Mere prediction about the future: Yajayo yanafurahisha, upo tayari?

Sikutarajia kama kuna watu wangekuja kupinga juu ya kilichoandikwa humu,nadhani ni sawa kuwa na mawazo tofauti ili tupate maendeleo lkn mawazo haya kinzani ya kuponda tu eti kwa sababu alishawah leta mada fulani za forex sijui!!??........niwatakie usiku mwema!!
 
Hebu niambie umeizidi nini teknolojia?

Au unajivunia uwezo wa jirani yako ukadhani na wewe unao?
Kwa hiyo hoja hapa ni mimi "muuza ubuyu" au "binadamu" kuizidi tekinolojia?

Au jirani yangu kuwa na uwezo mkubwa kunamfanya yeye asiwe binadamu?

Msihadaike, hizo tekinolojia zote mnazoziona zinagunduliwa na kuongozwa na mwanadamu. Kama huelewi pole!
 
Haya vijana acheni sijui kutafuta credit sijui ukasome HKL mara sijui ualimu, dunia inazidi kutanuka.

Nendeni Veta na vyuo vya Computer Science mkachukue maujuzi ya "IT" maana ndio kozi pekee iliyobaki inayoweza kukusukuma kwa siku za mbeleni ila uwe mjanja mjanja na wa kujiongeza.

Shukrani mkuu.
Mkuu umewaza km Mimi nilivyowaza ,
 
One day, technology will surpass human intelligence.

- Albert Eisten
haiwezi kuwa kamwe... haiwezi kuwa kamwe... labda kama itajitengeneza yenyewe na sio binadamu kuhusika na kuitengeneza katika muelekeo anao taka yeye....

NB:
Haiwezi kutokea... labda zije kuwa aliens tofauti na hapo hamna kitu
 
Hiyo ndo dunia ambayo nabii wa Mungu alionyeshwa ila kwakuwa tu wagumu kuamini lazma fire itatumulika hapo ni kuamua kumsikiliza Mungu ama mwanadamu
Nasubiri sehemu nyeti maana najua bado inakuja
"Bora kuamini Mungu yupo ukienda ukamkuta poa kuliko kuamini hayupo ukimkuta fire"
 
Sisomi comment za humu ndani Tena maana naweza kufa kwa kucheka..... Watu wana mambo kweli....
Bora mie ambae huwa sisomi kabisa vitabu, Mara ya mwisho nimesoma 2015
Zaidi ya hapo nasoma biblia na lesoni tu
Nataka uniambie comment ipi imekuchekesha nami nicheke
 
Africa tutafika?
Viongozi wote wa kiafrica ni wazee wenye fikra za miaka 1600 iliyopita halafu unataka mfike?

Maji safi ndani ya jiji la Dar ambalo limezungukwa na bahari ila maji tu ni kimbembe...

Hadi sasa hivi viongozi wetu wanapambana na ufisadi na kuteuwa na kutengua unafikiri kuna wakati watapata mda na kukaa chini na vijana wenye vipaji na kuona ni jinsi gani ya kuviendeleza?

Kule Zanzibar tumeambia leo kuna vijana wameunda ndege ila ukijaribu kufuatilia mwisho wake unaweza kulia..

Kule yule ndugu yetu wa mbeya aliyeunda helcopta mnajua alipo na anafanya kitu gani serikali au kuna makampuni ya ndani yamemsaidia kifedha kukamilisha project yake?

Huyu Musk ni mzaliwa wa Africa Kusini mkaburu alizamia canada ili apate urahisi wa kuzamia Marekani, ss hivi huyo anafanya maajabu...

Africa kinacho wamaliza ni siasa kitu wanaingiza siasa, mtu anasoma masomo ya niclear mwisho anakuja kuchukua form ya kugombea urais au ubunge

Mambo mengine kuyawaza yanatia sana hasira...
 
Uongo mkubwa uliowahi kuongea ww bwana Ontario ni kua "Eti kuna machine ya 3D inayatumika kuprint nyumba, so baada ya miaka kama 20 watu watakua wanafyatua nyumba kwenye mashine"

-Tera La Vista
Hii hata mimi kila nikijaribu "kulisukumizia" kwenye ubongo wangu linakataa kabisa,sasa kama nyumba inakuwa printed inamaana hilo printer lenyewe lina ukubwa kiasi gani?......lakini pia kuna lile la kumfyatua binadamu kama tofali maabara,hili nalo japo ni tecknolojia ila nahisi kama "kamba" hivi ila sijui tuendelee kusubiri lakini sidhani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom