliwa 1987.

CR7 alianza kucheza 1st team msimu wa 2002/03 Sporting Cp ya ureno akiwa na miaka 17 na Mesi alianza msimu wa 2004/5 pale Barcelona akiwa na miaka 17.

Katika club zote alizopitia CR7 yani Sporting Cp, Man United na Madrid, ametupia jumla ya goli 294 katka miaka 10 ya kucheza soka na Messi katupia goli 253 pale Barcelona katika miaka yake 10 ya kucheza soka.

Hayo magoli waliyofunga ni katka mechi za ligi tu.

Hivyo ukiamua nani mkali kwa kuangalia mwenye goli nyingi CR7 ni superior kwa Messi. Maana ametupia goli za kutosha, alafu alipoteza msimu wa kwanza kwenye timu isiyo na mbele wala nyuma Sporting CP tofauti na Messi aliyekua kazungukwa na Mafundi kama Gaucho na Deco.

NB: Asante Google kwa hizo data.

hv ww una ubongo kweli,kwa kifupi magoli ya ligi ambayo CR 7 anamzidi messi ni tofauti ya muda kila moja alipo anza kucheza.
 
Kuna sehemu moja nilipita nikaona jamaa mmoja anasema CR7 anacheza mpira ili tu ajioneshe yeye ni bora kuliko Messi wakati yeye Messi anacheza kwa mafanikio ya club..

Ronaldo kwenye mechi moja utakuta anapiga mashuti 20 golini ili tu afunge magoli mengi. Kuna sehemu zingine hazitakiwi kupiga shuti badala yake atoe kwa aliye kwenye nafasi nzuri afunge yeye hafanyi hivo. Ndio maana unaona Messi kamzidi assist Ronaldo
 
Endeleeni na siasa zenu lakini msisahau kuangalia game kwenye TV zenu, burudani imehamia Switzerland leo. Los blancos wanampiga mtu nyingi nyumbani kwake leo.

#Hala_Madrid!
 
Ha ha ha ha kweli Mkuu, harafu hana papara kama Ronaldo.

mijitu inayopiga kelele kwanza haingaliiag mechi

wanasubir mechi ichezwe wanunue gazet waangalie stats

ukiangalia stats za lamperd na ronaldinho gaucho automatic utasema lamperd ni zaid ya gaucho but mambo alokuwa anafanya gaucho ground only lord knowz
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom