Message inayo hatarisha mahusiano yangu

Message inayo hatarisha mahusiano yangu

Stamina

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2012
Posts
1,040
Reaction score
589
Habari zenu wana mmu.

Wandugu hizi simu ni nzuri sana kwasababu zina turahisishia mawasiliano ukilinganisha na zama zile za barua.

Lakini simu hizi hizi ziki kugeukia utaziona chungu, hasa kwenye suala la mahusiano.

Nimeandika yote hayo hasa baada ya kilichonitokea mimi jana jioni , (ingawa nilikuwa Nasikia tu kwa wengine jinsi simu zilivyovunja ndoa na mahusiano yao)

Jana jioni majira ya saa kumi jioni, nilitoka na mpenzi wangu kwenda kujivinjari maeneo ya kigamboni, mji mwema, kwenye fukwe tulivu za kipepeo beach, mbali na makelele na stress za jiji la Dar es salaam.

Sasa tukiwa huko tunapata vinywaji na vilaji, mpenzi wangu alichukua simu yangu akawa anaiangalia, kwakuwa sina tabia ya kuficha wala kulock simu basi nikamwachia aiangalie.

Wakati anaiangalia-angalia simu yangu, mara message ikaingia, nikaona kabadirika sura ghafla, nilipomuuliza hakunijibu nikaamua kuichukua simu na kuangalia hiyo sms ni ya nani?

Nilipoisoma iliandikwa hivi "mambo baby, vipi uko poa,?! Jana tulipoacha pale Ulifika salama baby? Basi baby, leo jioni tukutane annex bwana , pale pa jana sikupapenda makelele mengi? Sawa baby?
Nilishtuka sana maana kusema ukweli sina mchepuko nje, nikajaribu kumuelewesha mpenzi wangu, kuwa hiyo sms imekosewa lakin hakutaka kuelewe wala nini?

Kukata mzizi wa fitina nikaamua kumpigia simu huyo dada mbele ya mpenz wangu tena nikaweka loud speaker ili naye asikie, sasa yule dada aliyetuma sms akapokea simu alipogundua amekosea sms sijui ni uoga au vipi , akakata simu then akazima kabisa ikawa haipatikani tena.

Sasa akaniachia mzozo na mpenz wangu, najaribu kumwelewesha lakin hataki amenuna, hata kupokea simu yangu hataki na kujibu sms zangu hataki, wakati kusema ukweli kabisa ile sms ilitumwa kimakosa.

Sasa wadau naombeni ushauri nifanyeje ili apate kuniamini.
 
Nilitaka kusema ,it is none of our business lakini basi! Ngoja waje
 
Kabla sijasema meeengi ngoja nukuambiae kitu

Hebu "vaa viatu vyake" halafu uone utafanya nini,sitaki ujipendelee bali kuwa mkweli kwa nafsi yako na uone kila ambacho ungefanya .....

Baada ya hapo jiulize kama una haki ya kumlaumu .....!!
 
Siku hizi hapa JF hili jibu la NONE OF OUR/MY BUSSINES LIMEKUWA MAARUFU SANA... Haya niambieni vitu gani ndo vitawahusu... Ulitegemea MMU ukutane na topiki za aina gani..??

Asante kwa kuliona hili, siku hizi imekuwa kama fashion sasa sijui nini maana ya jukwaa la mmu?
 
Kabla sijasema meeengi ngoja nukuambiae kitu

Hebu "vaa viatu vyake" halafu uone utafanya nini,sitaki ujipendelee bali kuwa mkweli kwa nafsi yako na uone kila ambacho ungefanya .....

Baada ya hapo jiulize kama una haki ya kumlaumu .....!!

Ni kweli hata mimi ningeumia,

Lakin ningejitahidi sana kutafuta ukweli,
Sasa tatizo yeye hataki tuzungumze, hapokei simu zangu wala hajibu sms zangu,

Lakin simlaumu , nampa muda hasira ziishe naamin huenda anaweza kutafakari na kutambua ukweli uko wapi,
 
haki ya Mungu wakati nasoma nkajua mwenye thread hii ni mwanamke!! nkawa najiulza sasa kashapigiwa kakutwa dada!! kuna mzozo gan tena?? mweh! umekosea, alivyokasirika ungemuhamishia kijiji beach! hasira zote zingemwisha....
 
Achana nao wanaoshauri kama hawataki,endelea kumbembeleza atakubaliana na ww
 
Pole mkuu kama hataki kukuelewa nawe pumzika Fanya mambo yako atajifikiria then atakuomba msamaha!
 
naona umemjibu kwa level yake

Kum judge mtu level yake kwa kuleta topic fulan hapa jf sidhani kama ni njia sahihi

Sijui level yako lakin pia sijui kama unaijua level yangu mkuu, pengine hata nimekuzidi, unless tulikuwa wote pale hall 7,

Lakin Asante kwa ku- criticise, i take it as a challenge,
 
Mapenzi kubembelezana
Mbembeleze weee atakuelewa as long as she loves you!!!
 
Jamani mi nashauri tujitaahidi kutoa comment zenye kujenga na ushauri ulio makini ,sidhani kama mtu asiyekuwa na akili zake timamu anaweza kujiunga na JF, hivyo basi kejel na majibu ya kukatisha tamaa iwe ni marufuku!!!!!
Ushauri wangu; jitahidi kumuelewesha atakuelewa, pia unaweza kumtafuta huyo dada aliyekosea hata kwa namba tofauti na hiyo aliotumia kutuma txt kwako then mueleze alivyokusababishia matatizo na umpatie namba ya mpenzi wako amfahamishe kuwa hakukusudia kutuma hiyo msg kwako.. nafikiri it can work. thanks.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom