Message inayo hatarisha mahusiano yangu

Message inayo hatarisha mahusiano yangu

hakuna haja ya kumtafuta kabisa,,,,, we mbembeleze mahabuba wako atatulia tuu..... ana test uwezo wako wa kumrudisha kwenywe mood.... usichoke mkuu..

Thanks bro,
Nitajitahidi kadri ya uwezo wangu!
 
Mi nikiwaga yunk nilitumiwaga sms na mpnz wang akijifanya ni Ex Wang et tukutane kwa bahati nzuri nikashtukia Nikambwaga Mapemaa... Akimwaga mbogj we Mwaga Mpunga
 
Best mie ilishatokea ya style hiyo ..Bahati nzuri mie nilikuwa Bara ile meseji ilikuwa inaonyesha mtu na mbebi wake wakutate Zenji
kameseji kalikuwa kanasema

Baby your so darling i cant wait to hold youuuu in ma arms again
natamani masaa yakimbie ili tukutane ..
Mwisho kabisa ikasema leo nimechukua sehemu nzuri na tulivu hapa maeneo ya Nungwi
Duuh !

Penye ukweli uongo hujitenga atakuelewa tu
 
Siku hizi hapa JF hili jibu la NONE OF OUR/MY BUSSINES LIMEKUWA MAARUFU SANA... Haya niambieni vitu gani ndo vitawahusu... Ulitegemea MMU ukutane na topiki za aina gani..??
usihangaike na wagonjwa wa kukariri sikiliza kutoka kwa wenye fikra pevu.
 
hamna lolote mbona haikukosewa ikaenda kwa mkeo ikaja kwako tuu?





Habari zenu wana mmu.

Wandugu hizi simu ni nzuri sana kwasababu zina turahisishia mawasiliano ukilinganisha na zama zile za barua.

Lakini simu hizi hizi ziki kugeukia utaziona chungu, hasa kwenye suala la mahusiano.

Nimeandika yote hayo hasa baada ya kilichonitokea mimi jana jioni , (ingawa nilikuwa Nasikia tu kwa wengine jinsi simu zilivyovunja ndoa na mahusiano yao)

Jana jioni majira ya saa kumi jioni, nilitoka na mpenzi wangu kwenda kujivinjari maeneo ya kigamboni, mji mwema, kwenye fukwe tulivu za kipepeo beach, mbali na makelele na stress za jiji la Dar es salaam.

Sasa tukiwa huko tunapata vinywaji na vilaji, mpenzi wangu alichukua simu yangu akawa anaiangalia, kwakuwa sina tabia ya kuficha wala kulock simu basi nikamwachia aiangalie.

Wakati anaiangalia-angalia simu yangu, mara message ikaingia, nikaona kabadirika sura ghafla, nilipomuuliza hakunijibu nikaamua kuichukua simu na kuangalia hiyo sms ni ya nani?

Nilipoisoma iliandikwa hivi "mambo baby, vipi uko poa,?! Jana tulipoacha pale Ulifika salama baby? Basi baby, leo jioni tukutane annex bwana , pale pa jana sikupapenda makelele mengi? Sawa baby?
Nilishtuka sana maana kusema ukweli sina mchepuko nje, nikajaribu kumuelewesha mpenzi wangu, kuwa hiyo sms imekosewa lakin hakutaka kuelewe wala nini?

Kukata mzizi wa fitina nikaamua kumpigia simu huyo dada mbele ya mpenz wangu tena nikaweka loud speaker ili naye asikie, sasa yule dada aliyetuma sms akapokea simu alipogundua amekosea sms sijui ni uoga au vipi , akakata simu then akazima kabisa ikawa haipatikani tena.

Sasa akaniachia mzozo na mpenz wangu, najaribu kumwelewesha lakin hataki amenuna, hata kupokea simu yangu hataki na kujibu sms zangu hataki, wakati kusema ukweli kabisa ile sms ilitumwa kimakosa.

Sasa wadau naombeni ushauri nifanyeje ili apate kuniamini.
 
Ni haki yake kukasirika na kazi yako ni kumuelimisha mpaka akubaliane na unalomwambia,si rahisi kwake kukubali kuwa huchepuki hata ungekuwa wewe ndio umekuta msg kwenye simu yake usingekubali kirahisi eti hachepuki.
Cha msingi ni kujenga uaminifu kwa mwenzi wako na ukiona mamboyanazidi kuwa magumu kwako basi tafuta ndugu,jamaa na hata marafiki wa karibu ili kutafuta muafaka katika kunusuru mapenzi yenu.
Pole sana kwa lililokukuta na ni moja ya majaribu ya mwanadamu ambayo anayapitia na kila mtu anayapitia ingawa kwa njia tofauti.
 
Acha kuleta za mapenzi ya kwenye TAMTHILIA......Kama kweli anakuamini na mnaaminiana msingefika huko....yani ungemueleza na yeye angepiga mhesabu ya jana ulikuwa wapi.....then namba angeichukua yeye kama anamashaka mawewe ungeonyesha hauna wasiwasi .....sasa wewe unaonekana ulileta mcheheto sana....harafu inaonekana wewe ni mtu wakubembelezabembeleza saaaanaaaaaa....Ushauri wewe ni MWANAUME ongea na mtuwake yoyote wakaribu na huyo mazi muelezee then utakuwa umemaliza......ASIPORUDI UJUE TAYARI HUYO....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom