Meseji inayosambaa kwa walimu hivi sasa

Meseji inayosambaa kwa walimu hivi sasa

mtoto wa mwenzako ni wako

Nani kasema? Kwa hiyo riz moko ni mwanao? Wanaosoma ulaya wakati wako wanakalia vumbi ni wako? Jipe moyo kwa hilo. Watanzania wa sasa sio wa zamani, na bado. Walimu good keep it up! Wangu nawafundisha nyumbani mwenyewe. Mama salma akudanganye mtoto wa mwenzio ni wako
 
MAISHA BORA NDO HAYO MLIYATAKA WENYEWE NYIE... Mliichagua ccm ya nini. Mlitukanwa na kikwete mkamchagua tena
 
Wazr mzima hana hata aibu hana,Nanukuu ufaulu wa wanafunz wa std 7 umeongezeka mwaka huu,hii si aibu jaman na maks za ufaulu ni kuanzia 70 je ufaulu umeongezeka ama umepungua.....da Tz Elimu ndo inazkwa hvyo na utawala wa JK
 
mi ndo mana walimu nawadharau daily yan ni vilaza kweli,ss hl jambo la sifa!shame on you mwalimu wa tz akili huna

Wewe Javiary ndiyo kilaza mwanaizaya mkubwa! Kama siyo kazi kubwa ya walimu wako bila shaka tusingekujua humu JF na huo utumbo wako wala tusingeuona. Hakuna serikali yoyote duniani inayoweza kupata maendeleo endelevu kwa kudharau elimu. Na unapoongelea elimu mdau wake mkubwa ni mwalimu,pasipo mwalimu hakuna zuri lolote linaloweza kufikiwa. Unajua kwanini Japan na nchi zingine za ulaya zimeendelea? Kubwa ni kwasababu wamewekeza katika elimu,nyie hapa Bongo kwa ujinga mnawekeza katika siasa. Hebu fikiria mbunge ambaye kazi yake ni kulala na kugonga meza tu pale bungeni analipwa zaidi ya Tsh 7/= milioni kwa mwezi na posho ya Tsh 200000/= kwa siku wakati mwalimu analipwa Tsh 240000/= kwa mwezi pesa ambayo haitoshi japo kwa matumizi yake ya nusu mwezi. Mwalimu huyo huyo anaomba aongezewe mshahara ili aweze kujikimu wakati anaendelea na kazi ya kuelimisha watoto wa taifa hili,jibu la Rais anadai kuwa hata walimu wagome kwa miaka nane(8) hawawezi kuongezewa mishahara. Kwa kauli hiyo ya Rais ulitaka walimu wafanye nini? Hapa nani kilaza,walimu au wale wasiotaka kuwekeza katika elimu na badala yake wanaweka vipaumbele katika mambo ambayo hayastahili? Jenga hoja acha kuleta ujinga wako.
 
Joviary am sure umeandika out of jazba,nimawazo yako yataheshimiwa lakini ni ukweli usiopingika walimu wana madhila makubwa mno, na serikali yetu imeamua kuwafanya wanasiasa ndio wenye thamani na kuheshimiwa mno
wataalam wetu, madaktari ,walimu mabwana shamba ambao ndo injini na magurudumu ya Taifa hawapewi kipaumbele
 
