Meremeta & TANGOLD Revealed!


Hii inahusiana vipi na kinachoendelea? Una hakika kuwa Mwinyi ndiye aliruhusu watu kula nguruwe?
 

...duh, Bro jmushi1 you need a break! have a...

View attachment 1759

... ha ha
 

kwi kwi kwi,

Haya sasa, je zitto una la kujibu hapa? kwa nini mwinyi alitaka watu wale nguruwe?
 

Kuhani,
Naona umenielewa vibaya.
Sote tunaelewa Usalama wa Taifa haufanyi kazi zake ipasavyo.Ndiyo kuna mafisadi ndani ya usalama huo na ndiyo maana tunataka ufanyiwe marekebisho na ubadilishwe, kuwe na utaratibu mzuri wa kutoa ajira kwa watumishi na viongozi wake walio na machungu na nchi yetu,upewe resources na power ya kutosha ili kuweza kukabiliana na changamoto za 21st century na siyo za vita baridi, ufanye kazi zake kwa manufaa ya umma na mali zake na siyo kwa mafisadi na viongozi wa ccm.
Kuhusu ni nani watawalinda walinzi au usalama wa taifa pili watakapokiuka maadili yao ni sheria hizo mpya ambazo tunataka zitungwe na bunge ndiyo zitawabana usalama wa taifa.
Naomba nikueleweshe tu kuwa kwa hali ya sasa ni vigumu sana kudili na usalama wa taifa.Yaani hata kujadili kazi na shughuli zao inaonekana ni kuvunja sheria hivyo ndugu yangu mambo yanabidi yabadilishwe na kila kitengo au watumishi waweze kuhukumiwa kwa makosa yao au uzembe wao.
Kama kweli usalama wa taifa ungelikuwa unafanya kazi zake ipasavyo tusingekuwa tunazungumzia mambo ya meremeta hapa!!

-Wembe.
 
Mh. Zitto, hongera sana, nimepata furaha sana kusoma ulichosema leo bungeni, maana sijui kama kuna huwazi zaidi ya ulioueleza,umesahau tu kutaja majina ya hao wahusika haswa wa meremeta.
ushauri wangu:nakuomba kuwa muangalifu sana(sina maana huwe muoga),hao uwt wanatumiwa vibaya na hao mafisadi,jichunge bro taifa linakuitaji vibaya mno!
 

mpangilio wa uandishi unaotumia Mh. Zitto, unafanana na Mzee Mwanakijiji, huwa napenda anavyoandika,lugha nyepesi,lakini inaelezea linalokusudiwa.
 
Jmushi1

Punguza kuandika kama uko kwenye genge la kahawa.
 
Jmushi1

Punguza kuandika kama uko kwenye genge la kahawa.

Mkuu OLE heshma mbele!
Kama kweli unaamini hayo ninayoyaandika ni ya gengeni!
Basi tusubiri watakachokifanya!
Na kama yatalingana na ya kwangu...Then uombe msamaha!
Na ninakupa changamoto...Badala ya kukaa pembeni na kusema wenzako wana maneno ya gengeni....Njoo hapa na wewe utoe maoni yako ili tujue na wewe uko upande gani.
Asante.

NB:Hivi kwenye genge la kahawa watu wanaadika na nini?
How?
Hivi unaamini maneno yangu hapo juu ni pumba?
 
Kuhani
...Naomba nikueleweshe tu... Kama kweli usalama wa taifa ungelikuwa unafanya kazi zake ipasavyo tusingekuwa tunazungumzia mambo ya meremeta hapa!!

Na mimi naomba nikueleweshe kitu.

Kazi za idara yeyote inayoanzishwa kwa mujibu wa Sheria, haitakiwi kufanya yale ambayo sheria haisemi.

Usalama wa Taifa hauna majukumu kisheria kuzuia Umeremeta na Urichmonduli.

Tulishachambua hapa ndani na nje sheria za 1970 na 1996 za Usalama. Usalama wa Taifa haujumuishi kuzuia wizi. Hakuna kitu hicho.

Halafu nikuulize hivi: Kwa nini unadhani kwamba mkataba ukipitiwa na Chief of Intilligence ndio utachambuliwa vizuri kuliko Attorney General? Huyu Chenge si mnamuita Harvard Lawyer (even though he ain't), kwani yeye hakuwa na competence ya kupitia Mikataba? Kabla ya kuipeleka kwa Othman, kwanza nionyesha kwamba Chenge aliingia mkenge kwa sababu hakuwa na nyeti fulani ambazo RO angezishtukia.

Wakati mwingine inategemea na dhamira ya anae saini na kupitia mkataba. Usalama wa Taifa nako kuna ufisadi wa hali ya juu. Hata kama wao ndio walikuwa wanapitia mikataba, sidhani kama ingepona hii.

Ndio maana nasema usi assume kwamba mikataba ikienda Usalama itanyooshwa, kana kwamba mwanasheria wa wa Usalama ni muadilifu kuliko wa ofisi ya Attorney General.

Tunarudi pale pale:

"Who will watch the watchers?"
 

Tumeshaambiwa usalama wa Taifa hawaku clear mikataba.
Hivyo ni wazi kuwa hata usalama wa taifa haiusiki.
Hivyo kubishana kwetu kuhusu nani asimamie mikataba kuko nje ya topic!
MIKATABA ILISIMAMIWA NA MAFISADI NA SI USALAMA WA TAIFA!


Matatizo ya Mwembe chai MREMA akiwa waziri wa mambo ya ndani na Mwinyi Rais ni yapi?
 
Last edited by a moderator:
NB:Hivi kwenye genge la kahawa watu wanaadika na nini?How?
Hivi unaamini maneno yangu hapo juu ni pumba?


Kwa uelewa wangu mimi genge la kahawa waongea chochote kile (hawana focus yaani katika maongezi yao wanachanganya utumbo, steki, kachumbari, kiburu, machalari,kande, ugali, sukari na shubiri bila kuacha pilipili kichaa kwa pamoja) tu ili mradi saa ziende wacall it a day na mwisho wa siku wanaevaluate nani kaongea sana, sio nani kaongea nini.
 
whats this?
Mheshimiwa Mwenyekiti, nitatoa mfano wa masuala matatu tu. Kwa mfano, suala la nishati ni suala la Usalama wa Taifa, national security concerned ilikuwaje nchi yetu ikaingia mikataba ya nishati bila clearance ya Usalama wa Taifa. (Makofi)

Pinda Alisema Dili Ni Za Usalama Wa Taifa!
Na Hapo Juu Zitto Anasema Usalama Wa Taifa Hawa Ku Clear Hizo Contracts!
Tunataka Pinda Atueleze Alipo Kuwa Ana Refer.."usalama Wa Taifa" Alimaanisha Nini?
Na Tunataka Kujua Kama Usalama Wa Taifa Anayozungumzia Pinda Ni Sawa Na Ile Anayoizungumzia Zitto.
Kama Ni Moja Tujue.
Na Kama Ni Mbili Pia Tuambiwe!
Ila Moja Ni Lazima Si Nzuri Na Nyingine Ni Nzuri.
 
Jmushi01

Mkuu niko hapa kuona Threads hazichafuliwi, kama kweli hoja yako inasimama huna sababu ya kupost four or five posts at a go andika tu hata kama ni ndefu then post.

Kila member akifanya unavyoandika patakuwa hapatoshi hapa, ukiangalia mawazo yako yanakuwa yanajirudia rudia bila direction. Kuna wasomi hapa ambao wanauwezo wa hali ya juu kuchanganua habari.


Natumaini umenielewa.
 
Koba... usiwe na shaka ndugu yangu... mapambano safari hii yanapiganwa kitaalamu zaidi.. misingi huwekwa na jengo hujengwa.. tumpe support na kundi la wabunge wengine wanaokuja mbeleni... mabadiliko ni lazima, na yatatoka kwa wananchi wenyewe.

na mimi ni mmoja wapo ninayetaka kum-support Mh Zitto na wengine, ila sijui nifanye nini ku-support, kwa kuandika ujumbe hapa au kuna lolote twaweza fanya?
 

Kumbe na wewe umeona tatizo la Mushi, anakuwa na strong point lakini akianza kuandika kama ukuconcetrate kusoma then anakuacha kwa kuwa anapoza focus wakati wa kuandika.
 
Suala la NISHATI NI SUALA LA USALAMA WA TAIFA!
LAKINI MIKATABA YENYE KUHUSU NISHATI..AMBAYO INAANGUKIA KWENYE USALAMA WA TAIFA HAIKUPITISHWA NA USALAMA WA TAIFA KAMA ZITTO ALIVYOSEMA.
HOWEVER...PINDA ALISEMA KUWA MIKATABA HIYO NI USALAMA WA TAIFA.
ZITTO ALIVYOSIKIA HAKUPENDEZWA...NA AKAFUNGA SAFARI KWENDA DODOMA.
PINDA AKAKIMBIA!
SASA TUNATAKA AJIBU.
 

Labda anataka kufikisha post 30,000 kisha tumtumie pongezi
 

Misconception of Law.

Alichokisema Zitto ni vague. Sheria hazisemi hiyo ni kazi yao Usalama. Na Wabunge wamepiga makofi bila kujijua, kama kawaida yao. Wanadhani kwamba kila kitu kinacho sound muhimu muhimu kama nishati basi ni kazi ya Usalama wa Taifa. Dead wrong!

Kama kina Zitto wanataka mabadiliko ya sheria lazima wachonge hoja zao ziwe sharper. Ningekuwa mimi Mbunge fisadi hapa ningewatoa nishai kina Zitto na hiyo pointi yao hapo. Mikataba ya Tanesco sio mikataba ya Usalama, kwa mujibu wa Sheria.

Hawa wabunge kila siku kabla ya kusema kitu inabidi wamuulize Sitta kama it's ok, as if Sitta ndio arbiter wa sheria za immunity za Wabunge. Huyo Phillip Marmo mwenyewe hajui anachokifanya. Kamwambia Slaa, "Slaa unafanya jinai kutoa siri" za Meremeta Bungeni. Slaa akamwambia "nikamateni." Marmo akafyata. Alikuwa kakurupuka tu. Hawajui sheria hawa watunga sheria hawa. So pathetic!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…