Mengi yazidi kuibuka kuhusu Nyalandu

Mengi yazidi kuibuka kuhusu Nyalandu

Ni kweli,na ndio hao hao Wamarekani walimwambia agombee urais wa Tanzania wakati wa mchakato wa kumpata Rais wa awamu ya 5.
Lakini pia kuna jambo la msingi la kujiuluza,kwanini sasa?au ni kwa sababu Nyalandu ametoa msimamo wake kuhusu kuanzishwa upya kwa mchakato wa katiba ya Warioba?
Kweli CCM ni donda Ndugu,kupona kwake kunahitaji kudra ya mwenyezi Mungu.
 
Ivi yule twiga aliyekatiwa visa na passport then akapewa VIP seat kwenye ndege mnamkumbuka???
Naomba mniambie atakapokuwa amerudishwa....................???

Mana ili ni jipu lililoivaa na linaitaji kutumbuliwa bila ganzi....???

Nimemkuta Dubai kwa mwanamfalme amenawiri,sijui kama ni rahisi kurudi mbuhani Bongo maana Via yake imeisha na hajashtakiwa kwa kosa la over stay!
 
Lakini ndio wizara zenye funika kombe mwanaharamu apite hii ndio chama cha Machafuko aka ccm

Punguza siasa kemea mafisadi kwa majina sio kwa vyama vyao!, Hiyo njia ilishindwa toka enzi za Lyatonga Mrema. Hata kama una wadhifa wa kichama ndani ya cdm angalia unapotoka! Punguza propaganda za vyama tukemeee mafisadi
 
Natamani Donald Trump ashinde urais America aje kututawala watanzania. Haiwezekani nchi iwe na madudu kiasi hiki still tuseme tuna viongozi.
Hii inaonyesha jinsi gani hatuna kiasi wala aibu katika mambo tunayoyafanya. Yaani kila kiongozi Ukimchunguza utakuta anamtandao wa ujambazi dhidi ya maliasili za nchi hii.,
I am tired of these people
 
ni kweli nyalandu aligawa vitalu bure kwa marafiki zake wamarekani
 
Natamani Donald Trump ashinde urais America aje kututawala watanzania. Haiwezekani nchi iwe na madudu kiasi hiki still tuseme tuna viongozi.
Hii inaonyesha jinsi gani hatuna kiasi wala aibu katika mambo tunayoyafanya. Yaani kila kiongozi Ukimchunguza utakuta anamtandao wa ujambazi dhidi ya maliasili za nchi hii.,
I am tired of these people
Nihatari sana na inasikitisha sana sana alafu unatumbua chunusi wakati mabusha yapo
 
I wish Tanzania ingekuwa kama Kenya.Mh.Magufuli inawezekana yaliyosemwa ni kweli au uwongo......Uchunguzi ufanyike na ukamilike kwa muda mfupi ....one week inatosha.Ukianza na huyu utapandisha morale ya wananchi katika kuijenga nchi yao upya.
 
Nchi hii imefujwa sana na wakubwa....!! Dah... kibali cha kuwinda wa nyama pori 700 bila malipo!!!! Mia saba jamani!!!
 
Punguza siasa kemea mafisadi kwa majina sio kwa vyama vyao!, Hiyo njia ilishindwa toka enzi za Lyatonga Mrema. Hata kama una wadhifa wa kichama ndani ya cdm angalia unapotoka! Punguza propaganda za vyama tukemeee mafisadi
Namuunga mkono mleta mada..Lakini ni kama bado yuko kwenye kampeni.
 
Dah?!aisee vingine ni vitezi dume siyo vijipu inahitaji upasuaji wa operation siyo utumbuaji tena
 
Tanzania inanishangaza sana hakuna eneo la taaluma ambapo hakuna makapi!??? kazi ya waandishi kama hawa ni kujenga au kubomoa jamii????

Baada ya kusoma hii habari nimechukua muda mrefu sana kwanza kufuatilia na kupata uhakika na taarifa sahihi za maswala yote yanayohusu uwindaji wa kitalii (yaani uwindaji wa wanyamapori). Sijajua lengo la huyu mwandishi lilikuwa nini haswa lakini kuna kila dalili kuwa anatumiwa either kuchafua serikali au mtu au kampuni fulani. Mimi sipo huko, hata hivyo kazi yangu hapa ni kusema ukweli wote jinsi ulivyo sio ili nimtie aibu mwandishi ila nifute ule ujinga wa fikra ambao ameupandikiza ndani ya vichwa vya watu kwa kuweka taarifa hii.

Kwanza nimebaini kuwa leseni za uwindaji wa wanyamapori hutolewa kwa mtindo wa "hunting package" ambazo idara ya wanyama inawauza katika msimu wa uwindaji. Idadi na aina ya wanyamapori wanaoorodheshwa kwenye leseni ya uwindaji inakuwa determined na idadi ya siku ambazo inaweza kuwa siku saba, kumi na nne au siku ishirini na moja. Kwa kadiri mtalii anavyokubali kununua package ya siku nyingi na idadi na aina ya wanyamapori anaopewa pia inaongezeka. Sasa ifahamike kuwa uwindaji wa kitalii sio shopping ya supermarket ambayo unaenda unakuta wanyama kwenye shelf wanakusubiri uwawinde, its a business of probability ni swala la chance. unaweza kukaa porini kwa siku 21 na usipate mnyama unayetaka au upate wachache chini ya 15% ambayo umelipia. In most cases kulingana na wataalamu wa hiyo fani wanasema haijawahi kutokea mgeni akaweza kupiga wanyama wote anao orodheshewa hata hivyo itamlazimu kuwalipia wote.

Hao watu wanaotajwa kuwa walipewa kibali cha kuwinda wanyampori 700 kimsingi walikuwa wageni 7 jumla kila mmoja akiwa na leseni moja hivyo kufanya leseni saba, mbili leseni zao ziliwaruhusu kuwinda kwenye maeneo nane tofauti tofauti .

Kwa kawaida kibali cha raisi hutolewa bure lakini kwa vibali vinavyotajwa taarifa za uhakika ni kuwa vililipiwa kiasi kisichopungua 38,000US$. Hizi ni habari nilizozipata idara ya wanyamapori na kujiridhisha baada ya kuona baadhi ya nyaraka ikiwa ni pamoja na hati ya malipo ya serikali. Kwa mujibu wa sheria za wanyamapori (Wildlife Conservation Act #5 of 2009 - Tourist hunting regulations za 2010) zinasema wazi kuwa mtalii akishawinda hulazimika kupeleka mrejesho wizarani baada ya kumaliza uwindaji na pia wakati wa uwindaji wanapokuwa porini uwindaji wowote unafanyika chini usimamizi wa maafisa wa idara ya wanyamapori ambao hu record kila mnyama anaye windwa na mgeni na kuweka alama ya tick na kurekodi vipimo vya mnyama aliyewindwa katika karatasi maalumu. Nimethibitishiwa na kuona kuwa walifanya hivyo na hizo taarifa wala sio za siri. Nimefanikiwa kuona huu mrejesho, kwa jumla ya leseni zote saba idadi ya wanyama waliowindwa ni 8 tu kati ya wanyamapori 700 waliopo kwenye leseni zote ijapokuwa wanyama wote walilipiwa.

Swali ninalojiuliza ni kuwa mwandishi wa habari hizi alikuwa na nia gani na kwanini hakufanya jitihada za kuchunguza kwasababau haijanigharimu lolote mimi kufuatilia na kujua ukweli wa hizi ni taarifa ambazo zinapatikana kwa urahisi kabisa idara ya wanyampori.

Hapa naona mambo mawili; kwanza ni maslahi binfasi na pili ni swala la kisiasa zaidi. Ni vyema basi waandishi wetu wakafanya uchunguzi wa kutosha wa taarifa zao kabla hawajazitoa magazetini na kuishia kupotosha umma badala ya kuwapa wananchi ukweli.

Nchi hii imefujwa sana na wakubwa....!! Dah... kibali cha kuwinda wa nyama pori 700 bila malipo!!!! Mia saba jamani!!!
 
Back
Top Bottom