Sidhani kama kutumia nguvu au vitisho ni suluhisho na pia sio kweli kwamba hizo messages zote zinahusiana na mapenzi. Inawezekana, lakini pia inawezekana tu ni mambo mengine. Ni mambo yasiyopendeza kwani yanatoa kipaumbele kwa mtu au watu wasiostahili? NDIO.
Dawa ni kumfahamisha tu mama kuwa hilo linakukwaza na hulipendi na ungeshauri aliache ili kutoa kipaumbele kwa anayestahili ambaye ni mume. Mkumbushe kuwa hata wewe unaweza kuwa na simu na ukaamua kuendekeza anayoendekeza yeye na una hakika hatapendezewa. Asilopenda kufanyiwa yeye na basi asimfanyie mwingine.
Ni muhimu kumkumbusha wajibu wake kwani sisi binadamu tunahitaji saa zingine kukumbushwa. Usije ukamuachia akapotea ukabaki unasikitika. Anaweza akawa na mazuri mengi kulinganisha na mapungufu hayo ya messages. Pia anaweza tu kuhadaika, hivyo kumuokoa kweli hilo ni wajibu wako. Sidhani kama humpenda kwani usingemuoa au usingehangaika kutaka ushauri, hivyo basi usingependa apotee na kujikuta anahangaika baadae kwa kuhadaika tu.
Ndoa ni kuleana, kukumbushana, kufundishana/kuelimishana, kueleweshana,kusikilizana, kuheshimiana na kupendana.
Utakuwa unatimiza wajibu wako kumkumbusha nani ni muhimu katika ndoa yake. Akichagua hao usiowajua basi, lakini utakuwa umetimiza wajibu wako wa kumkumbusha na pia utakuwa umepigania haki yako ya kujaliwa.
Ndoa ina mitihani mingi mno hivyo nenda taratibu.