Mengine tunayapika wenyewe, hivyo wajibu tuyale tu

Dhahiri katiba yatupa haki ya kukosoa, kuhoji na hata kupinga mawazo ya kiongozi yeyote ila haitupi uhuru wa kumtukana, kumkashifu na kutumia lugha ambayo ni dhahiri ya kuudhi.

Tunapopinga vitendo vya utekaji, pia tupinge vitendo vya kutumia lugha za kuudhi dhidi ya wenzetu. Maana kukosoana kwa namna ya kutukana si utanzania na kinyume cha utu.

Tujue mtu kama Rais au kiongozi wa Chama kikubwa kama CHADEMA ana wafuasi wengi, unapomtukana ni dhahiri yeye anaweza kuona hayo ni gharama tu ya wadhifa wake, na asifanye lolote zaidi ya kusamehe, walakini kwa wafuasi wake huweza kuwa habari nyingine kabisa. Mfuasi anaweza kukosa uvumilivu kwa kiongozi wake kuchafuliwa.

Kumtukana Rais ni sawa na kuwatukana watu waliomchagua, na kumtukana Mbowe ni sawa na kuwatukana wanaCHADEMA wote. Wengi wanaweza kuvumilia matusi lakini si wote, pia mara nyingi watu wanaweza kuyapuuza matusi lakini si mara zote, na kwa msingi huo, pengine hii tekateka huu ndio usuli wake.

Mfuasi akishindwa kuvumilia matusi anayorushiwa kiongozi wake, anaweza kuchukua hatua ambayo haitazamiwi au si ya kutarajiwa. Matukio kama ya yaliyomkuta Mdude huko Vwawa na Tesha huko Igunga huenda yamesababishwa pia na ndimi zao chafu dhidi ya watu wenye wafuasi wengi; pengine wafuasi wa watu ambao mara kadhaa hawasalimiki na ndimi zao wamehusika katika yote haya. .

Kama kuna jambo baya ni kurukia kulishuku jeshi la Polisi juu ya yote haya. Sisemi Polis kama taasisi ya umma haifanyi makosa, walakini pia tusilipakaze matope jeshi letu kwa uovu ambao ni dhahiri jeshi hilo ni vigumu kuufanya hasa kwa kipindi kama hichi.

Hivi kwa aina ya uongozi wa Rais Magufuli na shutuma inazotupiwa juu ya haki za kibinadamu, hivi kweli Polis au TISS watafanya ushenzi ule kwa Mdude? Ili iweje? Ili utawala wa awamu ya tano uzidi kuoga na matope na kupoteza uungwaji mkono kutoka jumuia za kimataifa? .

Ulishawahi jiuliza? Kwanini utekaji akifanyiwa mpinzani shutuma hutupiwa TISS na Polis lakini akifanyiwa mwanaCCM hawahusishwi Polis au TISS?
Yote haya huenda wafuasi wa pande mbili wanatiana ADABU. Greenguard na Redbrigadia zitupiwe jicho.

Na
@jini_kinyongaView attachment 1093270
Fala sana Mdude ,analeta enzi za mwalimu JK Nyerere za ujima ana fananisha na zama za kileo tknolojia iko juu,
Anataka rais atembelee pijoti zama hizi?
 
Kosa la huyo Mdude ni kushindwa kuelewa kuwa yule Rais mmoja anayemuona ni kiongozi wa taasisi ya urais.

Kamkejeli na kumdhihaki rais wa nchi kama vile anayemuongelea ni rais wa wasafi au yule Manzese.

Huwa napenda kujiuliza tu, unaweza kumkejeli Kagame ukiwa Rwanda halafu ukaendelea kuliona jua linatoka mashariki asubuhi?.

Unaweza kweli kumkejeli Museveni halafu utoke salama Uganda?. La kujifunza ni kupima unaandika nini mitandaoni.

..Tanzania Bara tumewahi kuwa na watu waliohusishwa na UHAINI.

..Hilo ndilo kosa kubwa kabisa dhidi ya dola na kiongozi wake.

..lakini waliohusika na UHAINI huo hawakuuwawa [ isipokuwa Tamim aliye-resit arrest], kuteswa, au kudhalilishwa, kama wanavyofanyiwa wapinzani ktk awamu hii.

..kama Tanzania Bara tumewahi kuwa na wahaini na tukawafikisha mahakamani wakahukumiwa ,
nini kinatuzuia kufuata utaratibu kama huo kushughulikia wanaotuhumiwa kutoa "kejeli" ktk mitandao?

..natofautiana na mtizamo wako unapotulinganisha na Rwanda au Uganda. Kwa maoni yangu we are far better than them kwenye masuala ya Human rights.
 
Mtu akikwambia wewe ni mwizi unakasirika au hutakasirika?? je kuambiwa we ni mwizi kwa kuwa ni lugha ya kuudhi tupe neno mbadala la Mwizi kwa mujibu wa katiba tulitumie maana tumechoka kutekwa na kuuawa.
soma huo mchango wako kisha rejea hoja yangu msingi, pengine utaona ni kwa namna gani uko kabisa nje ya hoja.
 
Huenda zimeponza, na huenda wafuasi wa watu aliowatukana wameshindwa kumvumilia, na ndipo nikasema tukosoane kwa lugha ya hishima hata kama ikiwa kali.
Vipi na wafuas wa hao wanaotekwa wakianza kuwateka wanaowateka viongozi wao nchi itakuaje?
 
Utaonaje sasa kama baba yenu moja.
Kila mwanadamu ataonja mauti.
Swala la kutokuona jua kutoka mashariki Asubuhi ni la kilamtu.Sema style ndio tofauti.
Sijaona sehemu alipokosea mdude hapo.
 
Dotto C. Rangimoto,

..unafikiri green-guard au red-brigade wana uwezo wa kuondoa walinzi wa area D wanapoishi viongozi wa serekali na kumshambulia Mh.Lissu na wasijulikane mpaka leo?
Mkuu JokaKuu, hakuna namna ya kuweza kutetea uovu wa waliomteka mdude na wale waliotaka kumuua lisu. Lakini unafikiri ni busara kumuita rais mstaafu msukule na rais aliye madarakani jini?!

Huyu mdude anasema ni ofisa wa chadema kanda, pengine ni njia ya kuwaonyesha wakubwa wake kuwa anafaa katika nafasi anayoitumikia!
 
Na ndipo nikasema, Kikwete kuna watu wengi wanampenda hata sasa, alkadhalika na Magufuli wapo watu wengi wanampenda. Sasa hawa watu kweli wote wanavumilia matusi haya kwa wapendwa wao?? Kwanini tunakimbilia kuishutumu TISS na Polis tu bila kuwaza uwezekano wa kuwapo wafuasi, wapenzi na mashabiki wa viongozi hao walichoshwa na matusi dhidi ya wapendwa wao????
 
..kinachoendelea hapa ni sawa na mtoto wa kike abakwe halafu badala ya ku deal na waliombaka tunaanza kumlaumu kwanini amekuwa na tabia ya kuvaa nguo fupi!!

..ninachosisitiza mimi ni kuwa wanaotuhumiwa kutumia lugha za "kuudhi" WASIUWAWE, au WASITESWE, badala yake wapelekwe MAHAKAMANI.

..kwa maoni yangu Lissu kupigwa risasi, au Mdude kuteswa, ni tatizo kubwa ktk jamii yetu kuliko Raisi Mstaafu au wa sasa kuitwa majina mabaya.

..Mtu akiitwa jina baya hafi, au halazimiki kutibiwa hospitali miaka 2. Lakini mtu akipigwa RISASI anaweza kufa.
 
..mashabiki wa JPM wana mamlaka / uwezo wa kuondoa ulinzi Area D ili wapate kumtwanga risasi Mh.Tundu Lissu?
 
Dhahiri katiba yatupa haki ya kukosoa, kuhoji na hata kupinga mawazo ya kiongozi yeyote ila haitupi uhuru wa kumtukana, kumkashifu na kutumia lugha ambayo ni dhahiri ya kuudhi.

Tunapopinga vitendo vya utekaji, pia tupinge vitendo vya kutumia lugha za kuudhi dhidi ya wenzetu. Maana kukosoana kwa namna ya kutukana si utanzania na kinyume cha utu.

Tujue mtu kama Rais au kiongozi wa Chama kikubwa kama CHADEMA ana wafuasi wengi, unapomtukana ni dhahiri yeye anaweza kuona hayo ni gharama tu ya wadhifa wake, na asifanye lolote zaidi ya kusamehe, walakini kwa wafuasi wake huweza kuwa habari nyingine kabisa. Mfuasi anaweza kukosa uvumilivu kwa kiongozi wake kuchafuliwa.

Kumtukana Rais ni sawa na kuwatukana watu waliomchagua, na kumtukana Mbowe ni sawa na kuwatukana wanaCHADEMA wote. Wengi wanaweza kuvumilia matusi lakini si wote, pia mara nyingi watu wanaweza kuyapuuza matusi lakini si mara zote, na kwa msingi huo, pengine hii tekateka huu ndio usuli wake.

Mfuasi akishindwa kuvumilia matusi anayorushiwa kiongozi wake, anaweza kuchukua hatua ambayo haitazamiwi au si ya kutarajiwa. Matukio kama ya yaliyomkuta Mdude huko Vwawa na Tesha huko Igunga huenda yamesababishwa pia na ndimi zao chafu dhidi ya watu wenye wafuasi wengi; pengine wafuasi wa watu ambao mara kadhaa hawasalimiki na ndimi zao wamehusika katika yote haya. .

Kama kuna jambo baya ni kurukia kulishuku jeshi la Polisi juu ya yote haya. Sisemi Polis kama taasisi ya umma haifanyi makosa, walakini pia tusilipakaze matope jeshi letu kwa uovu ambao ni dhahiri jeshi hilo ni vigumu kuufanya hasa kwa kipindi kama hichi.

Hivi kwa aina ya uongozi wa Rais Magufuli na shutuma inazotupiwa juu ya haki za kibinadamu, hivi kweli Polis au TISS watafanya ushenzi ule kwa Mdude? Ili iweje? Ili utawala wa awamu ya tano uzidi kuoga na matope na kupoteza uungwaji mkono kutoka jumuia za kimataifa? .

Ulishawahi jiuliza? Kwanini utekaji akifanyiwa mpinzani shutuma hutupiwa TISS na Polis lakini akifanyiwa mwanaCCM hawahusishwi Polis au TISS?
Yote haya huenda wafuasi wa pande mbili wanatiana ADABU. Greenguard na Redbrigadia zitupiwe jicho.

Na
@jini_kinyongaView attachment 1093270
Amevuna alichopanda ma.mae...huwez kutusi dola af uwepo wepo tuu
 
..kinachoendelea hapa ni sawa na mtoto wa kike abakwe halafu badala ya ku deal na waliombaka tunaanza kumlaumu kwanini amekuwa na tabia ya kuvaa nguo fupi!!

..ninachosisitiza mimi ni kuwa wanaotuhumiwa kutumia lugha za "kuudhi" WASIUWAWE, au WASITESWE, badala yake wapelekwe MAHAKAMANI.

..kwa maoni yangu Lissu kupigwa risasi, au Mdude kuteswa, ni tatizo kubwa ktk jamii yetu kuliko Raisi Mstaafu au wa sasa kuitwa majina mabaya.

..Mtu akiitwa jina baya hafi, au halazimiki kutibiwa hospitali miaka 2. Lakini mtu akipigwa RISASI anaweza kufa.
Na mimi nimetahadharisha tu. Huko kutekwa na utesaji ni ajabu sana kuisingizia POLIS au TISS, ikiwa CCM ina mamilioni ya wanachama na Magufuli kapigiwa kura na mamilioni ya watu, sasa jiulize watu hawa wote wanaridhika na matusi ya Mdude kwa mwenyekiti wao au kwa mtu waliyemchagua kuwa Rais?? Kwahivyo huenda kuna mtu watu wamechoshwa na haya matusi,,,,na wakaamua kumshughulikia Mdude kwa njia zao....

Ni wajibu wa Polis kuwatafuta watekaji na ni wajibu wa Polis kumlinda Mdude, lakini si sawa kuilamu Polis au Magufuli ikiwa wao hawajawatuma watekaji, lakini pia tunaweza kumlamu Mdude sababu huenda kama asingewaudhi wafuasi wa Maguful asingekipata kisago. Unamtukanaje mtu mwenye wafuasi mamilioni ya watu??? Yeye atakupotezea, je wafuasi wake watakuacha kweli??? Hivi Kikwete anavyopendwa afu mtu anamwita Mzukule,,kweli???

Mdude ajifunze kukosoa na kujenga hoja pasina kutukana au kutoa lugha ya kuudhi.
 
Dotto hebu nisaidie kidogo. Vipi watekaji wakianza kuwateka watekaji nchi itakalika?
 
..kwa hiyo mtu akitumia lugha ya kuudhi dhidi ya kiongozi unayempenda dawa yake ni kumtwanga marisasi, kumteka, au kumtesa?

..upande wa upinzani nao wakianza kulipiza kisasi unafikiri tutakuwa na nchi kweli?
 
Si dawa yake lakini haimaanishi kuwa watu wenye kujichukulia sheria mkononi hawapo na kwa msingi huo kwanini tusiwaepuke hao watu kwa kuacha kutukana badala yake tujadili masuala?? mfano suala la gharama kubwa katika msafara wa Rais hivi hatuwezi kweli kulijadili pasina kutumia neno Jini, mzukule, mwizi, na mengine mfano ya hayo???

"Msafara wa Rais Mkubwa na mzigo kwa wananchi, kuna mambo muhimu yanahitaji fedha...." Waweza kusema hivi na ukaeleweka kabisa,,yanini utukane na kuwaudhi wafuasi wa mtu kisha uwape nafasi wakushughulikie???
 
Mtu akikwambia wewe ni mwizi unakasirika au hutakasirika?? je kuambiwa we ni mwizi kwa kuwa ni lugha ya kuudhi tupe neno mbadala la Mwizi kwa mujibu wa katiba tulitumie maana tumechoka kutekwa na kuuawa.

juzi tu mmeambiaa bahili mmekasirika mpaka basi
 
Back
Top Bottom