Message! Message! imeingia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Message! Message! imeingia

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by NgomaNzito, Mar 10, 2009.

 1. NgomaNzito

  NgomaNzito JF-Expert Member

  #1
  Mar 10, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 561
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nachoka sana na message message kila wakati ni message tu hana muda wa kufanya kitu ni message tu simu kila saa ni mlio wa triiiii!!! message imeingia hata muda wa kufanya jambo lolote hana ni triii message imeingia, ukikaa sekunde tano trii message wakati mwingine zinaingia daboli au mfululizo zinaingia tano sita zinatokea wapi?

  waifu amekuwa busy na message tuuu nifanyaje?

  halafu siku hizi kuna message zinasambazwa zinaelezea ohh wakati wa Mwalimu sijui watu walikuwa wanafanye lakini siku hizi watu wanafanya vibaya zaidi au tofauti yaani nachoka sijui nifanyaje?

  inafikia unaongea nae anashindwa kukujibu sahihi kisa macho yote yapo kwenye kioo cha simu sms tuuu hadi nawaza sijui nikikamate hicho kisimu nikikanyage au nikipasulie mbali lakini naona sio njia muafaka nifanyeje wajameni???
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Mar 10, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,610
  Likes Received: 82,187
  Trophy Points: 280
  Duh! Pole sana. Kaa chini umweleze kutoridhika kwako na hali hiyo na pia mtafute njia jinsi ya kupunguza hizo message. Si ajabu 99% hazina umuhimu wowote.
   
 3. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #3
  Mar 10, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Hiyo ndio mobile generation --
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  Mar 10, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Kaka... abiria chunga mzigo wako, haijawahi tokea mamaa akalose concentration kwa sms za kawaida

  Weka hoja mezani
   
 5. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #5
  Mar 10, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  yawezekana hana kazi ya kufanya?, ndio maana hutumia muda mwingi kukuandikia msg?, kama ni hivyo mtafutie kazi ama biashara. Ama ndio bado mpo katika ile stage ya mwanzo ya kuoana, mambo bado mteremko.
   
 6. Y

  Yassin JF-Expert Member

  #6
  Mar 10, 2009
  Joined: Jul 23, 2008
  Messages: 326
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mkuu mimi nadhani wewe kama kweli huyo mke wako basi chukua hiyo simu yake hata kama ukiona messeg zinaingia chukua simu angalia nini kinachoendelea sasa wewe unaona mke wako messeg zinaingia kama hivyo alafu unamuangalia tu???Kama mpenzi wako huna budi kuuliza hapa JF ila kama wife wako chukua simu angalia nini kinaendelea kama hamna kitu cha maana basi chukua hiyo line tupa mpe namba nyingine usicheke na mke wako kupita kiasi atakuletea mwanamme nyumbani kwako!!!...Maoni yangu ni hayo tu!!
   
 7. A

  Audax JF-Expert Member

  #7
  Mar 10, 2009
  Joined: Mar 4, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ndugu yangu huyo ni mke wako na kwenye ndoa cha kwanza ni piece ofmind,nadhani huna raha ya kuwa naye hata akiwa hasomi message.Ni kitendo cha kusoma hizo message maana waswahili walisema samaki mkunje angali mbichi!!
   
 8. N

  Neemah Member

  #8
  Mar 10, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo, ndugu, sio message. Tatizo limo ndani ya mwenza wako -- ana-respond to stimuli. Kwahiyo, hata ukimnyang'anya au kumtafutia kazi ya kufanya, kama walivyoshauri wengine, hautakuwa ufumbuzi.

  Kwa mfano, tuchukulie huna mtandao nyumbani. Leo umemnyang'anya simu, kesho, keshokutwa unaunganisha mtandao nyumbani. Kama umemshindwa ktk simu, kweli utamweza ktk huo mtandao? Jaribu kumuuliza vitu gani kwake anaona ni vipaumbele kwake. Hapo utaweza kujua ni mtu mwenye kupenda anasa au mtu anayependa maendeleo. Na hapo utakuwa na mwanzo mzuri wa kujua hatua inayofuata.
   
 9. Penny

  Penny JF-Expert Member

  #9
  Mar 10, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 577
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Pole kaka, tena unaonekana wewe ni mlokole kama sijakosea kutokana na ID yako hapo juu. Pengine nikuulize, mna mda gani katika ndoa na ulishawahi kumuuliza hizo message zina husu nini, na jibu lililikuwaje? Vipi na maelewano yenu kila mmoja anauwezo wakuwa free na simu ya mwenzie! Baada ya hapa then tutaendelea...
   
 10. S

  Sahiba JF-Expert Member

  #10
  Mar 10, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu inabidi muwe na nidhamu maana inaonekana imepotea nyumbani kwako.Inaonekana unataka attention ambayo ni haki yako unaporudi nyumbani na mwenzako hakupi hiyo attention kwa kuwa aidha hajui kama anakuudhi,vilevile ni upeo wake mdogo wa kufikiri ama bado ni tabia zake za kitoto kwa kuwa ni dhahiri wewe ukitumia muda mwingi katika hizo sms yeye atalalamika hivyo unatakiwa umueleze kwa taratibu,mkubaliane kuwa hakuna mobile baada ya saa fulani then mtaanzia hapo.


  SAHIBA.
   
 11. Violet

  Violet Member

  #11
  Mar 10, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwenye ndoa ni muhimu sana kuwa open kuzungumzia chochote, usiweke vitu moyoni, hivyo zumgumza naye tuu. Lugha utakayo tumia kumuuliza ni muhimu pia.
   
 12. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #12
  Mar 10, 2009
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Usiwe na hofu ila chunguza kwa makini,kama ulivyo sema msg nyingi ni zile "oh enzi za mwl ilikuwa hivi na vile lakini sikuhizi....wizi mtupu".
  Hizi zita isha kama promo ya sms zitaisha/sitishwa kwenye makampuni yanayotoa huduma hiyo kwani sasahivi ukiwa na 500/= utatuma sms siku nzima.
  Hii ina wafanya wengine watumie muda mwingi kutuma sms hizo ili 'kufidia'gharama zake hivyo wanaopokea nao ni wengi.
  Binafsi nimekua napoke sms nyingi za namna hiyo na hazina ujumbe wowote wa maana zaidi ya hayo na jokes.Kibaya zaidi unaweza kupokea msg 1 zaidi ya mara 10 kutoka kwa watu tofauti sababu ya copy n paste wanazo fanya.
  Inasikitisha kuna siku nimeshindwa kujibu sms muhimu kwa muda kwa sababu siku hiyo nilipokea sms nyingi za upuuzi huo,hata ilipoingia hiyo sikuisoma nikijua ndio zile zile..
  Mwambie mkeo hupendi hali hiyo na awaambie wanaomtumia sms hizo waache kufanya hivyo kwani hata mlio wa ku alert kuwa sms imeingia nao ni kero
   
 13. m

  mchamba wima Member

  #13
  Mar 11, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mkubwa wala hata usisumbuke huyo penzi lishachuja au kuna wenzio wanamega ,mjini hapa magoli ya off side siku hizi ndio ushindi wenyewe,we lemaa tu mwenzio anakupetea nje ya kumi na nane huwajui wanawake wewe shauri lako,hata hivyo kila la heri katika kusolve msala wako huo .
   
 14. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #14
  Mar 11, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...wala usikereke ndugu yangu, mu ignore tu japo unakufa na tai shingoni, tafuta jambo la kuku keep busy nawewe mpaka huo mzuka wake utapotulia...!

  ...kumnyang'anya hicho kilonga longa wala sio suluhisho la kudumu.
   
 15. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #15
  Mar 11, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,610
  Likes Received: 82,187
  Trophy Points: 280
  Hmmm Mbu..Tabia ya kufa na tai shingoni kwa mke wako wala haifai. Utajifanya hayakukeri kumbe moyo unaumia na ukizidi kuchelewachelewa utakuta mtoto si wako. Huyu mwenztu mpaka kuja hapa jamvini kuomba msaada afanye nini ili kuzuia hili jambo basi ujue lmeshamfika shingoni. Cha muhimu ni kukaa na mkewe kwanza kujua kama hizo jumbe hazihatarishi ndoa yao na kisha kutafuta namna na kuzipunguza au kuzisimamisha kabisa. Kama hizo jumbe zinahatarisha ndoa yao basi hapo tena wana tatizo kubwa sana ambalo labda litahitaji msaada zaidi ili kulitatua.
   
 16. Iteitei Lya Kitee

  Iteitei Lya Kitee JF-Expert Member

  #16
  Mar 11, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 589
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Angalia FATAKI asije kua ashampitia hivyo hasikii wala haoni.Mchunguze taratibu kisha muulize usikie atasemaje.Then mweleze unavyoboeka na hizo message zake.
   
 17. kimatire

  kimatire JF-Expert Member

  #17
  Mar 11, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 365
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mkuu elewa teke lililotujia linatumaliza wengi na hakuna masika yasiyokuwa na Mbu.Pls kaa mkao wa kuondokewa na huyo mwenzi wako.Hakika kuna kila dalili za ufedhuli hata huhitaji kwenda mbali sana kuliona hilo.Kama siyo mashoga, basi ni wadau wenzio wako kazini.
   
 18. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #18
  Mar 11, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Wadau...
  Kwa kweli hata mimi napata shida sana kutokana na Message za kipuuzi haswa kutoka kwa wateja wa kampuni moja ya simu za mikononi ambayo wakati mwingine inapunguza bei ya kutuma SMS kufikia hadi 250/-kwa siku yaani kuanzia alfajiri mpaka usiku wa saa 6...kampuni hiyo pia ina tabia ya kutuma SMS ambazo hazina...kichwa wala miguu mara jishindie Ipod mara pata maneno matamu ya kumwambia mpenziyo... What ze hell!!!!
  Mdau...
  Tusker Bariiiidi!!!
   
 19. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #19
  Mar 11, 2009
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Nashauri siku moja umtie makofi atatia akili. Uliona wapi mtu anakosa concentration na mumewe kisa message? Utandawazi umetufanya kuwa wajinga somehow. Una mume pia anaamka anaenda ****** kusoma message, hivi kweli hata huyo mtu unayefanya nae hivyo unafikiri atakuheshimu hata siku moja?

  Unaruhusu mpuuzi mmoja kuleta mtafaruku kwenye ndoa yako bila sababu. Kama kweli anakupenda si akuoe uache usumbufu kwa mwenzio.

  Huyo mwanamke siyo wa kuchekea mhabarishe akileta longo longo mpe vibao.
   
 20. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #20
  Mar 11, 2009
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Halafu hizi message za enzi za mwalimu nilishapiga marufuku mtu kunitumia, ule nao ni ujinga mtu mzima unakaa chini kusambaza message za kipuuzi. Unateketeza hela pasipo sababu.
   
Loading...