Meseji kutoka kwa mama mkwe

Meseji kutoka kwa mama mkwe

Amarosa

Member
Joined
Jan 13, 2018
Posts
32
Reaction score
23
Japo tunasema pesa si kila kitu, ila kiukweli pesa ukiwa nayo inakuongezea heshima kwa watu na inakuongezea furaha wewe binafsi.

Yaliyomkuta huyu jamaa yangu, kwa kifupi ndoa yake imekua na migogoro ya mara kwa mara na kiasi kikubwa mke ndio sababu kwani kila kinachotokea lazima akashtaki kwao (kwao mwanamke), wakikwazana kidogo mwanamke anashtaki kwa mama yake, basi hii imefanya kuzidisha mgogoro kati ya kijana na mama mkwe.

Kijana kiuchumi yupo kawaida tu japo anajitahidi kupambana ila mke anamzidi mshahara mama mkwe anajua hilo basi Jana mama mkwe kamtumia Meseji inasema hivi MWANAUME ANAEENDESHA GARI LA BABA YAKE HARUHUSIWI KUONGEA NENO KWENYE KUNDI LA WANAUME WANAOMILIKI BAISKELI ZAO.

kina mama punguzeni midomo kwenye ndoa za watoto wenu, wanaume mzidi kupambana, nanyi wanawake mjifunze adabu sio kila kitu ni cha kushtaki kwenu. Ila hili tusi la mama mkwe shkamoo!!!!!!
 
Ningemjibu hivi Mama mkwe:- Siri ya mtungi aijuae ni Kata. Namkoleza kwa Dushelele la Bombadia Sio Kiba 100 na ndio maana ametulia.

Dawa ya jeuri mwenzie kusudi, hapo mama mkwe lazima akitulize.
 
Ningemjibu hivi Mama mkwe:- Siri ya mtungi aijuae ni Kata. Namkoleza kwa Dushelele la Bombadia Sio Kiba 100 na ndio maana ametulia.

Dawa ya jeuri mwenzie kusudi, hapo mama mkwe lazima akitulize.
Umeuwaaa[emoji122][emoji122][emoji122]kama vipi akaolewe na baba yake tu.
 
Ndoa zina challenge sana, ila kitu Mhimu mwanaume ogopa sana mkeo kukuzidi kipato, hata iweje hawezi kuacha kukudharau. That's the nature, hata km Huyo mwanamke malaika atakuona Ww una mapungufu tu.

Ila pia mwanamke kupeleka ugomvi wenu kwa ndg zake Hiyo ni mbaya ssna
 
ova
Sent from my galaxy using jamiiforums app
 
Kuna wanaume wana moyo wa uvumilivu kweli yaani! Japo kutengena sio sifa nzuri ila nadhani kwangu huo ungekuwa mwisho wetu maana hapo nakuwa sina uhakika kama hajamtafutia mwanaume mwenye baiskeli yake!

Ni vizuri kumrudisha akawape hao wenye baiskeli zao!
 
Mama mkwe kamleaa, sasa anampanda kumkichwa..hovyo kweli huyu mume.
 
Busara ni kumrudisha huyo mwanamke kwa wazazi wake
 
MAMA MKWE YUKO SAHIHI..NA APA VIJANA WENYE AKILI ZA KULELEWA AU KUOLEWA NA MAMA ZAO HAWATOELEWA ATA KIDOGO.

NI UJINGA WEWE MTOTO WA KIUME KUENDESHA GARI YA BABA YAKO UKIWA TAYARI NA MJI WAKO..HII INA MAANA BABA YAKO AKITAKA MZIGO KWA MKE WAKO ANAPEWA TU. SABABU WEWE NGUCHILO HUJUI KUTAFUTA VYAKO.

MZAZI ANAERUHUSU HAYO NAE NI MJINGA TU..HUWEZI KUMDEKEZA MWANAO WA KIUME KIAS HICHO..STUPID FAMILY
Huo ni msemo, haendeshi gari la dingi, ila ni msemo kumaanisha mwanaume hana kipato, dongo yani kwa nilivoelewa
 
Kuna mama wakwe ili mkae sawa unagawa namba yake kwa marafiki zako viwembee wampitiee na ajue unatambua kapakuliwa
 
Ndoa zina challenge sana, ila kitu Mhimu mwanaume ogopa sana mkeo kukuzidi kipato, hata iweje hawezi kuacha kukudharau. That's the nature, hata km Huyo mwanamke malaika atakuona Ww una mapungufu tu.

Ila pia mwanamke kupeleka ugomvi wenu kwa ndg zake Hiyo ni mbaya ssna
Ni kitu kibaya sana obvious ndugu lazima wamchukie mme
 
Back
Top Bottom