Nchi nyingine walimu wanakufa kwa ajili ya wanafunzi wao, jinsi wanavyowapenda watoto/wanafunzi wao. Lakini bongo mwalimu ndio anaweza hata kuwamaliza hao wanafunzi, jinsi anavyowachukia. Yaani kosa la serikali, hasira zinamaliziwa wanafunzi. Hao viongozi serikalini watoto wao wako shule za nje au kwenye private schools. Nyie watoto wenu wa walala hoi ndio wanaenda kwenye hizo hizo shule. Wala hamuikomoi serikali, bali watoto wasio na hatia. Kwa nini unadhani serikali haitekelezi issue zenu, sababu haziwaumi/wahusu. Watoto wao hawa-attend hizo shule....So saaaad. Walimu muwe na moyo jamani na huruma kwa hawa viumbe wadogo wasio na hatia.
Miss-Thang, nadhani utakuwa unakosea..ni nchi gani Mwalimu tuko tayari kufa kwa ajili ya mwanafunzi wake?Utalinganisha mazingira ya KAZI, malipo ,na mengineyo katika nchi hiyo/hizo na Tanzania?
Kumbuka hapa unaongelea zile nchi ambazo, watu wenye ufaulu mkubwa huenda katika Taaluma(Profession) Ualimu ikiwa moja wapo.
Ni wanafunzi wangapi wenye ufaulu mzuri wanaenda Ualimu(hasa hawa wa miaka ya hivi karibuni)? Unadhani ni kwa nini, hawaendi?
Taaluma ya ualimu leo hii imekuwa chaguo(option) la mwiaho la kila mwanafunzi, tena miaka ya hivi karibuni hata wale wasio na ufaulu wanashauriwa kwenda huko...utasikia, "amefeli?.."ee, labda ajaribu teaching, watamchukua tu"
Dharau hii katika taaluma, katika jamii,na kwa Serikali(kutotimiza wajibu wao) inaeakatisha tamaa walimu. Hata wao ni binadamu, wanachoka(they have their limits, personal limits).Na ni katika hatua hii ikifika, ndipo binadamu hufanya chochote kile, hata kama ni mnyonge kwa kiasi gani.
Mkataba, haukuwa wao na watoto wa shule, ilikuwa wao(walimu) na mwajiri(Serikali, kupitia wizara) hivyo hali inapokuwa mbaya, Serikali inapaswa kumwajibisha mwajiriwa(Walimu).Lakini hii ni ngumu pale unapokuwa unafanya humjali/kumpuuza/kutomthamini mwajiriwa(walimu).