Wewe Javiary ndiyo kilaza mwanaizaya mkubwa! Kama siyo kazi kubwa ya walimu wako bila shaka tusingekujua humu JF na huo utumbo wako wala tusingeuona. Hakuna serikali yoyote duniani inayoweza kupata maendeleo endelevu kwa kudharau elimu. Na unapoongelea elimu mdau wake mkubwa ni mwalimu,pasipo mwalimu hakuna zuri lolote linaloweza kufikiwa. Unajua kwanini Japan na nchi zingine za ulaya zimeendelea? Kubwa ni kwasababu wamewekeza katika elimu,nyie hapa Bongo kwa ujinga mnawekeza katika siasa. Hebu fikiria mbunge ambaye kazi yake ni kulala na kugonga meza tu pale bungeni analipwa zaidi ya Tsh 7/= milioni kwa mwezi na posho ya Tsh 200000/= kwa siku wakati mwalimu analipwa Tsh 240000/= kwa mwezi pesa ambayo haitoshi japo kwa matumizi yake ya nusu mwezi. Mwalimu huyo huyo anaomba aongezewe mshahara ili aweze kujikimu wakati anaendelea na kazi ya kuelimisha watoto wa taifa hili,jibu la Rais anadai kuwa hata walimu wagome kwa miaka nane(8) hawawezi kuongezewa mishahara. Kwa kauli hiyo ya Rais ulitaka walimu wafanye nini? Hapa nani kilaza,walimu au wale wasiotaka kuwekeza katika elimu na badala yake wanaweka vipaumbele katika mambo ambayo hayastahili? Jenga hoja acha kuleta ujinga wako.
Safi kabisaaa.
 
kuna nyingine nimetumiwa "Walimu tumeweza maana wanafunzi wa darasa la 7 wamefeli, mpaka sasa wanachakachua mpaka wamechukua wenye Alama 70 baada ya kuona sekondari hazitakuwa na wanafunzi wa kidato CHA 1, tuungane mwakani waendelee kufeli mpaka tuongezewe mishahara. Serikali chezeya Walimu nyinyi.. Mshikamano daima tuma ujumbe huu kwa walimu 15.
 
Meseji za walimu kuhamasishana ziko Nyingi na zinasambaa kweli kweli kwa walimu hii nyingine "Ndugu mwalimu hakikisha humwandai mwanafunzi kupata A,B,C na D. Mwandae apate F,kwani hata akipata A hutaitwa bungeni kupongezwa Kama wanavyopongezwa wanafunzi 20 bora bila hata walimu wao kuwepo.wakipata B hupata kazi Nzuri lakini hawatawasaidia Kama vile watunga sera na waandaji wa mishahara wasivyothamini walimu. Wakipata C huwa WAFANYAKAZI wa kada nyingine ambao hawaungi mkono mgomo wa walimu ila huwacheka na kuwabeza. Wakipata D huwa wanawadharau waliowafundisha, hivyo wapate F ili wajinga wawe wengi na sisi tupate angalau ka heshima kutoka katika umati wa wajinga Kama enzi za mwalimu. Tuma SMS hii kwa walimu 10 wanaojitambua"
 
we Joviary utakuwa mwehu tu,msg yako inaonesha we ni pure tabula rasa...ungekuwa umemaliza atleast std7 ungejua umuhimu wa mwalimu
 
""HAIJAWAHI KUTOKEA!SERIKALI IMEAMUA KUTUMIA MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA KUFANYA SELECTION.
JE, HUKO NI KUTATUA TATIZO AU KUENDELEZA UDHAIFU??JE,UNAWEZA KUTATUA TATIZO KWA KUFICHA UKWELI???WANACHAKACHUA HADI WANAFUNZI WENYE ALAMA 70 WANACHUKULIWA ILI KUINGIA KIDATO CHA KWANZA.BIG UP KWA WALIMU HAKIKA TUKIAMUA TUNAWEZA NA MWAKANI WEMBE NI HUO HUO HADI WATUONGEZEE MSHAHARA.TUMA KWA WALIMU 10.MSHIKAMANO DAIMA!!""mwisho wa kunukuu
My Take::::Bila mjadala wa kitaifa kuhusu mustakabali wa elimu,elimu yetu itayumba na hivyo taifa litaingia kwenye wakati mgumu kimaendeleo.Tuwasikilize hawa walimu kuwakwepa haitatusaidia,wao wana mbinu nyingi za kutukomoa sisi wazazi kama tutawapuuza hawa walimu.
Nawasilisha

hii inanikumbusha wimbo fulani hivi sijui uliiimbwa na kina na nani wale,wanaimba hivi "Inapotokea vitaaa eeeeh wanaoteseka ni watoto na kina mama pia"..............endeleeni kuchekelea tu
 
Back
Top Bottom