Mkuu umejibu vizuri, hakuna wakati unaoenda kuwa mgumu kama baada ya uchaguzi,
1. Kama CCM watapita, watatka kurudisha gharama za uchaguzi ambazo zimekuwa mara 3 zaidi ya kipindi kingine chote cha uchaguzi, miradi ya wachina itaongezeka mjini hapa maana familia kuu itaendelea kushika hatamu kwenye hizi biashara. Sina uhakika kama kweli Magu anaweza kuzuia chochote, ukute na yeye ataingia huko kama watangulizi wake.
2. Kama upinzani utapita, kuna kurudisha gharama za uchaguzi, hapa ni kwa Lowassa na marafiki zake (anaosema ndo wanamdhamini), kuna kutaka kurudisha deal alizonyanganywa na Familia ya Mkuu kupitia kwa Rizimoko baada ya kuondolewa kwenye system, marafiki zake watataka nao wapate tenda mbali mbali ikiwamo kujineemesha na hii rasilimali mpya (gas) ambayo inatutoa macho, lakini pia watu kama Mbowe watakuwa kwenye system na tutaanza kuona nyota nyota sasa.
Mimi kwa utabiri wangu naiona miaka mitano ya ukame Tanzania kwa yeyote atakayeingia madarakani, kodi zitaongezeka, bei za vitu zitapanda, hela yetu itaendelea kushuka thamani, ajira zitakuwa ngumu, na mengineyo.
So, tujipange.