Mengine tunayapika wenyewe, hivyo wajibu tuyale tu

Mengine tunayapika wenyewe, hivyo wajibu tuyale tu

Kwa hiyo unatutangazia kuwa walio mteka huyo mtu ni watu wa serikali yenu?
Kosa la huyo Mdude ni kushindwa kuelewa kuwa yule Rais mmoja anayemuona ni kiongozi wa taasisi ya urais.

Kamkejeli na kumdhihaki rais wa nchi kama vile anayemuongelea ni rais wa wasafi au yule Manzese.

Huwa napenda kujiuliza tu, unaweza kumkejeli Kagame ukiwa Rwanda halafu ukaendelea kuliona jua linatoka mashariki asubuhi?.

Unaweza kweli kumkejeli Museveni halafu utoke salama Uganda?. La kujifunza ni kupima unaandika nini mitandaoni.
 
Na ndipo nikasema, Kikwete kuna watu wengi wanampenda hata sasa, alkadhalika na Magufuli wapo watu wengi wanampenda. Sasa hawa watu kweli wote wanavumilia matusi haya kwa wapendwa wao?? Kwanini tunakimbilia kuishutumu TISS na Polis tu bila kuwaza uwezekano wa kuwapo wafuasi, wapenzi na mashabiki wa viongozi hao walichoshwa na matusi dhidi ya wapendwa wao????
wanashtumiwa kwa sababu kazi yao nikuhakikisha hayo matukio hayafanyiki au wafanyaji wanakamatwa.
 
Dhahiri katiba yatupa haki ya kukosoa, kuhoji na hata kupinga mawazo ya kiongozi yeyote ila haitupi uhuru wa kumtukana, kumkashifu na kutumia lugha ambayo ni dhahiri ya kuudhi.

Tunapopinga vitendo vya utekaji, pia tupinge vitendo vya kutumia lugha za kuudhi dhidi ya wenzetu. Maana kukosoana kwa namna ya kutukana si utanzania na kinyume cha utu.

Tujue mtu kama Rais au kiongozi wa Chama kikubwa kama CHADEMA ana wafuasi wengi, unapomtukana ni dhahiri yeye anaweza kuona hayo ni gharama tu ya wadhifa wake, na asifanye lolote zaidi ya kusamehe, walakini kwa wafuasi wake huweza kuwa habari nyingine kabisa. Mfuasi anaweza kukosa uvumilivu kwa kiongozi wake kuchafuliwa.

Kumtukana Rais ni sawa na kuwatukana watu waliomchagua, na kumtukana Mbowe ni sawa na kuwatukana wanaCHADEMA wote. Wengi wanaweza kuvumilia matusi lakini si wote, pia mara nyingi watu wanaweza kuyapuuza matusi lakini si mara zote, na kwa msingi huo, pengine hii tekateka huu ndio usuli wake.

Mfuasi akishindwa kuvumilia matusi anayorushiwa kiongozi wake, anaweza kuchukua hatua ambayo haitazamiwi au si ya kutarajiwa. Matukio kama ya yaliyomkuta Mdude huko Vwawa na Tesha huko Igunga huenda yamesababishwa pia na ndimi zao chafu dhidi ya watu wenye wafuasi wengi; pengine wafuasi wa watu ambao mara kadhaa hawasalimiki na ndimi zao wamehusika katika yote haya. .

Kama kuna jambo baya ni kurukia kulishuku jeshi la Polisi juu ya yote haya. Sisemi Polis kama taasisi ya umma haifanyi makosa, walakini pia tusilipakaze matope jeshi letu kwa uovu ambao ni dhahiri jeshi hilo ni vigumu kuufanya hasa kwa kipindi kama hichi.

Hivi kwa aina ya uongozi wa Rais Magufuli na shutuma inazotupiwa juu ya haki za kibinadamu, hivi kweli Polis au TISS watafanya ushenzi ule kwa Mdude? Ili iweje? Ili utawala wa awamu ya tano uzidi kuoga na matope na kupoteza uungwaji mkono kutoka jumuia za kimataifa? .

Ulishawahi jiuliza? Kwanini utekaji akifanyiwa mpinzani shutuma hutupiwa TISS na Polis lakini akifanyiwa mwanaCCM hawahusishwi Polis au TISS?
Yote haya huenda wafuasi wa pande mbili wanatiana ADABU. Greenguard na Redbrigadia zitupiwe jicho.

Na
@jini_kinyongaView attachment 1093270
Mo, Zakaria, Bashe ni CHADEMA?

Suala la utekaji kwa Sasa hivi suspect ni wale wale tu uwe CCM, uwe CHADEMA
 
Kuna wafia chama wa pande zote mbili hapa hawatachangia huu uzi bila kuhusisha mihemko yao..ila mtoa mada umeonge ukweli ambao unawagusa moja kwa moja..

Kwenye key bord za simu zao wanaandika mihemko ila mioyoni mwao wanajua kuwa huyo binadamu mwenzetu ameteleza na alikuwa anateleza..

Kweli..tumepewa Uhuru kikatiba wa kufanya lolotee..lakini Uhuru huo ukawekewa mipaka ya kutovuka sharia..na moja ya sheria ni kutumia lugha nzuri katika jamii..

Yamkini nikawa kweli naichukia ccm na serikali yake...basi isiwe kigezo cha kunihalalisha nianze kutumia lugha isiyo staha kama huyo ndugu mdude...

Kama ulivyosema japo inawezekana kabisa na hata serikali yenyewe kwa maana tiss na polisi kuhusika moja kwa moja au indirect ...lakini tujue kuwa kukosoa hakuna mipaka..kama ilivyochuki ..lakini vyema ustarabu ukatumika na sio uhuni...
 
MOSI.
Kwenye 3 yako na ndipo ilipo hoja yangu. Kwanini wasema serikali isitumie njia za kimafia?? wataka kutuaminisha kuwa serikali ndiyo imefanya hayo kwa Mdude?? Hoja yako ya hiyo ya kudhani serikali ina mkono wake ndiyo msingi wa UZI wangu.

Nimefafanuwa vizuri, tusikimbilie serikali ikiwa huyo Mdude kawaudhi mamilion ya watu na hatujui hao mamilioni wangapi watamchukulia poa.

PILI.
Nimesema ni wajibu wa Polisi kulinda raia wote na si Mdude tu, lakini ulinzi wa raia huwa vipi??

A. RAIA KUJILINDA MWENYEWE.
Jukumu la kwanza kabisa la kila raia ni kuilinda nafsi yake kwa kila aina ya tishio. Kujilinda ni pamoja na kuepuka mambo yanayoweza kuhatarisha maisha yako. Huwezi kufanya mambo hatarishi kwa usalama wako kisa tu unaweza kujilinda au kuna Polisi itakulinda. Huu ni ujinga.

Hii ni sawa na kutembea Mtaa wa Kongo kwa miguu ukihesabu malaki au mamilioni ya Shilingi. Ukiporwa kisha lawama ulitupie jeshi la polisi.

Kuacha au kujiepusha kutukana watu ni hatua ya MSINGI KABISA katika kujilinda. Usifata hatua hiyo ya msingi hatua inayofuata itakuwa ngumu kuitekeleza.

B. WAJIBU WA POLISI.
Raia akishachukuwa hatua zote za kujilinda yeye na mali zake, hapo ndipo linapokuwa rahisi kwa jeshi la Polisi kuimarisha ulinzi aliojipatia Raia mwenyewe.

Sababu ukiacha kuudhi watu wengi ni dhahiri wajipunguzia hatari ya kushambuliwa na kubwa zaidi wajipunguzia maadui. Mtu mwenye maadui wachache ni rahisi kumlinda. Sasa Mdude anajijengea maadui wengi alafu anataka jeshi la polisi liwajibike kwa ulinzi wake, hivi hili jeshi lina ukubwa gani wa kuweza kutoa ulinzi maalum kwa kila raia?? Kwanini tusilipunguzie kazi kwa kupunguza maadui zetu??

MWISHO
Tunaweza kulilaamu jeshi letu katika mambo mengine, lakini kwa habari ya Mdude ni kulionea tu jeshi la Polis. Watu kama Mdude wabadilike, mambo mengine wanaweza kuyaepuka kwa kuacha lugha chafu tu.
Bado. Huna point yoyote ya maana.
1. Unaelezea mambo ambayo yako wazi na hayana haja ya kuelezea. eg: hakuna nilipoandika wajibu wa polisi ni kumlinda Mdude tu.
2. Mdude hakufanya uzembe wa kujilinda. Alichukuliwa kwa nguvu bila ridhaa yake kwa njia za kimafia.
3. Nimesema na narudia kusema tena: hakuna sheria inayosema kiongozi akisemwa vibaya basi wafuasi wake wana haki ya kulipiza kisasi. Na wafuasi wake wakilipiza kisasi basi polisi haitakiwi kuchukuwa hatua.
4. Sitaki kukuaminisha kuwa serikali ndiyo imefanya hivyo. Nimesema serikali inatakiwa kuchukuwa njia halali za kisheria kushughulikia watu kama hao.
 
Kwahiyo unataka kutuambia ni halali kuchukua sheria mkononi unapokosewa na mwenzio. Au ni kuwa unahalalisha watu kuvunja sheria kuwawajibisha wenzao sababu tu ya ushabiki. Kama wanausalama wetu wangekuwa serious na kazi yao, wewe ungewekwa ndani utoe Maelezo dhidi ya uchochezi
 
Sidhani kama unao ushahidi kwamba MO Dewji alitekwa kwa amri ya mkuu wa nchi. Yule ni mfanyabiashara mwenye uhusiano wa kibiashara na watu wengi tu, afrika na duniani kwa ujumla.

.." huna ushahidi " naona imekuwa ni kichaka cha kulea MAOVU ktk jamii yetu.

..lakini sasa hivi kunaibuka tatizo lingine la wananchi kuanza kupoteza imani na vyombo vya uchunguzi na vyombo vya kutoa haki.

..sidhani kama huo ni muelekeo mzuri kwa nchi yetu.

..Naamini AMANI inadumishwa kama kutakuwa na HAKI.

..Na HAKI inapatikana ikiwa kuna uchunguzi wa kweli na wa uhakika, na masuala yetu yanaamuliwa na mahakama zilizo huru.
 
Back
Top Bottom