haki ya Mungu wakati nasoma nkajua mwenye thread hii ni mwanamke!! nkawa najiulza sasa kashapigiwa kakutwa dada!! kuna mzozo gan tena?? mweh! umekosea, alivyokasirika ungemuhamishia kijiji beach! hasira zote zingemwisha....
Kum judge mtu level yake kwa kuleta topic fulan hapa jf sidhani kama ni njia sahihi
Sijui level yako lakin pia sijui kama unaijua level yangu mkuu, pengine hata nimekuzidi, unless tulikuwa wote pale hall 7,
Lakin Asante kwa ku- criticise, i take it as a challenge,
Km umeumia sana na unadhani bila yeye maisha yako hayana thamani tena,me nakushauri bora UJIUE! Lkn km unafikiri vizuri na ukweli unaujua kwamba jambo hilo si la kweli,wala huhitaji kuwaza sana,kubali kilichotokea na kubali uamuzi wake kukutolea yy nje siyo mwisho wa maisha yako. Kwani ungesikia amekufa na wewe ungekufa!??Habari zenu wana mmu.
Wandugu hizi simu ni nzuri sana kwasababu zina turahisishia mawasiliano ukilinganisha na zama zile za barua.
Lakini simu hizi hizi ziki kugeukia utaziona chungu, hasa kwenye suala la mahusiano.
Nimeandika yote hayo hasa baada ya kilichonitokea mimi jana jioni , (ingawa nilikuwa Nasikia tu kwa wengine jinsi simu zilivyovunja ndoa na mahusiano yao)
Jana jioni majira ya saa kumi jioni, nilitoka na mpenzi wangu kwenda kujivinjari maeneo ya kigamboni, mji mwema, kwenye fukwe tulivu za kipepeo beach, mbali na makelele na stress za jiji la dar es salaam.
Sasa tukiwa huko tunapata vinywaji na vilaji, mpenzi wangu alichukua simu yangu akawa anaiangalia, kwakuwa sina tabia ya kuficha wala kulock simu basi nikamwachia aiangalie.
Wakati anaiangalia-angalia simu yangu, mara message ikaingia, nikaona kabadirika sura ghafla, nilipomuuliza hakunijibu nikaamua kuichukua simu na kuangalia hiyo sms ni ya nani?!
Nilipoisoma iliandikwa hivi "mambo baby, vipi uko poa,?! Jana tulipoacha pale Ulifika salama baby? Basi baby, leo jioni tukutane annex bwana , pale pa jana sikupapenda makelele mengi? Sawa baby?"
Nilishtuka sana maana kusema ukweli sina mchepuko nje, nikajaribu kumuelewesha mpenzi wangu, kuwa hiyo sms imekosewa lakin hakutaka kuelewe wala nini?
Kukata mzizi wa fitina nikaamua kumpigia simu huyo dada mbele ya mpenz wangu tena nikaweka loud speaker ili naye asikie, sasa yule dada aliyetuma sms akapokea simu alipogundua amekosea sms sijui ni uoga au vipi , akakata simu then akazima kabisa ikawa haipatikani tena.
Sasa akaniachia mzozo na mpenz wangu, najaribu kumwelewesha lakin hataki amenuna, hata kupokea simu yangu hataki na kujibu sms zangu hataki, wakati kusema ukweli kabisa ile sms ilitumwa kimakosa.
Sasa wadau naombeni ushauri nifanyeje ili apate kuniamini.
Jamani mi nashauri tujitaahidi kutoa comment zenye kujenga na ushauri ulio makini ,sidhani kama mtu asiyekuwa na akili zake timamu anaweza kujiunga na JF, hivyo basi kejel na majibu ya kukatisha tamaa iwe ni marufuku!!!!!
Ushauri wangu; jitahidi kumuelewesha atakuelewa, pia unaweza kumtafuta huyo dada aliyekosea hata kwa namba tofauti na hiyo aliotumia kutuma txt kwako then mueleze alivyokusababishia matatizo na umpatie namba ya mpenzi wako amfahamishe kuwa hakukusudia kutuma hiyo msg kwako.. nafikiri it can work. thanks.
Km umeumia sana na unadhani bila yeye maisha yako hayana thamani tena,me nakushauri bora UJIUE! Lkn km unafikiri vizuri na ukweli unaujua kwamba jambo hilo si la kweli,wala huhitaji kuwaza sana,kubali kilichotokea na kubali uamuzi wake kukutolea yy nje siyo mwisho wa maisha yako. Kwani ungesikia amekufa na wewe ungekufa!??
Hivi haya matumizi ya "X" badala ya "S" yanawasaidia nini?
Kum judge mtu level yake kwa kuleta topic fulan hapa jf sidhani kama ni njia sahihi
Sijui level yako lakin pia sijui kama unaijua level yangu mkuu, pengine hata nimekuzidi, unless tulikuwa wote pale hall 7,
Lakin Asante kwa ku- criticise, i take it as a challenge,
Baxi xawa tumekuxikia
Hahahaaaaa nlijua ni pekeangu ndio sipendi ayo matumiz ya s kua x........mkuu Nmeweka lakin ditumiagi nmeona mleta maada nikimuandikia kawaida hataelewa
sielewagi mnatoka wapi kuzoea simu ya mpenzio unaanzaje haya ni mazoea ya kijinga sana nayapinga kabisa.... kuweni na mipaka hivi ni vifaa lolote laweza tokea hata mpenzio wa zamani anaweza kukumbuka ikatleta balaa nani atayekubali ni siku hiyo kakukumbuka.. acheni kujidnganya kuwaachia wapenzi wenu simu free ndiyo dawa ya kuuwa mzizi wa fitina .... muhimu muwe na mipaka yeye anasimu yake achezee yake .. unashika simu yangu kuna kitu umesahahu hapo au unadhani mimi sitafutwi? omba kama unahitaji nikutafutie lazima tuwe na mipaka nasisitiza...
Ushauri mzuri sana huu,
Wenzio tunafanya hivyo kujenga kuaminiana, maana ukimzuia pia asiishike atakuwa na mashaka na wewe,
Lakin ushauri wako mzuri sana, kuondoa sintofahamu yoyote ni vyema kuepuka mambo kama haya!
Nina wax wax na iq yako
Kawaida kwanini nisielewe mkuu,
Mara nyingi matumizi ya herufi hizo hutumiwa na form two au ordinary level, wenyewe wanaita swagga. Hasa big results now,
Sasa kwa level yangu ya chuo kuniandikia hivyo nikama kunitusi mkuu, ndio maana ile comment yako niliipotezea tu.