Message inayo hatarisha mahusiano yangu

Message inayo hatarisha mahusiano yangu

kama anakupenda kweli atakuelewa..endelea kumwelewesha..
akiwa mgumu kuelewa, keep quet for a while..then atakutafuta mwenyewe..
 
pole sana,,, hizo ni ajali kazini...ingekua alishawahi kukufuma ukimsaliti ningesema za mwizi zimetimia ila kwa maelezo yako unaonekana wazi huna kosa bali hiyo hutokea kukosewa sms hata mtu ku wrong number jaribu kumwelewesha mtaftie watu wamshushe hasira zake ila anadeka huyoo,,,,,
 
Mimi hapo ndo relationships zinanitoa kamasi unakuwa mtu wa kutoa maelezo kila wakat utafikiri upo central police umekamatwa na mkono wa albino!? Mimi hapo simbembelezi wala simuelezi zaidi nafunga vioo tu manake sio kila kitu kina maelezo ya kutosha,F.uck love
 
acha kutudanyanga!huyo ni mchepuko wako tuu sema hauku balance mambo sawa
 
Kama umemueleza vizuri na unajua hauna hatia katika hilo mpe muda kuwa busy na mambo yako act a as a man timiza majukumu yako kama kawaida .Atajirudi tu mwenyewe
 
Jamani mi nashauri tujitaahidi kutoa comment zenye kujenga na ushauri ulio makini ,sidhani kama mtu asiyekuwa na akili zake timamu anaweza kujiunga na JF, hivyo basi kejel na majibu ya kukatisha tamaa iwe ni marufuku!!!!!
Ushauri wangu; jitahidi kumuelewesha atakuelewa, pia unaweza kumtafuta huyo dada aliyekosea hata kwa namba tofauti na hiyo aliotumia kutuma txt kwako then mueleze alivyokusababishia matatizo na umpatie namba ya mpenzi wako amfahamishe kuwa hakukusudia kutuma hiyo msg kwako.. nafikiri it can work. thanks.

hakuna haja ya kumtafuta kabisa,,,,, we mbembeleze mahabuba wako atatulia tuu..... ana test uwezo wako wa kumrudisha kwenywe mood.... usichoke mkuu..
 
Jamani mi nashauri tujitaahidi kutoa comment zenye kujenga na ushauri ulio makini ,sidhani kama mtu asiyekuwa na akili zake timamu anaweza kujiunga na JF, hivyo basi kejel na majibu ya kukatisha tamaa iwe ni marufuku!!!!!
Ushauri wangu; jitahidi kumuelewesha atakuelewa, pia unaweza kumtafuta huyo dada aliyekosea hata kwa namba tofauti na hiyo aliotumia kutuma txt kwako then mueleze alivyokusababishia matatizo na umpatie namba ya mpenzi wako amfahamishe kuwa hakukusudia kutuma hiyo msg kwako.. nafikiri it can work. thanks.

Bora umesema ndugu..... kama huna cha kumshauri soma alafu upite si lazima ujibu
Nae yamemkuta ni vibaya kuomba ushauri jaman ..... daaa watu.....

Kaka mtoa mada pole kwa kilichokusibu ..... naamini ni hasira tuuuu ziikiisha ataelewa tuuu..... kuwa mvumilivu usichoke ht mtafuta ..... hayo tuuu
 
Kabla sijasema meeengi ngoja nukuambiae kitu

Hebu "vaa viatu vyake" halafu uone utafanya nini,sitaki ujipendelee bali kuwa mkweli kwa nafsi yako na uone kila ambacho ungefanya .....

Baada ya hapo jiulize kama una haki ya kumlaumu .....!!

Yaaan huyo dada angebutuliwa angechakaa dk 0 tu
 
Habari zenu wana mmu.

Wandugu hizi simu ni nzuri sana kwasababu zina turahisishia mawasiliano ukilinganisha na zama zile za barua.

Lakini simu hizi hizi ziki kugeukia utaziona chungu, hasa kwenye suala la mahusiano.

Nimeandika yote hayo hasa baada ya kilichonitokea mimi jana jioni , (ingawa nilikuwa Nasikia tu kwa wengine jinsi simu zilivyovunja ndoa na mahusiano yao)

Jana jioni majira ya saa kumi jioni, nilitoka na mpenzi wangu kwenda kujivinjari maeneo ya kigamboni, mji mwema, kwenye fukwe tulivu za kipepeo beach, mbali na makelele na stress za jiji la Dar es salaam.

Sasa tukiwa huko tunapata vinywaji na vilaji, mpenzi wangu alichukua simu yangu akawa anaiangalia, kwakuwa sina tabia ya kuficha wala kulock simu basi nikamwachia aiangalie.

Wakati anaiangalia-angalia simu yangu, mara message ikaingia, nikaona kabadirika sura ghafla, nilipomuuliza hakunijibu nikaamua kuichukua simu na kuangalia hiyo sms ni ya nani?

Nilipoisoma iliandikwa hivi "mambo baby, vipi uko poa,?! Jana tulipoacha pale Ulifika salama baby? Basi baby, leo jioni tukutane annex bwana , pale pa jana sikupapenda makelele mengi? Sawa baby?
Nilishtuka sana maana kusema ukweli sina mchepuko nje, nikajaribu kumuelewesha mpenzi wangu, kuwa hiyo sms imekosewa lakin hakutaka kuelewe wala nini?

Kukata mzizi wa fitina nikaamua kumpigia simu huyo dada mbele ya mpenz wangu tena nikaweka loud speaker ili naye asikie, sasa yule dada aliyetuma sms akapokea simu alipogundua amekosea sms sijui ni uoga au vipi , akakata simu then akazima kabisa ikawa haipatikani tena.

Sasa akaniachia mzozo na mpenz wangu, najaribu kumwelewesha lakin hataki amenuna, hata kupokea simu yangu hataki na kujibu sms zangu hataki, wakati kusema ukweli kabisa ile sms ilitumwa kimakosa.

Sasa wadau naombeni ushauri nifanyeje ili apate kuniamini.

Mpe namba ya aliyekutumia waongeeeee watukananeeeeee wasutaneeee then baadae ukimwambia mambo vipi atakujibu fresh
 
mimi namuelewa sana mpenzi wako ila mapenzi ni kusameheana kama anakuwa mgumu sana kuelewa ujue ana matatizo kidogo na kama unategemea kumuoa itabidi ujitahidi kum mould awe sawa ili usipate shida kwenye ndoa
 
Kaka Stamina kwa nionavyo mimi huo ni mchezo umefanyiwa kutokana na mazingira mpaka hiyo sms ikaingia na uundwaji wa meseji yenyewe. Hapo atakua alimwomba mtu atengeneze sms kama iyo ili aje kuituma baada ya yeye kuwa na simu yako,lengo linaweza kuwa ni kutaka kujua tofauti ya response yako kwenye matukio au vitu vya uongo na vilivyo na ukweli au anafanya utukutu nje ili ukija usikie uhisi labda analipiza kisasi. Nimesema ivo cos hata sms inaweza thibitisha,haiwezekani mpenzi wako muachane usiku aje kukuuliza eti ulifika salama jana.duuu
 
Mpe namba ya aliyekutumia waongeeeee watukananeeeeee wasutaneeee then baadae ukimwambia mambo vipi atakujibu fresh

Haaa! Haaa! haaaa!

Nimecheka sana, u made myday be Nice!

You are verry funny indeed,
 
mimi namuelewa sana mpenzi wako ila mapenzi ni kusameheana kama anakuwa mgumu sana kuelewa ujue ana matatizo kidogo na kama unategemea kumuoa itabidi ujitahidi kum mould awe sawa ili usipate shida kwenye ndoa

Asante, nitafanyia kazi hili..!
 
Kaka Stamina kwa nionavyo mimi huo ni mchezo umefanyiwa kutokana na mazingira mpaka hiyo sms ikaingia na uundwaji wa meseji yenyewe. Hapo atakua alimwomba mtu atengeneze sms kama iyo ili aje kuituma baada ya yeye kuwa na simu yako,lengo linaweza kuwa ni kutaka kujua tofauti ya response yako kwenye matukio au vitu vya uongo na vilivyo na ukweli au anafanya utukutu nje ili ukija usikie uhisi labda analipiza kisasi. Nimesema ivo cos hata sms inaweza thibitisha,haiwezekani mpenzi wako muachane usiku aje kukuuliza eti ulifika salama jana.duuu

Inawezekana pia, lakin nitachunguza pole pole nijue ukweli. Nitaongea nae taratibu tu nijue ukweli uko wapi,
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom