Mkuu una haki ya kunilaumu, CCM wamenifanya Zombie, na kuna kila dalili za kuendelea kunifanya Zombie, kwa sababu, this time ni either uchague CCM Mama (ambayo ndiyo iliyotufikisha kwenye huu umaskini) au CCM Branch (UKAWA) ambayo mgombea wake na baadhi ya wafuasi wake wamemeguka kutoka CCM Mama na wameshiriki moja kwa moja katika kutufikisha hapa.
Uamuzi ni wako.
Ni kweli CCM kanifanyia ufirauni, lakini je huyu Lowassa, Mwapachu, Masha na Sumaye si ni moja ya member wa CCM iliyonifanyia uhuni? Atawezaje kuacha kuendelea kunifanyia uhuni wakati ameshaprove kwamba ni muhuni, kajitenga na wahuni aliokuwa nao, nitaamini vipi kwamba huyu jamaa hajaja kutengeneza kundi lingine la kihuni?
Lowassa hata kama atakuwa rais, maisha ni yale yale, hatakaa aache ufisadi, na maumivu yatakuwa yale yale kwa sababu tunamjua, ni Fisadi na hajawahi kuahidi kwamba atapambana na mafisadi au wala rushwa kwa moyo dhati.