Dotto C. Rangimoto
JF-Expert Member
- Nov 22, 2012
- 1,985
- 1,286
Dhahiri katiba yatupa haki ya kukosoa, kuhoji na hata kupinga mawazo ya kiongozi yeyote ila haitupi uhuru wa kumtukana, kumkashifu na kutumia lugha ambayo ni dhahiri ya kuudhi.
Tunapopinga vitendo vya utekaji, pia tupinge vitendo vya kutumia lugha za kuudhi dhidi ya wenzetu. Maana kukosoana kwa namna ya kutukana si utanzania na kinyume cha utu.
Tujue mtu kama Rais au kiongozi wa Chama kikubwa kama CHADEMA ana wafuasi wengi, unapomtukana ni dhahiri yeye anaweza kuona hayo ni gharama tu ya wadhifa wake, na asifanye lolote zaidi ya kusamehe, walakini kwa wafuasi wake huweza kuwa habari nyingine kabisa. Mfuasi anaweza kukosa uvumilivu kwa kiongozi wake kuchafuliwa.
Kumtukana Rais ni sawa na kuwatukana watu waliomchagua, na kumtukana Mbowe ni sawa na kuwatukana wanaCHADEMA wote. Wengi wanaweza kuvumilia matusi lakini si wote, pia mara nyingi watu wanaweza kuyapuuza matusi lakini si mara zote, na kwa msingi huo, pengine hii tekateka huu ndio usuli wake.
Mfuasi akishindwa kuvumilia matusi anayorushiwa kiongozi wake, anaweza kuchukua hatua ambayo haitazamiwi au si ya kutarajiwa. Matukio kama ya yaliyomkuta Mdude huko Vwawa na Tesha huko Igunga huenda yamesababishwa pia na ndimi zao chafu dhidi ya watu wenye wafuasi wengi; pengine wafuasi wa watu ambao mara kadhaa hawasalimiki na ndimi zao wamehusika katika yote haya. .
Kama kuna jambo baya ni kurukia kulishuku jeshi la Polisi juu ya yote haya. Sisemi Polis kama taasisi ya umma haifanyi makosa, walakini pia tusilipakaze matope jeshi letu kwa uovu ambao ni dhahiri jeshi hilo ni vigumu kuufanya hasa kwa kipindi kama hichi.
Hivi kwa aina ya uongozi wa Rais Magufuli na shutuma inazotupiwa juu ya haki za kibinadamu, hivi kweli Polis au TISS watafanya ushenzi ule kwa Mdude? Ili iweje? Ili utawala wa awamu ya tano uzidi kuoga na matope na kupoteza uungwaji mkono kutoka jumuia za kimataifa? .
Ulishawahi jiuliza? Kwanini utekaji akifanyiwa mpinzani shutuma hutupiwa TISS na Polis lakini akifanyiwa mwanaCCM hawahusishwi Polis au TISS?
Yote haya huenda wafuasi wa pande mbili wanatiana ADABU. Greenguard na Redbrigadia zitupiwe jicho.
Na
@jini_kinyonga