Kuna siku nipo nasubiri simu ya muhimu, ghafla ikapigwa simu na hao wehu wa mitandao eti nidownload sijui wimbo gani....!!
Kuna siku nipo nasubiri simu ya muhimu, ghafla ikapigwa simu na hao wehu wa mitandao eti nidownload sijui wimbo gani....!!
Kama mimi muda mfupi uliopita wamenipigia kwa namba 0717 124 469. It really annoyed me as I was in the middle of something very important. Nimelazimika kuangalia jina la mtu aliyesajiliwa kwa namba hiyo na kukuta ni FRANK NDUNGURU. Simjui hanijui. Mara tu baada ya kupokea simu nikasikia ujumbe wa promotion.
Hii inanikumbusha kipindi cha uchaguzi mkuu uliopita watu wengi tulipokea sms za kuomba kura kutoka kwa watu tusiowajua huku zikionyesha kabisa kwamba mtuma sms anajua muda huo uko jimbo gani la uchaguzi.
Inawezekana pia wakati wa kujisajili kupata namba za simu kwenye zile form tulizosaini kuna kipengele kinachotutaka sisi wateja kuwa tayari kupokea matangazo ya aina yoyote kutoka kwao. Nasi kwa kutokuwa makini au kutokuwa na option tukawa tunajisainia tu. Katika hali kama hiyo watu wa mitandao wanakuwa wana hakika ya kutushinda hata kama tutawapeleka kwenye vyombo vya sheria na pengine ndiyo sababu pamoja na kelele zetu za muda mrefu hakuna mabadiiko na badala yake kero zinazidi hadi kufikia kutumia hata namba binafsi kama hiyo niliyotaja hapo juu. Tukumbuke hapo siku za nyuma kutuma sms au matangazo ya sauti ya promotion walikuwa wakitumia namba zenye uniqueness fulani hivi.
Otherwise TCRA wasaidie kuondoa hii kero kwani kwa sasa imekua kwa kiwango kikubwa sana.